FAHAMU NAMBA KIBIBLIA NA MAANA ZAKE KATIKA ULIMWENGU WA ROHO NA MWILINI

NAMBA NA MAANA ZAKE KIBIBLIA.
Utanguizi.
Tunapoendelea kujifunza maneno ya Mungu, Leo nimepewa fulsa ya kujadiliana kuhusu Namba ndani ya biblia na maana yake katika maisha yetu ya kimwili na Kiroho hapa Duniani..Namba ndani ya biblia zimewekwa na Mungu na tunatakiwa kuziangalia kwa umakini wake sana kama vile maneno(text) tunavyoyatumia.Tumepewa na Mungu kanuni ya kulinganisha mambo ya Kiroho na Roho(1Wakoritho 2:13) Na inatuonesha ya kwamba Biblia na yaliyomo ndani yake ni sehemu ya mambo ya Kiroho.Na tunajua ni lazima tutafute na kujua kwa namna gani Mungu anazitumia namba. Biblia ni kitabu sahihi kabisa hakina makosa wote tunafahamu na yamevuviwa na Mungu (pumzi ya Mungu). Vilevile Namba ni sehemu ya Maneno kwa maana nyingine tunasema ndani ya maneno kuna namba. Mungu ameweka maneno yake ndani ya biblia kiasi kwamba hata mtoto mdogo wa miaka 6 anaweza kuelewa kwa usahihi kabisa kama mtu mzima kama Mungu anavyotaka. Ni kweli Biblia ni kama msitu unaweza potelea huko na usiweze kuelewa lakini kwa msaada wa Roho mtakatifu tunaweza kuelewa ukweli wote wa biblia (Mark 4:11-12;Mithali 25:2;1Wakori. 2:11-14).
Jambo la msingi hapa ni lazima uelewe kwanza kwamba Namba ni maneno (Numbers are words) ndipo utakapo zitumia namba vizuri bila shida kama maneno.
Sasa kwa nini kwa nini  ? Ni kwa ni nadra sana kuona somo hili likifundishwa
Si kwamba namba zote ndani ya biblia zina maana flani ila kwa madhumuni maalum kwa mfano;
1              .Namba zinaweza kutumika katika kupima muda (Kutoka 12:40)
  1. Namba zinaweza kutumika kuelezea kundi fulani la watu,madhumuni mbalimbali na nk(1petro 3:20).
  2. Namba zinaweza kutumika kupima kitu Fulani(Mwanzo 6:15).
  3. Namba zinaweza kutumika kwa maana Fulani na kwa wakati huohuo maana ya Kiroho au Alama Fulani(Yohana 21:11) samaki 153 waliovuliwa hawa ni samaki halisi waliovuliwa lakini Namba 153 pia ina maana maalum Kiroho lakini imejificha sana kwenye uelewa wetu.
  4. Kwa wakati mwengine namba zinaweza kuwa na maana ya kiroho au alama Fulani yenye kutambulisha kitu Fulani.
Kwa mfano ,Petro alimuuliza Yesu ni mara ngapi mtu akikukosea unaweza kumsamehe hata mara saba?(Mathayo 18:21)
Na yesu akajibu sio mara saba tu lakini hata sabini mara saba. Sasa 70 x 7 = 490 je Yesu alifundisha tusamehe mara 490 halafu tuwache kumsamehe mtu? Na tunajua Yesu alitufundisha tuwasamehe watu kama yeyey alivyotusamehe sisi bure, Na tunafahamu ya kwamba Yesu hakusamehe mara 490 pale msalabani.Alipokufa pale msalabani alisamehe watu na dhambi zao zote bure (Mark 2:5-12;Yohana 8:10-11;Wakolosai 2:13) kwa hiyo 70×7 ina maana ya Kiroho zaidi kwamba kusamehe hakuna mwisho (completeness cycle) hata leo Yesu anasamehe ukitubu na kuacha dhambi zako.
  1. Namba kubwa ugawanjwa vipande vipande (by using factors) vya namba ndogo ili kuona maana yake Kiroho. Mfano 490 = 70 x 7, 153 = 3x3x17. Namba (3) ni kusudio la Mungu ,Namba (17) kuwapeleka mbinguni wale waliookoka wakati wa mwisho.
Namba ndani ya biblia hazipo kwa bahati bahati tu bali zina makusudio maalumu kuwekwa hapo.Kwa kifupi na tuanze kujadili Namba moja moja ina maana gani au ishara gani Kiroho.
Namba 1
Hii ni namba ya Mungu. Mungu ni mmoja ni yeye peke yake hakuna Mungu mwingine.
