SABABU ZA KIBIBLIA KWA NINI USIWE MGONJWA
Kati ya mambo ambayo yanampa 
mwanadamu wakati mgumu katika kipindi chake cha kuishi hapa duniani ni 
swala la kukosa afya…kuwa na udhaifu au kuwa na ugonjwa katika mwili 
wake.
Ukisoma Biblia inazungumzia 
habari ya uumbaji wa Mungu hapo mwanzo, na haioneshi hata sehemu moja ya
 kuwa Mungu aliumba magonjwa,udhaifu au mateso kati ya vitu alivyoumba. 
Magonjwa ni matokeo ya anguko la mwanadamu, alipokubali kutomtii Mungu 
na kumsilkiliza shetani. Akauza haki yake ya kumiliki na kutawala katika
 maeneo yote (ikiwemo afya).Akamuuzia Shetani haki ya kuwa ‘mungu wa 
dunia hii’ japo Mungu alimuumba mwanadamu awe ‘mungu wa dunia hii’…yaani
 awe mwenye kauli ya mwisho hapa duniani kwa niaba ya Mungu aliye hai.
Hata baada ya anguko la 
mwanadamu, bado Mungu aliweka ‘plan B’ ya urejesho wa kile 
tulichokipoteza kwa kutokutii kwetu…akaweka SHERIA, KANUNI na TARATIBU 
ambazo kama zikifatwa kwa usahihi na mwanadamu zitamtoa pale alipo na 
kumrejesha katika ‘KUMILIKI NA KUTAWALA’ japo si kwa urahisi na wepesi 
kama kabla ya anguko.
Nilipokuwa ninayapitia maandiko 
kwa muda wa miaka karibu 9 sasa tangu nilipopata ‘NEEMA’ ya kumjua Yesu 
kama BWANA na MWOKOZI wangu binafsi…Mungu amenifundisha ‘kweli’ nyingi 
sana na mojawapo ni hii ya kuwa na ‘AFYA TIMAMU’…Sababu hizi saba za 
kibiblia zinaeleza ni kwanini uwe na afya timamu(out of sickness and 
disease phase)…Zinafanya kazi katika maisha yangu…NA HAKUNA WAKATI 
WOWOTE NINAWEZA KUWA MGONJWA…HAIWEZEKANI NA HAITATOKEA…ni sehemu ya 
Mpango wa Mungu kwa maisha ya kila mmoja wetu…si kwangu tu…wala kwa 
baadhi ya watu wenye ‘IMANI KUBWA’ au ‘UPAKO’ sana. Ni kwa ajili yako na
 ni sasa….!
Ebu tuanze kuzichambua kweli hizi saba, kwa Jina la Yesu:
 1.KAZI YA MSALABA
Kama unamwamini Yesu we si mgeni 
wa neno hilo hapo juu…ina maanisha kufa na kufufuka kwa Yesu…na matokeo 
yake chanya juu ya maisha yetu.Wengi tunajua Msalaba umetupa kuwa wana wa Mungu, watu wa nyumbani kwa Mungu,umetupa Uzima wa milele,umetupa msamaha wa dhambi nk
Lakini hatuko tayari kukubali 
kwamba msalaba huohuo umeleta “AFYA YA KIMUNGU” ndani yetu! Biblia ktk 
1Petro 2:24 inasema, “Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu MWILINI 
MWAKE juu ya mti ili tukiwa hai kwa mambo ya haki tuwe wafu kwa mambo ya
 dhambi, NA KWA KUPIGWA KWAKE TULIPONYWA” Haisemi tunaponywa au 
tutaponywa…inasema ‘TULIPONYWA’  Andiko lingine linatoka katika Mathayo 
8:17, “Yeye mwenyewe(Yesu) aliuchukua UDHAIFU wetu, amejitwika MAGONJWA 
yetu’…kama ameyachukua magonjwa yetu, kwanini sisi(Wakristo) 
tunayang’ang’ania? kama amejitwika magonjwa yetu kwa nini sisi 
tunalazimisha kujitwika Magonjwa? Utamsikia Mkristo aliyeokoka tena 
kajazwa na Roho wa Mungu lakini anasema…’Yaani hiki kichwa changu 
kinauma kila mara tangu nikiwa mdogo’…mwingine anasema…’Hili tatizo la 
kubanwa na kifua ni la familia yetu, hata mama naye analo…’ huku ni 
kujaribu kukana kile ambacho Yesu alishafanya MSALABANI…ALIYEKUSAMEHE 
DHAMBI ZAKO NDIYE ALIYEKUPONYA….”Akusamehe maovu yako yote akuponya 
Magonjwa yako yote” Zab 103:3
Kama unamwamini Yesu…tena kwa 
moyo wako wote na unasema wewe ni raia wa mbinguni na unadai ya kuwa 
Mungu ni baba yako…HURUHUSIWI KUWA MGONJWA, DHAIFU hata mara moja…tembea
 katika afya timamu tangu sasa kwa Jina la Yesu wa Nazareth.
