"Your life style affects you more than your prayers"


"21 Mjue sana Mungu, ili uwe na amani; Ndivyo mema yatakavyokujia. 22 Uyapokee, tafadhali, mafunzo yatokayo kinywani mwake, Na maneno yake yaweke moyoni mwako.23Ukimrudia Mwenyezi, utajengwa; Ukiuondoa udhalimu mbali na hema yako. 24 Nawe hazina zako ziweke mchangani, Na dhahabu ya Ofiri iweke kati ya mawe ya vijito; 25Naye Mwenyezi atakuwa hazina yako, Atakuwa ni fedha ya thamani kwako. 26Kwani ndipo utakapojifurahisha katika Mwenyezi, Na kuinua uso wako kumwelekea Mungu. 27Utamwomba yeye naye atakusikia; Nawe utazitimiliza nadhiri zako. 28 Nawe utakusudia neno, nalo litathibitika kwako; Na mwanga utaziangazia njia zako. 29Hapo watakapokuangusha, utasema, Kuna kuinuka tena; Naye mnyenyekevu Mungu atamwokoa. 30Atamwokoa na huyo asiye na hatia; Naam, utaokolewa kwa sababu ya usafi wa mikono yako." (Ayubu 22:21-30)

Katika maombi kuna nguvu na ushindi. Maombi ni silaha, njia ya kupata mahitaji yetu na kuinuliwa, lakini MAOMBI yetu hayana maana kama TUNAISHI (enenda), yaani kuwaza, kunena na kutenda KINYUME na tuombavyo! kwa maana imeandikwa "imani bila matendo haizai" (Yakobo 2:20). 

Angalia hapa, watu wengi wanadhani WANAFANIKIWA sana kwa sababu wameomba! Sawa, hiyo ni sehemu tu, lakini nakwambia leo, ukichunguza maandiko yanazungumzia habari ya utaua, kumcha Mungu, kumjua Mungu, kumpenda Mungu, mtu mwema, nk. Maombi ni muhimu na LAZIMA, ila maombi bila matendo yako ni sawa na kujaza maji kwenye gunia, halitajaa kamwe. Je! waweza kuomba ukafanikiwa pasipo imani? na je! unaweza kusema unaimani pasipo matendo (mwenendo wa imani)?

Mmoja atasema, "maombi ni jambo la kwanza kabla ya matendo", nami nasema, "huwezi kutenganisha maombi na matendo, ila cha kwanza ni matendo yako". Ndipo Yakobo aksema, "nioneshe imani yako kwa pasipo matendo nami nitakuonesha kwa matendo" (Yakobo 2: 18), je! Atendaye kwa sababu anaamini si mkuu kuliko aombaye bila kutenda? Angalia tena, kinachokuathiri zaidi ni mwenendo wako au maombi yako? 

Ukiangalia katika Ayubu 22:21-30 utaona msisitizo wa maisha (lifestyle) na KIU ya ndani ya kumjua Mungu SANA, ndipo mema yatakapokujilia. Ukizidi kusoma utaona habari ya KUJENGWA kama utamrudia Mwokozi. Je! utajuaje kama haya yamo ndani yako? Dalili ya kwanza, angalia kiwango chako cha maombi?Jiulize, wewe ni mwombaji? Imekupasa kuomba angalau mara kadhaa kila siku na angalau kwa dakika chache, au unakumbuka kuomba wakati wa chakula na kulala, au ukibanwa na shida tu? Pili, angalia kiwango chako cha kusoma Neno. 

Ukiona unasahau kusoma neno hadi wiki inapita, jua ile HAMU ya "kumjua Mungu sana" haipo. Tatu, je! kuna uhusiano wa IMANI yako na maisha ya KILA SIKU? Yaani katika biashara, shule, na mambo ufanyayo, je! iko hofu ya Mungu? kwa lugha nyingine, je! kuna mambo huwezi kufanya kazini kwako kwa sababu tu unamcha Mungu? Je! kwa maisha yako tu bila kusema neno na kushuhudia, watu watajua kwamba umeokoka? Je! yupo atakayevutwa kwa BWANA au KUMSHUKURU Mungu kwa ajili ya matendo yako? Je! wajua kwamba Injili ni mfumo wa maisha na wala sio kuhubiri tu?

Sasa ufanyeje kama umepungua katika hayo? Kwanza, Toba ya kweli, Pili, Omba BWANA akurudishe tena katika njia zake, soma neno na litafakari kila siku, mchana na usiku. Anza kufanya yakupasayo (mwenendo wa Kitaua), hapo utaona faida kubwa.

Comments

Popular Posts