MAJARIBU/VISHAWISHI

Majaribu ni moja ya mambo makubwa ambayo wana wa Mungu kikamilifu wanapitia ,yamkini wengine inaonekana   wanashawishiwa  sana kuliko wengine. Hakuna mtu hata mmoja ambaye hawezi kuzuia au kujiepusha asipatwe na majaribu, Adam, Lucifer na Yesu walijalibiwa.

Mungu ametufunza kuuweka huu mgawanyo katika maisha yetu ya kila siku ya kusali. “usitutie majaribuni /vishawishi,  lakini utuokoe kutoka dhambini”
Baadhi ya Mitume wakubwa walisumbuka sana kwa sababu walifikiri kushawishi au jaribu ni lazima liwe ovu/uovu au baya. Lakini kushawishiwa au kujaribiwa siyo dhambi, dhambi ni kukubali kishawishi au kishawishi kinaposhinda au akikubaliana nacho.
Ushindi katika kishawishi kimoja unaweza kukusaidia kushinda na vishawishi vingine.
Hatuwezi kuwazuia ndege kuruka au kupaa angani juu ya vichwa vyetu, lakini tunaweza kuwazuia ndege hawa kuweka makazi au viota vyao kwenye nywele zetu; hatuwezi kuzuia mawazo ya dhambi katika fikra zetu, lakini tunaweza kuyazuia mawazo au fikra za dhambi kuweka makazi kwenye ufahamu wetu  na fikra zetu.
Mtu mmoja alimwuliza swali msichana mdogo kuwa anafanya nini majaribu au vishawishi vikija? Akajibu, “majaribu au vishawishi ni kama shetani abishaye hodi moyoni mwangu, na nikimwona shetani anabisha hodi, namwita Yesu aje afungue mlango”  Shetani anaganda na kutoweka anopomwona mwenye nguvu na mamlaka ya ushindi pale Kalivali (calvary).  Yesu anapoongea katika Yakobo  1:12 Heri mtu astahimiliye majaribu ……..,  i.e, anakataa majaribu na kuwa mshindi kwa kupitia damu ya Yesu Kristo aliyoimwaga msalabani.
1.Korinto  10:13., “Jaribu halikuwapata ninyi isipokuwa lililokawaida ya wanadamu ila Mungu mwaminifu ambaye hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo, lakini pamoja na lile jalibu atafanya na mlango wa kutokea ili mweze kustahimili.