 2.WEWE NI NYUMBA YA MUNGU (MAKAO YA MUNGU)
Biblia inasema ya kuwa unapompa 
Yesu maisha yako na kumwamini, unakuwa ndani yake na Yeye ndani yako 
wewe, na pia MWILI wako unapata ‘HADHI’ au ‘HESHIMA’ ya kuwa 
NYUMBA/MAKAZI YA MUNGU ALIYE HAI….”Je hamjui ya kuwa MIILI yenu ni 
hekalu la MUNGU, na ya kuwa ROHO WA MUNGU anakaa NDANI yengu?” 1Kor 
3:16-17, 1Kor 6:14-19
Biblia inaeleza ya kuwa Mungu 
anakaa sasa ndani ya MWILI wako…kwenye CELLS, TISSUE,ORGANS na System za
 mwili wako….Je unadhani vimelea vya MAGONJWA vitaweza kuishi katika 
uwepo wa Mungu uliotuama ndani yako…unaotiririka ndani yako? HAIWEZEKANI
 NA HAITAWEZEKANA
 3.UKO NDANI YA YESU
Biblia inasema katika 2Kor 5:17 
ya kuwa “Hata imekuwa mtu akiwa ndani ya Kristo Yesu, ya kale yamepita 
na tazama yote yamekuwa mapya” Tangu siku ile ulipompa Yesu maisha 
yako…uliingia ndani yake!
Huo ndo ukweli wa mambo hata kama shetani anajitahidi kukuzuia usilifahamu hili.
Kama ni hivyo, ebu tembea na 
Ufunuo huu alionipa Mungu nilipokuwa ninafundishwa hili…Ili Ugonjwa 
uweze kukufikia wewe unapaswa kwanza umtoboe Bwana Yesu, kisha ndio 
ukufikie na ukupate…kwa hiyo unaamini kuna ugonjwa wenye nguvu ya 
kumtoboa Bwana Yesu? achilia mbali kuusogelea tu uwepo wake…KUWA NA AFYA
 NI SEHEMU YA MAISHA YAKO NDANI YA YESU.
