Siku ya JUMAPILI, ambayo ndiyo siku ya
kwanza ya juma, SIKU YA BWANA aliyoshinda mauti na kufufuka [UFUNUO1:10]
Tunaitenga maalum kumwabudu Bwana kwa sababu:-
a) Ni sikukuu ya malimbuko ya mavuno
ambayo ilifanywa katika Agano la Kale, SIKU YA PILI baada ya Sabato;
Ikiwa ni utabiri wa Kristo ambao ni LIMBUKO lao waliolala
[WALAWI23:9-14;1WAKORINTHO15:20].
b) Ni siku ya ushindi ya Bwana wetu Yesu
aliyofufuka, na kujidhihirisha kwa wanafunzi wake baada ya kufufuka kwa
Yesu [YOHANA 20:1,19,26 WARUMI 10:9].
c) Siku ya kuja Roho Mtakatifu,
Mwangalizi mkuu wa kazi yote ya Mungu katika kanisa, ilikuwa siku ya
Pentekoste ambayo ni Jumapili, siku ya pili baada ya sabato [MATENDO
2:1]
d) Siku ya Pentekoste, Jumapili ndiyo
siku ya kwanza ambayo kanisa la kwanza lilianza mahubiri na watu 3,000
wakaokoka na kuanza kusanyiko la kwanza la Ibada kanisani [MATENDO 2].
e) Wakristo wa kanisa la kwanza walikusanyika Jumapili [MATENDO 20:6-12;1WAKORINTHO 16:1-2].
Sababu hizi, zinadhihirisha pia wazi wazi kwamba kuabudu Jumapili hakukuanzishwa na mfalme CONSTANTINE wala kanisa Katoliki.
Hakuna andiko lolote linalosema mtu
yeyote anayeabudu Jumapili ana alama ya 666 ya mnyama. Huo ni uzushi.
Biblia inatupa uhuru wote katika kuchagua siku ya kumwadhimisha Bwana
[WARUMI14:5-6]. Vilevile ni muhimu kufahamu kuwa siku zote ni siku za
kujifunza Neno [MATENDO 17:11;2:46].
KUSHIKA SIKU, SIYO NJIA YA KUOKOKA
Kushika siku yoyote hata iwe Jumapili,
sio njia ya kuokoka.Tunaokolewa kwa kumuamini Yesu kuwa ni BWANA na
MWOKOZI na sio kwa kushika siku yoyote [WARUMI 10:9-10,13]
Comments
Post a Comment