Agano jipya la damu ya Yesu:
Muhtasari wa tofauti kati ya
Agano la Kale na Agani Jipya
Mpendwa msomaji,
wakati tunapohitimisha mada hii ya Agano la damu, sina budi nikupitishe kwanza
kwa jumla kuhusu tofauti za maagano mawili yaliyomo katika Biblia. Kisha
nitakuonesha tofauti zilizomo kwa kuzingatia vipengele maalumi li upate kujua
ni kwanini inatupasa kujena fundisho la imani kwenye maandiko ya Agano Jipya
badala ya Agano la Kale.
Kimsingi,
Japokuwa Maandiko katika Biblia ni ya kitabu kilichounganisha ujumbe wa vitabu
vyote, lakini iko tofauti kati ya maandiko kati ya Agano la Kale na yale ya
Agano Jipya. Agano la Kale limeweka misingi inayoonekana kuwa kweli za Agano
Jipya zinathibitishwa. Aidha Agano la Kale limesheheni nabii ambazo zimetimia
katika Agano Jipya
Agano
la Kale linaonyesha visa na historia za watu mbali mbali, wakati Agano Jipya
linamlenga Mtu mmoja ambaye ni Yesu Kristo. Agano la Kale linadhihirisha
ghadhabu ya Mungu dhidi ya dhambi (sehemu ndogo ya neema); wakati Agano Jipya
linadhihirsha neema ya Mungu kwa wenyedhambi (na kwa sehemu ghadhabu ya Mungu)
Agano
la Kale linatabiri ujio wa Masihi (Isa.53), na Agano Jipya linamtambulisha
Masihi mwenyewe (Yh.4:25-26) Agano la Kale limeandika Sheria ya torati, na
Agano Jipya linaonesha jinsi Yesu kama Masihi alivyotimiliza sheria ya torati
(Matt.5:17; Ebr.10:9)
Agano
la Kale linajihusisha zaidi na taifa teule la Wayahudi; wakati Agano Jipya
linajihusisha zaidi na Kanisa la Kristo (Mat.16:18)
Baraka
za kimwili zimeanishwa katika Agano la Kale (Kumb.29:9), wakati Baraka zote za
rohoni zimetolewa katika Agano Jipya (Efe.1:3)
Kwa
kuwa ufunuo wa Mungu katika Maandiko ni endelevu, Agano Jpya linaweka mkazo
kwenye kanuni ambazo zilikwisha kutambulishwa katika Agano la Kale. Mathalan,
waraka kwa Waebrania unatafsiri jinsi Yesu alivyo Kuhani Mkuu wa kweli, na
jinsi ambavyo anachukua nafasi ya dhabibu zote zilizotangulia kufanywa katika
Agano la Kale kama kivuli
Mwana-kondoo
wa Pasaka katika Agano la Kale (Ezr.6:20) anafanyika Mwanakondoo wa Mungu
katika Agano Jipya (Yh.1:29). Agano la Kale linatoa sheria. Agano Jipya
linaweka bayana kile ambacho sheria zilimaanisha zikionesha hitaji la wokovu na
sio kwamba sheria ndio msingi wa wokovu (Rum.3:19)
Agano
la Kale linaonesha jinsi paradise ilivyopotea kwa sababu ya Adamu; wakati Agano
jipya linaonesha jinsi paradisho ilivyoreshwa kupitia Adamu wa pili, yaani
Kristo. Agano la Kale linatangaza jinsi binandamu alivyotengwa mbali na Mungu
kwa sababu ya dhambi (Mwanzo 3), na Agano Jipya linatangaza binadamu
alivyorejeshwa kwa Mungu kupitia Kristo (Warumi3-6)
Vipengele
vitano vya tofauti za
Agano la Kale
na Agani Jipya
1. Tofauti
za kihistoria.
Vitabu
vya Agano la Kale viliandikwa tangu enzi za Musa mpaka mwaka 400 K.K Hii ni
sawa na miaka ipatayo elfu moja kuanzia wakati wa uumbaji wa ulimmwengu mpaka
Wayahudi kurejea Yerusalemu chini ya Ezra na Nehemia. Maandiko ya Agano Jipya
yaliandikwa kati ya miaka 50 B.K na 150 B.K
2. Tofuati
za kimwelekeo.
Agano la
Kale limenaidka nguvu na matendo ya Mungu vikiashiria ujio wa Masihi. Agano
Jipya linamfunua Yesu kama Masihi, likisimulia maisha yake na mafundisho yake
kama msingi wa Kanisa na uenezaji wa Injli.
3. Tofuati
za kinabii
Sehemu
kubwa ya nabii za Agano la Kale zililenga mambo yajayo na hazikuwahi kutumia
baada ya mchakato wa maandiko ya Agano la Kale kukamilika. Agano Jipya
linadhihirsha utimilifu wa nabii za Agano la Kale, zikiwemo zaidi ya nabii 300
katika maisha ya Yesu Kristo
4. Tofuati
za matendo ya ibada
Sehemu
kubwa ya Agano la Kale inalenga ibada za hemani na hekaluni kama sehemu kuu ya
mahali pa kuabudia. Humo ndimo yameanishwa mambo yote kuhusu dhabihu, sikukuu
za kiibada na yote yenye kuhusiana na hayo. Katika Agano Jipya, Yesu
alijitambulisha kuwa ndiye mlengwa wa ibada, akijitaja kuwa yeye ndiye njia, na
kweli na uzima, na kwamba hakuna awezaye kuja kwa Baba isipokuwa kupitia kwake
(Yh.14:6)
5. Tofauti
za kiagano
Agano la
Kale limejengwa kwenye torati ya Musa. Agano Jipya limeanza na “Agano Jipya”
ambalo Yesu alikuja kuitimiza torati. Wayahudi na mataifa hawahitajiki tena
kufuata torati ili kuhesabiwa haki; bali Yesu alitoa msamaha na uzima wa milele
kwa wote wanaomwamini.
Na kwa
mantiki hii, fundisho la imani kwa waamini linatakiwa kujengwa kwenye msingi wa
maandiko ya Agano Jipya, na maandiko ya Agano la Kale yanabaki kama historia ya
mambo yaliyotimizwa kwenye agano jipya.
Comments
Post a Comment