 Namba 2
Namba 2 ni Namba ya wale waeneza Neno la Mungu (Wainjilishaji) Kwa mfano Yesu aliwatuma wanafunzi wake 70 “Wawili wawili”(Luka 10:1). Ufunuo 11 tunaona wale Mashaidi 2 waliouwawa na baadaye wakafufuka kutangaza Neno la Mungu. Matendo 13, Paulo na Barnabas walipelekwa pamoja kama Wamisionari wa kwanza kutangaza neon la Mungu. Kwa hiyo Namba 2 kama ina maana Kiroho au ina alama fulani basi kwa wale wasambaza neno la Mungu Wainjilisti na watu wengine waoeneza neon la Mungu kwa njia moja au nyingine. (Nimefanya utafiti kwa ku angalia miaka na tarehe ya kuzaliwa na katika maisha yao kwa ujumla namba 2 inajitokeza sana )
Namba 3
Namba 3 Ni Kusudio la Mungu/Kusudi la Mungu kwa mfano wakati wa tukio zima la kusulubiwa kwa bwana Yesu Lilikuwa ni kusudio la Mungu mwenyewe.Kumbuka kulikuwa na Misalaba 3(Marko 15:27) Petro alimkana Bwana Yesu mara 3(Marko 14:66-72) Mitume 3 walikuwa pamoja na Bwana yesu pale bustani ya gethsemani(marko 14:33),Bwana Yesu aliomba mara 3 mle Bustanini(marko 14:32-41),Jina “YESU WA NAZARETH MFALME WA WAYAHUDI” Liliwekwa msalabani kwa lugha 3 (Yohana 19;19-20) makundi 3 Makuhani, Viongozi wa dini na waalimu na Wote walitaka Yesu asurubiwe(Mathayo 26:59)nk.Vilevile kuna Namba inaweza kujitokeza katika namba kubwa lakini zikiwa sawa na 3 kama Yuda alipewa vipande 30 kumsaliti Yesu(Mathayo 26:15), Kulikuwa giza masaa 3 kutoka saa 6 mpaka saa 9, 12, 27 nk (mathayo 27:45).Kwa matukio yote hayo hii namba 3 inayojirudirudia ni kwa bahati mbaya au ni kwa kusudi maalum? Namba 3 hapa inatuonyesha kwamba tukio lote la kusulubiwa kwa Bwana Yesu ilikuwa kwa Makusudi ya Mungu (purpose of God/willing of God) Fikilia kukiwa na mashaidi wawili watatu basi neno lidhibitike, pakiwa na wawili watatu na Mimi Mungu nipo pamoja nao.
 Namba 4
Namba 4 inamaanisha dunia nzima (Ulimwengu) (worldwide) Biblia inatabua kwamba kuna pande 4 za dunia Mashariki,Magharibi,Kaskazini na Kusini (zaburi 107:3). Biblia Inazungumzia pepo (winds) 4 za dunia (Mathayo24:31) na inatambua kuna pande 4 za dunia (Ezk 7:2).Kwa hiyo kama namba 4 inamaanisha alama yeyote au maana yeyote Kiroho basi inatambulisha Dunia au Ulimwengu kwa ujumla.
Vilevile namba 4 iamaanisha ukamilifu wa jambo linapofikia mwisho kabisa (hitimisho la jambo) kwa mfanoYesu alisubili mpaka siku 4 Lazaro alipokufa kabla yakufufuliwa (Yohana 1:15-17) Mfalme Jehu’aliruhusiwa kutawala kizazi cha 4 (2Wafalme 10:30,13:1,9-10,14:16,2915:8-18) Israeli walikaa utumwani mpaka kizazi cha 4 baada ya kutumikishwa miaka zaidi 400 (Mwanzo15:13-16).Abraham alinunua kipande cha ardhi kwa ajiri ya kumzikia Sarah mkewe kwa shekeli 400 (Mwanzo23:15) Kwa hiyo kwa maaana hii Namba 4 vivile ina maana ya utimilifu wa kitu au mwisho wa kitu ktk muda, kwa kipidi Fulani. hata kumaanisha Mwisho wa dunia (2Petro 3:10).
Namba 5
Namba 5 ina maanisha Wokovu au Hukumu.Yesu alipata hukumu ili tupate Wokovu kwa hiyo usishagae namba 5 ikiwakilisha Wokovu au hukumu kwa wakati mmoja .Namba 5 inaonekana ½. Namba ya 10, 5 inawekuwa kama 5 50 500 5000 nk. Unaweza kufikiria ushuru wa hekalu ulikuwa shekeli 5(kutoka 30:13) au wale watu 5000 aliowalishwa chakula Bwana Yesu (Yohana 6:10-13) au unawea kufikiria wale wanawali 5 wapumbavu na 5 wenye busara (mathayo 25:1-2) nk .kwa hiyo kama namba 5 ni alama au maana fulani ya Kiroho basi ni hiyo yaWokovu au Hukumu.
