Mahusiano kwa vijana kuelekea ndoa!

Kumekuwa na theology nyingi sana kuhusu kuanzisha mahusiano, ambazo nyingi ni za uzoefu wa watu binafsi hasa wasiona MUNGU, au wale wanaofuata DINI tu. Nitajaribu kuzungumzia kwa kirefu zaidi kuanzisha mahusiano kwa vijana waliookoka kutakuwa na contents zifuatazo
– Mahusiano kwa vijana wasiookoka na athari zake
– Mahusiano kwa vijana waliookoka
– Maandalizi kabla ya uchumba au ndoa kwa vijana wa kike na wakiume,
– Hatua za mwanzo kabla ya uchumba
– Kupata mchumba toka kwa BWANA
– Dhana ya upendo
– Utaratibu wa kanisa katika hatua za uchumba, n.k
Lakini Kwa ufupi nielezee kuhusu mahusiano yasiyo na MUNGU.
1. *MAHUSIANO KWA VIJANA WASIOOKOKA NA ATHARI ZAKE:*
Vijana wengi ambao hawajaokoka huwa hawana hofu ya Mungu ndani yao, hivyo wanakuwa na maamuzi yoyote kuhusu kufanya dhambi, ikiwa ni pamoja na kufanya ngono pasipokupata hukumu ndani ya dhamiri zao, Sababu yake kubwa BIBILIA inasema kwamba dhamiri zao zimekufa kwani wamesha kuwa wafu japo watembea. Matakwa Yao wenyewe yasiyo na kujali kuwa hili ni kosa mbele za Mungu au si kosa ndio wanayafanya.
*KUFUATA MATAKWA YAO NA ATHARI ZAKE:***
*Uharibifu na magonjwa:*
Kuna uharibifu mkubwa ambao hujitokeza katika mahusiano ambayo hufuatwa na vijana wasio na hofu ya Mungu.
– Kupata mimba katika umri mdogo na kukatishwa masomo (wasichana)
– Kupata magonjwa ambayo hutokana na zinaa, kama vile (Ukimwi), n.k.
*Kukosa mwelekeo sahihi:*
– Pindi vijana wanapokatishwa masomo, hukosa mwelekeo sahihi wa maisha yao. Na hata baadaye wanapokuwa hawana elimu, huishia kujiingiza katika makundi mabaya.
– Kujiingiza katika (ukahaba) kwa kujiuza miili yao na hata kupata mahitaji yao (wasichana).
– Kujeruhiana baada ya kuchokana kimapenzi kwa kuachana bila taratibuKupata watoto wa mitaani
– Kuanzisha mahusiano mengine na msichana au mvulana mwingine hatakama hawajatarakiana. Na mengine mengi sana
– Kujiingiza katika makundi mabaya ya uvutaji bangi na utumiaji wa madawa ya kulevya na vitendo vya ujambazi na matokeo yake ni kifo.
1. *MAHUSIANO KWA VIJANA WALIOOKOKA*
*(Mungu ndiye Mhusika mkuu)*
Vijana wengi waliookoka, huishi maisha matakatifu ambayo humpendeza Mungu. Na pia hujiepusha kujiingiza katika vitendo vya kumchukiza Mungu Kama walivyo watu wa mataifa. Hasa pindi ambacho tamaa katika miili yao hazijaanza kuamshwa. Japo kuwa wengine wameokoka wakiwa katika umri mkubwa na waliishi isipositahili lakini wakiokoka YESU huingia ndani yao na kuzichukua zile kiu za dhambi zao.
* [Waefeso 4:22-24, inasema, Mvue kwa habari ya mwenendo wa kwanza utu wa zamani,unaoharibika kwa kuzifuata tama zenye kudanganya.(23) Na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu. (24) Mkavae utu mpya,ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli.
* *Kuna mambo mengi ambayo kama vijana tuliookoka tunatakiwa kujiepusha
nayo, ili tusije tukaingia katika majaribu na kuangukia dhambini kingono.
i. *Simu za Mikononi*:
Simu za mikononi, ni jambo moja wapo ambalo linaweza kuchangia mabinti tukawa na uhusiano wa karibu sana na kijana wa kiume na matokeo yake kuvuka mipaka na kumsahau Mungu, mfano, tunaweza kujikuta tunatumiana message za kutaniana na baadaye ule utani ukaanza kuleta hisia tofauti baina yetu na baadaye tukaunda kitu, na tukaamua kufanya kweli.