 4.UMEZALIWA KWA NENO LA MUNGU
Biblia inasema ya kuwa tulio 
ndani ya Yesu, tumezaliwa mara ya pili(tumeokoka) kwa Neno la Mungu…Soma
 1Petro 1:8, Yakobo 1:8… kwa maneno mepesi tu wana wa NENO LA MUNGU….na 
Biblia inasema ya kuwa NENO ni MUNGU (Yohana 1:1-3)…na kama unataka 
kupiga hatua yoyote kubwa kiroho au kimwili ni lazima ulitumie NENO na 
uliishi NENO, yaani uliweke NENO kwenye matendo (Yakobo1:21-24)
Mithali 4:20-22 Inasema, 
“Mwanangu yasikilize maneno yangu, tega sikio usikilize kauli zangu, 
zisiondoke machoni pako, uzihifadhi moyoni mwako, maana ni UHAI kwa 
walio nazo(waliozishika) na AFYA ya mwili wao wote”
 5.KUMTUMIKIA MUNGU
Biblia katika KUTOKA 23:25-26 
inasema, “NAWE UTAMTUMIKIA BWANA MUNGU WAKO; NAMI nitakibarikia chakula 
chako na kinywaji chako…SITATIA JUU YAKO MAGONJWA YOTE niliyotia juu ya 
Wamisri(wasioamini)…kwa maana mimi ni BWANA MUNGU NIKUPONYAYE”
Kama unataka kufurahia afya 
timamu wakati wote hauna budi kuwa na muda wa kutosha wa kumtumikia 
Mungu, kwa nguvu zako, fedha au mawazo yako. Na kama ukiwa na bidii 
katika hili utayapiga teke Magonjwa maishani mwako…Utafurahia AFYA YA 
KIUNGU kila iitwapo leo!
 6.UMEINGIA SAYUNI NA YERUSALEM WA MBINGUNI
Ukisoma katika Isaya 33:21-24 
utaona ahadi za ajabu walizonazo wale wanaoishi katika Sayuni…amani, 
usalama, kumiliki,nk lakini zaidi ni ile iliyoko mstari wa 24 isemayo, 
“Wala hapana MWENYEJI wa mji huo atakayesema mimi Mgonjwa”…yaani watu wa
 Sayuni hawana habari ya magonjwa maana Mungu ndiye Mfalme wao na pia 
ndiye mtetezi wao!
Ukisoma Waebrania12:22 Biblia 
inasema ya kwamba sisi(tuliokombolewa na Yesu) tumeufikiria mlima Sayuni
 na Yerusalem wa mbinguni, mji wa Mungu aliye hai, ambako kuna majeshi 
ya malaika (malaika wa vita/wapiganaji) maelfu elfu…Huku ndiko tuliko, 
ambapo Mungu ni baba yetu… na sie ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu 
wa NYUMBANI KWA MUNGU(Waefeso2:19)
Kama uko ndani ya Yesu, unaishi Sayuni, na HAURUHUSIWI KUWA MGONJWA…maana hapana mwenyeji hata mmoja atakayesema mimi mgonjwa!
 7.KAA UWEPONI MWA BWANA
Zaburi 91:1-16 Inasema “Aketiye 
uvulini(uweponi) mwa aliye juu atakaa salama…Hauaogopa TAUNI(UGONJWA WA 
MLIPUKO)iliyo gizani  wala UELE uharibuo adhuhuri…ijapokuwa watu elfu 
wataanguka(waakufa kwa sababu ya Magonjwa) mkono wako wa kushoto, naam 
kumi elfu mknono wako wa kuume,lakini hautakukaribia wewe…maana Bwana 
atakufunika kwa manyoya yake na chini ya mbawa zake utapata kimbilio…”
Ukitaka kuongeza miaka yako ya 
kuishi, ukitaka kuwa na Afya ya Kiungu, kulindwa na Nguvu za Mungu, 
kustawi, kutukuzwa na kuinuliwa na Mungu, yote haya yako katika UWEPO 
WAKE.
Lazima ujifunze kukaa mbele za 
Bwana, kupitia maombi, kulisoma NENO, Kumtafakari Mungu, kwa Kusifu na 
kwa kuabudu pia…TUMIA MUDA WAKO MWINGI UWEPONI KWA BWANA.
Ni maombi yangu kwa BWANA kwamba 
Mungu aliye hai atayafungua macho ya moyo wako, na Nuru ya Kristo 
itang’aa ndani yako mara tu umalizapo kuusoma ujumbe huu…Ni ujumbe wa 
Mungu kwako!
Wako katika Ndani ya Kristo Yesu
Comments
Post a Comment