Namba 6
Kama namba 6 inamaanisha alama au maana yeyote Kiroho basi itakuwa inamaanisha KAZI. Mungu alitumia siku 6 kuumba ulimwengu (kutoka 20:11).Namba 666 katika Ufunuo 13:18 ni Wasiookolewa walio kwenye mikono ya shetani wakijitahidi kupata haki mbele ya Mungu.
Namaba 7
Namba 7 inatumika sana kwenye biblia katika maana ya Ukamilifu wa Ki Mungu (Completed cycle) (siku7, miaka7) kama kusamehe ni 70x7times maana yake kusamehe hakuna mwisho samehe samehe samehe……Vile vile namba hii 7 inatabulika kama na namba ya Mungu. Ukiomba kitu chochote katka Mungu mara 7 hakika Mungu atakupa jibu.(Tatizo letu tunamchagulia Mungu majibu, Majibu mengine hatutaki na tunaendelea kuomba kwa hasara).Kwa mfano Ukuta wa babeli ulidondoka baada waisrael kusunguka mara 6 na mara 7 ukuta kukadondoka.Naamani aliambiwa akajichofye mara saba na baada ya hapo ukoma ukapona kabisa.
Namba 8
Namba 8 ni 2×4 au 2x2x2 maana yake ni mchanganyiko wa maana ya namba 2 na namba 4.
 Namba 9
Namba 9 ni 3×3.kwa hiyo maana yake ni sawa na namba 3
Namba 10
Namba 10 ni sawa na namba 1inaweza kuwa 10, 100, 1000, 10000…. Nk. Namba 10 ina maanisha Ukamilifu kamili. Biblia inasema kuhusu sarafu 10(luka 15:8), Kondoo 100 (luka 15:4) miaka 1,000 (2Petro 3:8),Vizazi 1000 (Kumb.7:9)etc.kwa hiyo kama namba 10 ni alama ya jambo fulani au ina maana fulani kiroho basi ni Ukamilifu.
Namba 11
Namba 11 inatumika katika biblia inamaanisha mapungufu katika usahihihi (defective fullness). Kwa mfano kulikuwa na makabila 12 (lakini halisi ni 13) ya waisraeli, lakini Daudi alipofanya sensa Mungu alisungumzia Makabila 11(1wafalme 11:31-32).Wakati Yuda aliyekuwa mmoja kati ya Wanafunzi wa Yesu 12 (Yohana 6:70-71) alijiua baada ya kumsaliti Yesu, Walibakia Wanafunzi 11, Baadaye alichaguliwa Mtume mwingine kuchukua nafasi yake na kuwa 12 tena.(Matendao 1-13-26). Kwa hiyo namba 11 kama ina alama yeyote au maana yeyote kibblia basi ni Usaliti.
Namba 12
Kama namba 12 ni alama au ina maana yeyote kiroho basi ni Utimilifu katika muonekano Kwa mfano kulikuwa na Makabila 12 na Mitume 12, Mji mtakatifu una urefu wa 12000 mara 12000 mara 12000 (Ufunuo 21-16)nk. Kwa hiyo kama namba 12 ina maanisha alama au ina maana Kiroho basi ni Utimilifu katika muonekano.Namba 7,10,12 zote zinafanana kila moja kama utimilifu wa kiroho isipokuwa ikiambatanishwa na namba zingine kama 2×6,2x2x3 nk..
 Namba 13
Namaba 13 kama ina maanisha alama au maana fulani ya Kiroho basi ni Hakika ya Utimilifu. Biblia inasungumzia Mitume 12, Lakini hakika kabisa ni 13. Wa 13 ni Mtume Paulo aliposisitiza akiwa katika katika roho Mtakatifu kuwa amekidhi matakwa/Vigezo vyote vya kuwa Mtume kama wale 12.(1Wakoritho9:2;15:8-9; 2Wakoritho12:11-12) Biblia kwa kawaida kabisa inasungumzia Makabila 12 ya Israel lakini Uhakika na kimsingi Yalikuwa Makabila 13(Mwanzo 49:1-28;Hesabu 32:33;Joshua 16 na Joshua 17) Namba 13 ina maanisha Uhakika wa Ukamilifu.