* ii. **Matumizi ya mitandao ya internet.*
Hili ni janga kuu na ni kubwa sana, maana vijana wengi wamekuwa wakidanganyika kwa kuangalia picha ngono kwenye mitandao na video za ngono kwenye simu na casseti. Hivyo hili linatupasa kujiepusha Sana, ili lisitujengee akili dumavu(ukiangalia picha chafu hizo utaishia kwenye kujichua, na kujichua kunaharibu akili kwa asilimia 90%, EPUKA). pia Matumizi mabaya ya Facebook, na technology nyingine zinazokuwa kwa kasi kubwa kabisa kwa sasa.
iii. *Kwenda kuhudumu vijana wa jinsia tofauti mkiwa wawili: *
* *Tunaweza tukawa na ukaribu sana kama kaka na dada, na baadaye tukaanza kwenda kuhudumu/kushuhudia pamoja ,na itafikia hatua tutazoeana na hata kutaka kuwa na muda wa kukaa pamoja na kujifunza neno na hata kuomba pamoja, labda nyumbani kwa kijana wa kike au kijana wa kiume. Na matokeo yake tukaanza kuwa na hisia tofauti na kuona kuwa tunapendana na kuwa (tumeona maono) tutakuja kuoana, au binti akawa na hisia tofauti na kuhisi kuwa kijana wa kiume anampenda wakati sivyo. Na baadaye ikionekana kuwa yule kijana anachumbia mtu mwingine, yule binti ataumia sana na matokeo yake kuamua kuacha wokovu. Na pia tunapoenda kushuhudia inatakiwa kuwa watu watatu au zaidi ,akiwepo mmoja wa jinsia tofauti na wawili wa jinsi moja ni nzuri zaidi.Au wote tukawa jinsia moja.Hiyo inaleta ushuhuda mzuri kwa wale tutakao kuwa tunawashuhudia neno la Mungu, hawatakuwa na maswali mengi kuhusiana na sisi.Pia kukutana kwenye hotels/ hostel au mahali pa kificho kwa ajili ya kujadili huduma au appointment huku ukijua mtakuwa wawili, au kusafiri kikazi na mwanamke/mwanamme asiyeokoka au ameokoka na mkapanga HOTELI MOJA, hapo ni hatari sana.
* iv. **Binti kujiachia kwa mvulana kupita kawaida:
* *Binti aliyeokoka anatakiwa kutumia akili katika uhusiano wake na vijana wa kiume. Sawa kuwa na kaka mpendwa siyo mbaya ila inatakiwa ukaribu wetu usivuke mipaka [Mfano,utaona binti anamzoea sana kijana (kaka) na kufikia hatua kumtembelea kijana katika chumba chake anachokaa.Na hata kuanza kumsaidia kazi za ndani kama vile kudeki,kupika na hata kufua kwa kigezo cha (mpendwa).Huko ndiko binti kujiachia kwa mvulana.Kwa sababu unapoenda kwake na yeye anaishi peke yake unategemea nini? Na yeye ni mwanadamu kama wanadamu wengine anahisia kama wanaume wengine japo kuwa ameokoka, kufanya kwako hivyo hata kama ulikuwa hauna nia mbaya kutomuingiza majaribuni kijana huyo. Na matokeo yake yatakuwa mabaya na machukizo mbele za Mungu
(kuanguka dhambini kingono, tena mtaanza na kukumbatiana, then kubusiana baadae ulimini). Vyote hivyo havistahili kutajwa kwa watakatifu wa Bwana.
