KUIMARISHA NGOME

Mchungaji Josephat Gwajima

SOMO: KUIMARISHA NGOME

Kuna magonjwa ya kiroho na yanahitaji ufumbuzi wa kiroho, kama ambavyo matatizo ya kiroho yanahitaji ufumbuzi wa kiroho, hata vita ya kiroho inahitaji ufumbuzi wa roho pia.
Neno Shetani maana yake ni mtengaji, na kwa jina lake anaweza kutega mali na mwenye mali, anaweza kutega wana ndoa, shetani pia kama asili ya jina lake anatenga haki na mtu anayestahili kuwa na haki hiyo.

Ibilisi maana yake ni mshindani au msababishaji, na kwaasili ya jina lake hilo anaweza akasababisha chemi chemi ya matatizo, anasababisha magonjwa, umasikini, uoga, kushindwa, kufeli, kuchanganyikiwa, kutokuonekana, kujiua nk.
Leo duniani unaweza ukamuona mtu amefanikiwa katika jambo lakini bila kufahamu kunakuwa na nguvu ya rohoni inayosababisha watu kuwa hivyo, unaweza ukamuona mwana siasa maarufu, lakini nyuma ya umaarufu wake kukawa na nguvu zinazomsababisha kuwa vile alivyo.

Imeandikwa “Ahabu mwana wa Omri alianza kutawala juu ya Israeli katika mwaka wa thelathini na nane wa Asa mfalme wa Yuda; akatawala Ahabu mwana wa Omri juu ya Israeli katika Samaria miaka ishirini na miwili. Ahabu mwana wa Omri akafanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana kuliko wote waliomtangulia. Ikawa, kama ingalikuwa neno dogo tu kuyaendea makosa ya Yeroboamu mwana wa Nebati, akamwoa Yezebeli binti Ethbaali, mfalme wa Wasidoni, akaenda akamtumikia Baali, akamsujudia. Akamjengea Baali madhabahu katika nyumba ya Baali, aliyoijenga huko Samaria. Ahabu akaifanya Ashera; Ahabu akazidi kumghadhibisha Bwana, Mungu wa Israeli, kuliko wafalme wote wa Israeli waliomtangulia. Katika siku zake, Hieli Mbetheli akajenga Yeriko; akatia misingi yake kwa kufiwa na Abiramu mzaliwa wake wa kwanza, na kuyaweka malango yake kwa kufiwa na mwana wake mdogo Segubu; sawasawa na neno la Bwana alilolinena kwa Yoshua mwana wa Nuni.” 1 Wafalme 16
Wana wa Israel walitumia miaka 40 kutoka Misri kwenda Kaanani nchi ambayo waliahidiwa na Bwana, dhambi iliyokua katikati yao iliwagharimu kutumia muda mrefu kuifikia katika ahadi ya maisha yao. Dhambi inauwezo wa kukuchelewesha kufika kule unakotakiwa kwenda.
Wakati wako njiani kuelekea kwenye nchi ya ahadi ndipo walipokutana na mji wa Yeriko, na baada ya Mungu kutenda mambo makubwa na kuangusha ngome ya Yeriko, Yoshua akasema malango yale ya Yeriko na kuta zake zisisimamishwe na atakayesimamisha atafiwa na mzaliwa wake wa kwanza na mwana wake wa kiume.

Lakini alitokea mtu aliyeitwa Herieli Mbetheli amabye aliamua kuyajenga malango yale, na akafiwa na watoto wake wa kiume. Yamkini watu walimuona anafanikiwa tu kujenga ngome bila kujua amefanikiwa kwasababu ya kafara ya watoto wake wawili.
Watu waovu wanajua kwamba asipo kujitoa , au kutoa kafara hawawezi kufanikiwa, hii ndio sababu hata kwa Mungu ili ufanikiwe unatakiwa kujitoa kwa Mungu asilimia mia moja, ukijitoa kwa Mungu kwa asilimia 50 na matokeo yake yanakua asilimia 50.

“Ndoto zako haziwezi kufanikiwa mpaka uwe umezishinda nguvu za giza kwa jina la Yesu na Damu ya mwanakondoo”
Elieli Mbetheli akamtoa mwanae wa kwanza kafara na wa mwisho ili ajenge utawala mpya.
Kafara hufanywa kwa damu ambayo ina uhai na mashetani hupewa damu hiyo ili wainywe na kuagizwa waende kwa mtu ali aachike kwenye ndoa yake, afeli mtihani, kuna watu wanatoa kafara ili wewe ubaki pale ulipo nayeye abaki pale alipo, kuna watu wanatakiwa wastaafu lakini hawastaafu na kuna watu ambao ni mahiri kuliko yeye lakini kimsingi amejiimarishia ngome ili abaki pale. Leo tunaibomoa ngome hiyo kwa jna la Yesu.

Ngome inayoimrishwa na kafara inakua imara na inamfanya mtu aendelee kuwa vile vile kama mashetani wanavyotaka awe.
Na mashetani wanapata nguvu ya kukuzuia, hata kule unakotakiwa kwenda huwezi kwenda.
Imeandikwa: Kwa hiyo tulitaka kuja kwenu, naam, mimi Paulo, mara ya kwanza, na mara ya pili, na Shetani akatuzuia. 1 wathesalonike2
Unaweza kukuta mtawala anatoa kafara, inapotolewa mashetani yanapewa damu ile na ngome inajengwa ili kuimarisha ngome na atakaye igusa atakufa sababu damu ile ina nena mabaya
Unakuta mtu anaamua kutengeneza ngome ya kukuaribu na kukutumia mashetani yakulinde ukae kwenye ngome ya umasikini ukipata hela inaisha muda si mrefu au unashindwa jinsi ya kuitumia, unapoanza kazi linatokea jambo la kukuudhi uichukie hiyo kazi ili urudi kwenye hali ya kutokuwa na kazi, wanapambana na wewe kuanzia rohoni hadi mwilini, ukae kwenye ngome ya umasikini, upate kazi na usiolewe, biashara yko ifilisike, wamekaa kuzuia ndoto yako isitimie, wamekaa kukupa usingizi wa kichawi.

Wale wasio kupenda watumishi wa shetani wao uwezo wa kuchukua nyota ya mtu na kuitumia, nyota ya elimu, biashara, safari, kibali na ndio maana tunapoomba tunasema njoo ili ile nyota yako iliyoibiwa na mtu fulani irudi na ungae tena. Kile ulichopewa na Mungu kinachukuliwa na mtu mahali na kutumiwa naye.

KAFARA YA DAMU VUNJIKA KWA DAMU YA MWANA KONDOO.
Yesu alikuja kufungua walio fungwa, alikuja kuwaweka mateka huru
“Katika jina la Yesu ninaamuru ile damu iliyotolewa kafara juu yangu ivunjike kwa damu ya mwana kondoo, kwa jina la Yesu.”
“KWA JINA LA YESU NINAAMURU NGOME YEYOTE YA KAFARA YA DAMU ILIYOJENGWA JUU YANGU JUU YA FAMILIA YANGU IVUNJIKE KWA DAMU YA YESU, MTU YEYOTE WA KAZINI, NDUGU YANGU AU RAFIKI YANGU ALIYE NIJENGEA NGOME NINAAMURU IVUNJIKE KWA DAMU YA YESU.”

Comments

Popular Posts