Namba 17
Inaonekana sehemu nyingi katika biblia ikisimama kwa maaana ya Mbingu/uungu (Heaven) Kwa mfano katika miaka 17 ya mwisho ya maisha yake Yakobo chini ya Yusufu ambaye ni mtoto wake kipenzi ambaye alisalitiwa kama alivyosalitiwa Yesu wakati alipotumika badala ya Mungu kuwaokoa na njaa kali (Mwanzo 47:28)Yeremia alininunua shekeli 17 kuwanunulia wana wa israel kipande cha ardhi kuonyesha kwamba Mungu amewarudisha tena kwenye nchi yao.Kipande kile kilikuwa kinamaanisha Ufalme wa Mungu umewarudia tena (yeremia 32:9) Kwa hiyo namba 17 kama ina alama au maana ya Kiroho ni mbingu/ Uungu (heaven).
Namba 37
Kama ilivyo namba 23 zinamaanisha Hukumu ya Mungu.Nuhu alikuwa kwenye Safina kwa muda wa siku 370 wakati mungu alipo hukumu dunia(Mwanzo 7:11;8:14-18).Jehsi la Sennacherib liliangamizwa na Mungu kwa usiku mmoja watu 185,000(2Wafalme 19:35) 185,000 = 5x37x1,000.Namba 666, ambayo ni namba inamaanisha watu wasiookoka wali chini ya hukumu ya Mungu(Ufunuo 13:18) kama namba hiyo ukiivunja vunja katika namba ndogondogo ni 3x6x37.Kwa hiyo Namba 37 kama ina alama au maana yeyote Kiroho basi ni Hukumu..
 Namba 40
Namba 40 inajirudiarudia katika biblia ikimaanisha Mwisho wa majaribu/Majaribu.Musa alikaa siku 40 katika Mlima Sinai(Kutoka 24:18), Huku nyuma Wana wa Islael walijaribiwa na kushindwa kuvumilia na kutengeneza miungu yao(Kutoka 32:1-4).Israel walikuwa Jangwani kwa kipindi cha miaka 40 walishindwa na hakuna aliyeokolewa wote hawakufika Kanani isipokuwa watoto wao amabao waliozaliwa baada ya kutoka Misri.(Waebrania 3:17).Yesu alijaribiwa na shetani siku 40 mchana na usiku (Mathayo 4-1-2:Luka 4:1-2) pamoja na majaribu hayo tunamshukuru Mungu kwamba Yesu hakushindwa alimshinda shetani (Mathayo 4:3-11;Luka 4-3-14) Kwa hiyo kama namba 40 inamaanisha alama au maana yeyote Kiroho basi ni Majaribu. Fikiria watu wengi wakifikia umri wa miaka 40 shida na masumbufu huwa yanakwisha na hili kila mtu anaweza kujichunguza au kuchunguza hata kama maisha ya mtu huyo ni ya kimasikini lakini amani na utulivu unakuwepo katika maisha yake( Focus on Future destenity) Utu uzima ni miaka 40. Chunguza 40 zinavyotumika katika maisha na kwa jamii kwa ujumla hizo ni maana za kiroho kumbuka!
Namba 43
Namba 43 ina maana ya Hukumu au Wokovu.Kwa mfano Israel walikaa Misri kwa miaka 430.Mwisho wa miaka hiyo 430 hHukumu ilishuka kwa Wamisri na Uhuru Wokovu kwa kwa Israel). Kwa hiyo namba 43 kama inamanisha alama au maana Kiroho basi ni Hukumu au Wokovu.
Ndugu mpendwa Mungu akubariki na tilia maanani somo hili litakusaidia na wakati mwingine kukuonyesha njia. Unaweza patwa na shida au jambo Kumbuka Mungu anazungumza kupitia Namba. Kwa nini 3 kwa nini 7,2,5,10 nk..Mungu anapozungumza na wewe anaweza kukuonyesha ishara mbalimbali za namba kati jambo fulani katika maisha yako kiroho. Vilevile kumbuka si kila namba ina maana ya kiroho.
Kuna baadhi ya dini na madhehebu huwa wana utaratibu wa kuhesabu hesabu vitu Fulani kama ushanga na nk hata kwa wachawi na waganga huwa wanahesabu hesabu kwa namna Fulani ili kupata namba na maana zake kwenye mambo yao ya kichawi. Nimekwambia hayo ili uweze kujua kwamba katika namba kuna siri kubwa kiroho kwetu sisi tulio okoka na kwa wale wasio mwamini Bwana Yesu.
Asante Mungu akubariki tuombeane

Comments

Popular Posts