DELIVERANCE FROM THE POWERS OF DARKNESS

KUKOMBOLEWA KUTOKA KATIKA NGUVU ZA GIZA

Nikusudi la Mungu mwanadamu aishi maisha mazuri na yakumpendeza yeye,tena Mungu alimuweka mwanadamu kuwa mtawala katika ulimwengu huu ambao Mungu aliuumba ila tu mwanadamu alipoteza nafasi hiyo baada ya kufanya dhambi (Yer.5:25)lakini Mungu kwa neema yake na upendo wake alimtuma Mwanawe wa pekee Yesu Kristo awakomboe wanadamu(Yoh.3:16) nakuwapatanisha na Mungu na hivyo kuirudisha nafasi ile ambayo Mungu alimuwekea mwanadamu ila shetani kwa ujanja  wake aliichukua(Mwanz.3:13)
Fuatana nami  katika mafundisho haya,tafakari kwa kina kisha chukua hatua
Ukisoma katika Uf.12:17 utaona kuwa shetani amekasirika dhidi ya mwanamke na amedhamiria kufanya vita juu ya uzao wa mwanamke lakini hasira yake ni juu ya wale wazishikao sheria za Mungu na wenye ushuhuda wa Yesu (Ebra.12:1); nia yake ni atawale kizazi cha mwanamke,wale wasiompinga hana hasira nao maana wanakuwa chini yake (Ef.2:1-3).
Katika Mwanzo 3 tunaona kuwa Wazazi wetu wa kwanza,adamu na hawa,walimkabidhi shetani dunia waliyopewa na Mungu (2Kor.4:3-4), hivyo basi shetani akatumia hila na uongo (Yoh.8:44) ili awafunge waweke patano/mkataba nao
Shetani ni mwerevu mwenye ngazi ya kimalaika,kumbuka hapo mwanzo alikuwa malaika mwenye cheo kizuri huko Mbinguni(Isa.14:9-17),anafahamu tabia za Mungu na mambo yote mazuri ambayo Mungu ameyaweka kwaajili ya mwanadamu ndio maana alitaka kumpindua Mungu akashindwa na badala yake amekusudia kumpotosha mwanadamu ili asipate yale ambayo Mungu ameweka kwaajili ya wanadamu
Kumbuka mwanadamu nizaidi ya malaika ndio maana malaika hakupewa kutawala na Mungu isipokuwa mwanadamu(Mwanz.1:26, 1Kor.6:3).
Shetani naye anatamani kuabudiwa na kuogopwa na mwanadamu ndio maana anafanya yote haya(Isa.14:13); biblia inasema shetani alipambana na malaika,hivyo mwanadamu peke yako huwezi kupambana naye  isipokuwa ukiwa na Nguvu za Mungu na kwa kumkubali Yesu katika maisha yako maana yeye ni Jemedari wa vita(Rum.10:9-10).
Shetani anaelewa kwamba Mungu ni wa maagano,na agano linadumu kizazi hata kizazi (Torati 8:18,Zab.102:12) Shetani anafanya mbinu za kuwadanganya wanadamu wapuuze mkataba wao na Mungu halafu anawashawishi kuanzisha mkataba mpya nao(2Tim.2:26)
Shetani baada ya kuiteka dunia kutoka kwa Adamu na Eva aliweka mtandao wake kabambe wenye ‘programs’ ili ashinde,ana ‘administration’ yenye vyeo mbalimbali,mfano Ef.6:12,Ef.2:3
  • Falme na mamlaka
  • Wakuu wa giza hili
  • Jeshi la pepo wabaya
Shetani alipomjaribu Yesu alimuonyesha milki hizo na alitaka Yesu amsujudie lakini Yesu alimshinda(Luka 4:5-13).
Mfano wa program za kishetani ni kutambika mizimu,ibada za sanamu,uzinzi n.k.(1Kor.6:9-10)
Kizazi kinapoanza kumdharau Mungu na kuingia mikataba mingine na shetani laana inaanza kutembea kwa kasi mfano;laana ya magonjwa,umaskini na ‘abnormalities’ zisizotibika (Kut.20:5)
Laana inarithiwa kama vile ambavyo Baraka inavyoweza kurithiwa,Kutoka 20:1-6, Mungu aliamua laana itembee,agano linapowekwa si rahisi kulivunja, Gal.3:15,Yer.6:16-20
Nimuhimu pia kufahamu baadhi ya aina za laana kama ifuatavyo;
  1.  Laana zitokazo kwa Mungu zisababishwazo na kwenda kinyume na sheria za Mungu     Tor.11:26-29
  2. Zitokanazo na watumishi wa Mungu  Mk.11:20-24,Mdo.13:8-12, 2Waf.5:20-27, 1Waf.16:34, Josh.6:26-27
  3. Laana za mahusiano
i) Mtu kujilaani mwenyewe Mwn.27:24-25
ii) Kumtendea mtu mwingine uovu Mwn.4:9-11
iii)Mzazi kwa mototo Mwn.31:22-29 (kumbuka laana isiyo na sababu haimpati mtu)
iv)Mtu kujiunganisha na nafsi nyingine,hapa kuna njia nyingi kwa mfano;
  • Kuchanjiana damu
  • Kwa njia ya zinaa
  1. Laana zenye mkono wa ibilisi au kupitia wajumbe wake mfano;kwa njia za matambiko,kwenda kwa waganga n.k
Kumbuka milango ya madhabahu za shetani;
  • Kupewa majina ya waaguzi na wachawi
  • Kupewa majina mabaya
  • ibada za ndoa za kienyeji
  • kuchanjwa na wajumbe wa shetani
  • kutoa vitu kwa mganga au kutumia vitu vilivyotolewa kwa mganga
  • kuvaliana nguo
  • kutoa mimba
Matokeo ya laana ni;
v  Magonjwa yasiyotibika
v  Ndoa zinazovunjikavunjika,kutokuolewa au kuoa ktk koo
v  Mimba kuharibikaharika
v  Watu kujinyonga au vifo visivyoeleweka ktk ukoo
v  Vifo vinavyofanana ktk ukoo
v  Hali ya kichaa au mataahira ktk ukoo
v  Ukoo kusambaratika na kuchukiana
v  Roho za zinaa,ulevi n.k ktk ukoo

Haya ni baadhi tu ya mambo ambayo yanaweza kukusaidia umetoka wapi,uko wapi na unakwenda wapi au unatakiwa kufanya nini katika maisha yako ya kimwili na kiroho pia,hivyo basi;

Nini chakufanya:
  1. Kumbuka swala la kumpendeza Mungu na kwenda Mbinguni ni lako binafsi (2Kor.13:5)
  2. Mungu hakukuumba uishi maisha ya taabu bali ya raha na ya kiutawala (Mwanzo 1:26)
  3. Baadhi ya laana na mikataba ya giza unaweza kuivunja kwakusema kwa kinywa chako maneno yaliyo kinyume na mikataba hiyo na kuamua kuachana nayo kabisa (Rum.10:9-10, Mat.12:37, Mith.18:21).
  4. Kuzivunja laana na mikataba/maagano ya giza na kukubali kumpokea Yesu katika maisha yako,Damu yake iliyomwagika Msalabani inatakasa laana na maagano yote kwa agano jipya ktk damu yake takatifu,na jina la Yesu ndilo pekee linaloweza kuvunja laana na kukuweka huru (Mat.4:12,Fil.2:9-10,Mat.1:21)

Comments

Popular Posts