* v. **Uhuru wa kuchangamana na kutoka pamoja kaka na dada mkiwa wawili (outing):*
* *Tukiwa vijana tuliookoka,tunatakiwa kuangalia mambo ambayo yanaweza kutuangusha katika dhambi. Kitendo cha kutoka outing si kibaya (kama wapendwa) ila inatakawa kuwa zaidi ya watatu.Utaona kaka na dada wanatoka na kwenda, labda beach na si ajabu anaenda kwa nia nzuri tu ya kubadilishana mawazo na hata kupunga upepo ila ,shetani ni mjanja sana, pindi wakiwa ufukweni wanaweza kuwaona watu wakiwa na (wapenzi) wao. Labda wanashikana shikana na hata kula mate (romance). Na wao wakiwa kama wanadamu wenye hisia kama wanadamu wengine lazima ile hali wataiweka katika vichwa vyao. Na hata wakiwa wanaenda mara kwa mara na kuendelea kuiona ile hali,itafikia hatua watashawishika na kufanya hivyo kama wengine wafanyavyo, na matokeo yake ni kuangukia dhambini.
* vi. **Mahusiano ya kadi za Valentine kwa kaka na dada ni kinyume na mapenzi ya Mungu: *
* *Ni vijana wengi tuliookoka pindi ifikapo siku ya Valentine,tunajishughulisha kwa kununua kadi na maua na kupeana, kama kaka
na dada. Na bila kujua nini maana ya siku ya Valentine na ilitokana na nini.Inatakiwa kabla ya kufanya kitu tuangalie kwanza mwanzo wake ni nini? (Mf. Tunasherehekea Chrismas kwa sababu tunajua mwanzo wake ni nini, tunapeana kadi na hata zawadi pia ikibidi) lakini sherehe ya valentine inahusiana na Uzinzi, kama tukifuatilia mwanzo wake tutajua hilo.Vijana tuliookoka tunatakiwa kufanya mambo ambayo ni mapenzi ya Mungu si kuiga tu mambo ya dunia hii.Na matokeo yake kutumiana kadi na maua (kaka na dada), inakuja kuunda kitu tofauti kabisa katika akili zetu na mwisho wake ni kuangukia dhambini.
* vii. **Kujiepusha kuingia maeneo yasiyo husika:*
* * Sisi kama vijana tuliookoka inatakiwa tuangalie sehemu ambazo tunaingia, mf ,Utakuta kijana aliyeokoka anaingia Night clubs, Casino .n.k. Na sehemu kama hizo mara nyingi uasi mkubwa hutendeka na matokeo yake shetani anaweza kukushawishi na ukaangukia dhambini na kufwatisha uasi huo.Kwa hiyo sisi kama vijana tuliookoka tunatakiwa tuangalie sehemu za kuingia siyo kila sehemu ,sisi tunaingia.Na mwisho wake tunaweza kumtenda Mungu dhambi.
* viii. **Kuzoea kuingia kwenye vyumba vya Wasichana au Wavulana:*
* *Mazoea ya binti kuingia kwenye vyumba vya wavulana na kukaa kwenye kitanda cha mdada, si jambo jema na hata mvulana kuingia kwenye chumba cha binti si jambo jema na si heshima.Inatakiwa tuheshimiane sisi kwa sisi .Na si kwamba siyo heshima tu, bali tunaweza kujikuta tunaangukia dhambini kutokana na mazoea kama hayo.
* ix. **Kuwa na Boyfriend na Girlfriend, mara nyingi inapelekea vijana wengi dhambini:*
* *Kwa habari ya kuwa na Girlfriend au Boyfriend, ni kweli wakati bado hatujampokea Bwana Yesu kuwa Bwana na Mwokozi wa Maisha yetu,wengi wetu tulikuwa nao.Lakini inashangaza na kusikitisha na hata leo katika Kanisa la Kristo vijana tuna kuwa na tabia kama ya mwanzo ambayo tuliishazizika. Na matokeo makubwa ya kuwa na uhusiano huo, mwisho wake ni kuangukia dhambini. Kwa hiyo sisi kama vijana tumtumikie Mungu,wakati ukifika Bwana atafanya njia na atatupa waume na wake kutoka kwake. Na watakuwa baraka
katika maisha yetu.
Katika mahusiano yetu sisi kama vijana tuliookoka inatupasa kutunza ushuhuda wa Bwana wetu Yesu Kristo.

Comments

Popular Posts