Shalom Wependa. 
Jamani kuna shuhuda nyingine si tu 
zinasisimua/leta raha rohoni mara tu uzisikiapo lakini pia zinakua 
challenge/ somo kabisa la kutendea kazi na ku-share mara moja ili 
kusaidia/kubariki na wengine. Pia zinafanya hata mtu unashangaa na 
kupenda jinsi gani Wapendwa wanapoamua kutembea na Mungu na kumtumikia 
inavyopelekea Bwana naye kufurahi kua na mambo yao toka hatua za mwanzo 
kabisa.
Kila mmoja wetu anajua kua Bible 
inaongea sana jinsi ya kupata Mke kuliko Mume na maandiko maarufu ni 
kama-‘’Mithali18:22-‘’Apataye mke apata kitu chema; Naye ajipatia kibali
 kwa Bwana’’ na Mithali.31:10-’’Mke mwema( Kiswahili imetumia neno moja 
tu .’’Mwema’’ lakini Kiingerea ktk Bible mbalimbali imetumia maneno 
mengi yenye nguvu ya ajabu na kushangaza kujua kumbe Mwanamke mtarajiwa 
kua Mke ni kitu kizuri na cha ajabu sana hasa aliyetoka kwa Bwana.Maneno
 yaliyotumika ni kama.’’ wife of noble character’’, ‘’capable’’, 
‘’intelligent’’ ‘’virtuous woman’’, ‘a competent wife’’, ‘’worthy 
woman’’), ni nani awezaye kumwona? Maana kima chake chapita kima cha 
marijani. Tena Biblia ya King James na New King James ndizo zimetumia 
neno ‘’Virtuous woman’’( notice: Ni woman!) na maana ya neno 
‘’Virtuous’’ ni ‘’good’’, ‘’moral’’, ‘’ethical’’, ‘’upright’’, 
‘’honourable’’, ‘’excellent’’, ‘’pure’’, ‘’worthy’’, ‘’honest’, 
‘’righteous’’, ‘’exemplary’’, ‘’squeaky clean’’, ’’blameless’’, 
’’praiseworthy’’, ‘’incorruptible’’, ’’high-principled’’), pia 
Mwanzo.24:1-67. Katika Agano Jipya, tunakutana na neno kuchumbia au 
Mchumba wazi wazi ktk Luka.2:5 ingawa hatuambiwi Joseph alimpataje mdada
 Mary. Kwakua ni ivyo kwamba Bible imeongolea sana kupata Mke mwema 
ambaye anapatikana tu kwa Bwana, mchumba bora je anayepelekea mke mwema,
 tunampataje? kwa kizazi chetu cha leo Agano jipya ambapo hatuchanguliwi
 Wachumba/Wake zetu na na wapendwa, Viongozi wa Kanisa. Wazazi kama 
zamani,tunafanyeje kua salama? Karinu soma ushuhuda mfupi ufuatao bila 
shaka kuna jambo Bwana atasema nasi.
USHUHUDA: Ni kijana mwenye bidii ya kazi
 ya Bwana na mpenda mambo ya kanisa, maongozi na mipangilio ya 
Wachungaji wake.Amekaa kanisani muda wa miaka kumi toka aokoke na 
imefika wakati sasa anataka kuachana na ukapera.Katika kukaa kwakwe 
kanisani na kushiriki mambo mengi,amefahamiana na wadada wengi kwa 
sababu iyo toka aanze kuwaza kuoa uku akiendelea na maombi na huduma, 
binti sayuni mmoja anaitwa Magret akawa anakuja-kuja sana ktk akili na 
nafsi yake na taratiibu akaanza urafiki wa kawaida lakini yeye anajua 
anacholenga. Akaendelea na maombi na huduma na shughuli za kanisani kama
 kawaida. Siku ya siku akasema, yatosha maombi na sasa ni wakati wa 
kwenda kumtamkia mdada uyo. Akiwa njiani kwenda na hata alishamwambia 
mdada mhusika kua wakutane mahala ‘’kuna ishu moja anataka 
kumtaharifu’’, ghafla moyoni akasikia mdada mwingine kashuka/kaingia na 
sauti hapo hapo inasema naye moyoni..’’ Magret hatakua mkeo bali Anna’’.
 Da! Kijana akashangaa kweli, akadhani ni mawazo au devo! Akavuta hatua 
kuendelea kidogo ghafla tena sauti ile ile.. ’’ Magret hatakua mkeo bali
 Anna’’.Kitu cha ajabu kingine ni kwamba, wakati sauti inasema naye, 
hapohapo akasikia love( falling in love) hamna mfano kwa Anna! Anasema 
hajawahi penda ivyo ghafla ingawa pia wanafahamiana naye Anna kwa miaka 
ktk huduma ya watoto ( Sunday school). Kijana akageuza kurudi kanisa 
kuingia chumba cha maombi na kumuuliza Mungu imekuaje? Wala hakusikia 
tena sauti bali ni growing love na peace ambayo hana jinsi ya 
kutoisikia/hisi-imejaa na inakua..Aliamua kwenda nyumbani na kupumzika. 
Anapoamka tu kwenda kanisani, ni love na amani ya ajabu inawaka ndani 
juu ya Anna and no more to Magret, lo! akajaribu kufanya maombi Bwana 
amsaidie kujua ni kweli ni Anna na love and peace anayosikia ni Yake 
Bwana au kibinadamu? ( ingawa kwa dalili zote. Alijua ni Mungu anafanya 
jambo ila kibinadamu akawa anasitasita tu. Aliporudi nyumbani, 
kilichotokea kilimshangaza kuliko kawaida..ghafla simu yake 
inalia…kuangalia kuna msg imetoka kwa binti sayuni Anna ikisema’’’Asante
 Yesu kwa kunipa Mkaka Mzuri mtumishi wako’’, alipoisoma 
hakuamini!!!!!!! akiibeba simu yake moja kwa moja mpaka kwa shemasi na 
kumwambia story nzima na ile sms. Shemasi hakua hata na muda wa 
kupoteza, akata shauri lile na leo hii Anna ndiye na Magret 
siye-atangoja wake.
Kwakua Mke mwema anapatikana/anatoka kwa
 Bwana basi vivyo ivyo kwa nini isiwe hata Mume na pia mchumba?.Na kweli
 ingawa Magret,Anna, wote ni wadada wa nguvu ktk kanisa na utumishi 
lakini kujua hasa ni nani kati ya hao maana wote wana viwango tu kiimani
 na kikanisa/kiushirika,hakika Roho Mtakatifu inabidi ahusike, 
otherwise, it is confusions out of so many blessings maana wote wanafaaa
 na wanalipa maana wana mpenda Yesu na wako serious ktk utumishi na 
wokovu na wanakwenda mbinguni.
Press on,
M.L