MWONGOZO WA KUOKOKA NA KUMRUDIA MWENYEZI MUNGU.
WOTE TUMETENDA DHAMBI.
Warumi 3:23. Kwa sababu wote wamefanya dhambi na kupungukiwa
na utukufu wa Mungu.
Kama jinsi maandiko yanavyothibitisha hapo juu, kutokana na
mwenende wa maisha yetu tunamkosea Mungu. Hii ni kwa sababu tunaishi kwa
kutimiza tamaa na mapenz ya mwili, lakini waliookolewa kwa damu ya Yesu Kristo
hawatendi dhambi na wanahesabiwa haki kwa imani.
MSHAHARA WA DHAMBI.
Warumi 6:23. Kwa maana mshahara wa dhambi ni mauti; bali
karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu Bwana wetu.
UNAWEZA UKAOKOKA PIA.
Yohana 3:16. Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu,
hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima
wa milele.
Maandiko hapo juu yanatueleza wazi, kuwa njia pekee ya
kuupata uzima wa milele ni kwa kumuamini Yesu Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.
Na pia hakuna atakye ingia mbinguni pasipo kupitia Yesu Kristo.
Yohana 14:6. Yesu akamwambia, Mimi ndimi njia, na kweli, na
uzima; mtu haji kwa Baba, ila kwa njia ya mimi.
Na siyo kwa kuamini tu, ni lazima ukiri kwa kinywa chako
kuwa Yesu Kristo ni Bwana na Mwokozi wa maisha yako. Ukikiri kwa nia ya dhati
kutoka ndani ya moyo wako, unapokea wokovu.
Warumi 10:10. Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata
haya (ya wokovu), na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu.
Sasa tamka sala ifuatayo kwa imani kabisa, na Mungu anatakusamehe na kukupa wokovu.
“Ninakiri ya kwamba Yesu Kristo u Bwana na Mwokozi wa roho
na maisha yangu. ulikufa msalabani ili uniokoe, ninaomba unirehemu na unitakase
makosa yangu muda huu ninapotubu”.
Amini, umeokoka sasa. Yesu Kristo ameingia katika maisha
yako, unachotakiwa kufanya sasa ni kukua katika kumjua Yesu Kristo na Mungu
kupitia mafundisho ya Biblia.
2 Petro 3:18. Lakini, kueni katika neema, na katika kumjua
Bwana wetu na mwokozi Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hata milele.
Kwa kuwa sasa ni Mkristo mpya, tafuta kanisa au kusanyiko
linalohubiri wokovu karibu nawe. Hakikisha unatafuta kanisa au kusanyiko linalomuhubiri
Yesu Kristo wa Nazareti.
"Na Mungu wa mbinguni aishiye milele, akubariki sana. Amina".
Comments
Post a Comment