1.CHANZO CHA MAJARIBU.
1.1 Mungu huruhusu ;
Hayatoki kwa Mungu , Yakobo 1;13 mtu ajaribiwapo asiseme, ninajaribiwa na Mungu, maana Mungu hawezi kujaribiwa na maovu, wala yeye mwenyewe hamjaribu mtu., kwa mfano Ayubu, Mungu alimpa shetani ruhusa ya kumjaribu Ayubu, lakini kwa kiwango Fulani tu. Ambacho Mungu aliruhusu. (Ayubu 1:12, 2-6)
1.2  shetani-   Mathayo  4:3., shetani alimjaribu Yasu Kristo.
1.3  Mwili- Yakobo1:14., Lakini kila mmoja hujalibiwa na tamaa yake mwenyewe huku akivutwa na kujidanganya.
Hii inaonekana katika Nyanja kuu tatu;
  1. Tamaa ya mwili., -1:Yohana 2:16
  2. Tamaa ya macho., -1: Yohana 2:16
  3. Kiburi cha maisha ., -1:Yohana 2:16
1.4  Marafiki waovu ., -Mithali 1:10., “Mwanangu mwenye dhambi akikushawishi wewe usikubali”
1.5   Wakristo marafiki., -Mathayo 16:22,23., “…….Nenda nyuma yangu shetani wewe……” Yesu alimwambia Petro.
2. SABABU YA MAJARIBU.
2.1   Ni mtihani/kipimo kwa imani yetu., Yakobo 1:2,3., ndugu zangu hesabuni ya kuwa ni furaha tupu ya kuwa mkiangukia katika majaribu  mbalimbali, mkifahamu ya kuwa kujaribiwa kwa imani yenu huleta saburi…,
Dr.Hardema katika hadithi yake ya shirika la reli lililokuwa linajari abiria        wa daraja jipya mlimani., mara gari moshi mbili zikawasili kwa kasi kubwa darajani na kuzifunga breki zake kwa ghafla, zile injini za gari moshi zikapita darajani kwa mwendo wa taratibu kwa muda wa saa. Daraja likabaki vilevile  na wataalamu wakajua daraja lile  linaweza kuhimili vitu vizito.
Kwasababu Yesu alipata majaribu makubwa  hapa Duniani anaweza kutusaidia mara tujaribiwapo.
2.2   Ni mtihani kwa utii wetu., Mwanzo 22:1.-      “…ikawa baada ya mambo hayo Mungu alimjaribu Ibrahimu akamwambia .,  Ee  Ibrahimu ! …… umchukue mwanao, mwana wako  wa pekee, umpendaye Isaka ……. Ukamtoe sadaka ya kuteketezwa…...”  Mungu anawajaribu watu kujua upendo wao na uaminifu  na utii, Tunasema kirahisi sana kuwa tunampenda Mungu  ya kuwa tutamtii katika hali zote, kwa hiyo wakati mwingine inabidi tujaribiwe ili kujua kweli tuyasemayo tuna maananisha.’
. 3. WIGO WA MAJARIBU/KIWANGO CHA MAJARIBU
1:Korintho 10:13.,  “….hatawaacha mjaribiwe kupita mwezavyo” Mungu anajua wigo wa uwezo wetu,anajua jaribu gani tunaweza kuhimili. yenye uzito zaidi hayaruhusiwi kupita  kwenye hilo daraja mpaka yapunguze uzito. Mungu anapunguza majaribu  yaendane na uwezo wa mtu kwa namna mbalimbali.
A.- Anaweka muda wa hilo jaribu .,- anajua kama ni ndani ya saa moja au zaidi tunaweza kulishinda jaribu.
B.- Anaweka muda  wa jaribu kuanza .,-Anaruhusu  jaribu kwa muda ambao tuko tayari kukabiliana nalo.
C.- Analinda mawazo yetu na nguvu zetu majaribu yanapoanza.,-Macho yake  yanatuangalia kila dakika na tunapofikiria kushindwa na jaribu na kuanguka dhambini yeye anafungua mlango wa kutokea ndani ya hilo jaribu.

    
4.NJIA AU MITINDO YA MAJARIBU.
  1. Kwa kupitia umaskini,- Mithali,30:9 “…..wala nisiwe maskini  sana nikaiba,na kulitaja bure jina la Mungu wangu”
  2. Kwa kupitia mafanikio- Mithali 30:9 “Nisije nikashiba nikakukana nikisema Bwana ni nani”.
  3. Kwa kupitia utukufu wa kidunia- Hesabu 2:17 “maana nitakufanyizia heshima nyingi sana”
  4. Kwa kukata tama-Zaburi 42:11 “Nafsi yangu kwanini kuinama na kufadhaika ndani yangu? (Falme 19:4)
5.JINSI YA KUSHINDA MAJARIBU
  1. Kwa kumuamini Mungu.1 Korinto 10:13, Muhubiri 3:10 “…..atafanya na mlango wa kutokea ili muweze kustahimili”. Tunatakiwa kumwamini Mungu 1Korinto 1:9,Mungu habadiliki.
  2. Kwa kutumia neno la Mungu kwa usahihi- Yesu ameongelewa mara tatu katika Mathayo 4.
  3. Kwa maombi binafsi- Mathayo26:48 “ kesheni muombe msije mkaingia majaribuni”
  4. Kuwa huru- 2 Timotheo 2:22 “lakini zikimbieni tama za ujanani” Mithali 4:14,15 “usiingie katika njia ya waovu wala usitembee katika njia ya wabaya”
  5. Kwa kukataa.Yakobo 4:7 “Basi mtiini Mungu ,mpingeni shetani,naye atawakimbia”
  6. Kwa  kukubali njia ya kutokea- 1 korinto 10:13.

Comments

Popular Posts