KUMTAFUTA NA KUMWITA MUNGU KWA BIDII KTK MAISHA YETU.
Maandiko matakatifu yanatuasa tuite jina la Bwana Mungu wetu
wakati tukiwa kwenye shida na raha. Yeye husikia na hujibu maombi yetu. Imekuwa
kawaida kwa wanadamu kumhitaji ama kujisogeza karibu na Mungu wakati wa shida
tu. Na mara shida zikiisha humsahau Mungu. Mwanadamu husahau kuwa anatakiwa pia
kumuita Mungu akiwa katika raha na mwenye furaha.
Kama maandiko matakatifu yanavyosema Bwana yu karibu na wote
wamwitao. Anasema wote wamuitao kwa uaminifu atawafanyia mambo makuu. Sasa basi
unamuiteje Mungu? Haijalishi kuwa
unajua kusali ama la, kwa maana watu wengi wana mashaka kuwa si rahisi kumuita
Mungu kwa kutaja tu jina lake akaskia. MUNGU ANASKIA NA KUJIBU HATA KABLA
HUJAMUAMBIA SHIDA YAKO. Kuita kwa kutaja jina lake YESU! YESU! YESU! Inatosha
kabisa, waweza kusema ASANTE YESU na yeye anasikia. Soma Zaburi
145: 18-19 ikuongoze katika hili.
Mungu anasema “Niite name nitakuonyesha mambo makubwa na
magumu usiyoyajua” (Yeremia 33:3) Yamkini
umepitia katika mapito mengi na mambo magumu ambayo yanakufanya uogope na kuwa
njia panda usijue la kufanya, yeye anaweza yote. Mwite na atakuitikia. Ukuu
wake ni wa ajabu na matendo yake mengi hushangaza watu.
Jifunze kutumia muda wa faragha na unene na Mungu. Mueleze
shida zako na hali zako za namna tofauti unazopitia naye atakuwa pamoja nawe. Soma Isaya 58: 9 ikuongoze katika hili.
Vifungu vingine vya Biblia ambavyo vinatuongoza katika kujua
kumuita Mungu ni Mathayo 7:8, Wathesalonike 5:17 na Soma Yohana yote kwa ufunuo zaidi. Ni lazima
kujifunze kuomba bila kukoma na kumshukuru Mungu kwa kila jambo. Hakika Mungu
ni mwema kwa sisi wanadamu.
Mbarikiwe mpaka mshangae!
Comments
Post a Comment