OMBA NA RUHUSU MUNGU AONEKANE KUPITIA NAFASI AU KITU ULICHONACHO
MATHAYO 14:13-21
Katika mistari hii tunaona habari za Bwana Yesu akiwalisha watu zaidi ya elfu tano kwa mikate mitano na samaki wawili tu. Kabla ya yote yatupasa kutambua kwamba kuna uhusiano mkubwa kati ya Mungu na mwanadamu hasa katika utendaji kazi. Mungu humtumia mwanadamu pia kuweza kudhihirisha nguvu zake na ukuu wake lakini wakati mwingine ni lazima pia tumruhusu Mungu ili aweze kujidhihirisha kwetu na kwa wengine pia.
Mambo yafuatayo ambayo yote tunayapata katika mistari hiyo hapo juu ni muhimu kuyazingatia ili Mungu aweze kuonekana:
1. KUWA NA FARAGHA NA MUNGU (SPEND TIME WITH GOD);
Ukianza mstari wa 13 utaona kuwa baada ya kusikia hayo(habari za kuuwawa Yohana mbatizaji) alikwenda faragha(kuongea na Mungu-kuomba). Je mimi na wewe tuna faragha na Mungu?
2.MAONO (VISION);
Wanafunzi walipoona muda umeenda walimfuata Yesu nakuongea kuhusu watu kula na kulala badae; waliona mbali. Je unayo maono kwaajili ya maisha yako na Mungu pia?
3.IMANI (FAITH);
Yesu anawaambia wanafunzi wawape wao chakula kwakua aliamini inawekana kwa imani, kumbuka imani ni kuona kile usichokiona. Je unayo imani dhabiti inayomruhusu Mungu aonekane?
4.TUMIA ULICHONACHO (USE WHAT YOU HAVE);
Mikate mitano na samaki wawili vilionekana kidogo kwa wanafunzi lakini mbele za Mungu vilikua vingi. Kidogo ulichonacho waweza kukitumia na Mungu akaonekana, kumbuka hata Musa alikuwa na fimbo tu mkononi lakini Mungu alionekana katika bahari ile ya shamu.
5.SHUKRANI (THANKS GIVING);
Kumshukuru Mungu kwa kidogo ulichonacho hufungua milango ya Mungu kuonekana kwa vikubwa pia. Yesu alichukua mikate mitano na samaki wawili akaibariki na kushukuru kisha muujiza ulitendeka. Je unamshukuru Mungu kwa ulichonacho?
6.TATHMINI (SELF EVALUATION);
Bwana Yesu aliwauliza wanafunzi wake ‘watu wanasema mimi ni nani? Wakamwambia wengine husema Yohana mbatizaji,wengine nabii yule n.k. Yesu alikuwa akijifanyia tathmini. Baada ya watu kula na kushiba walihesabiwa wanaume pale wakawa elfu tano na makombo vikapu 12, hiyo ilikuwa tathmini! Je unayo nafasi ya kujifanyia tathmini mbele za Mungu ili kudhihirisha nguvu zake?
Mungu atusaidie katika kumdhihirisha yeye kwa nafasi na vitu alivyotupa!

Comments
Post a Comment