Imani au Kuamini Katika Akili

Roho iliyo jawa na imani ya akili iliyo zalishwa kwa jitihada na bidii ya mwanadamu haifanyi kazi, lakini kijiko ya chai kilicho jawa na imani ya Yesu ita zongeza milima kila wakati.
Hili ni pengo kubwa kati ya kuamini katika akili na aina ya imani ya Mungu. Kuamini katika akili ni jambo la asili. Ina kuja kuambia akili zetu ni hivyo. Imani ya kweli ni ile isio kuwa ya kawaida. Ina zongeza milima na inapatikana tu katika Yesu.
Vitabu vya injili vina tupa habari nyingi ya kujisomea ambayo ina linganisha kuamini kwa akili na imani ya aina ya Mungu. Mathayo sura ya kumi na saba inanza na Yesu na wanafunzi Wake watatu katika Mlima wa mabadiliko. Walipo shuka chini toka mlimani, Yesu kwa upesi akawa na uchungu wa kibinadamu na mateso. Tuna soma, “Walipofika penye umati wa watu, mtu mmoja akamjia Yesu na kupiga magoti mbele yake, akasema, “Bwana, mhurumie mwanangu. Yeye ana kifafa na anateseka sana. Mara kwa mara huanguka kwenye moto au
kwenye maji. Nilimleta kwa wanafunzi wako lakini hawakuweza kumponya.’’ (Mathayo 17:14-16)
Unaweza kuona ushusho? Ni kama kawaida wanafunzi wa Yesu waliamini katika uponyaji, la au la hawange jaribu kuponya yule kijana. Babaye ni lizama aliamini katika uweza wa utendaji wa miujiza, maana baadaye ana sema, “Bwana, nina amini, nisaidie kuto amini kwangu!” (Mark 9:24)
Hatujui habari zaidi, lakini tuna weza kufikiri jinsi wanafunzi waljisanya kuzingira huyu kijana alipo kuwa akipiringika chini, akitoa pofu mdomoni. Labda wali kemea ibilisi au waliamru pepo wachafu kuondoka na hakuni kilicho tendeka. Kuna uwezakano walijaribu kurudia maombi tena, na kufunya dua wakimsihi Mungu. Labda wali mwiimiza babake kuamini zaidi au kwa bidii, waki taka kuweka kwake imani zaidi au juu ya yule kijana. Je wanafunzi waliweza kupambanua ile sababu ya magonjwa ya yule kijana? Labda walijaribu kufanya uchunguzi ya chanzo cha yale pepo wachafu kuanza kusumbua huyu kijana na jamii yake. Hatujui sawasawa jinsi walijaribu kuponya yule kijana, lakini tunajua wali jaribu. Bado baada ya maombi hayo yote, kukemea na kumlilia Mungu ilipo fika mwisho, matokeo yalikuwa duni. Na yule kijana alikuwa mgonjwa kama hapo awali. Na sasa wengine waka sema ya kwamba haikuwa mapenzi ya Mungu kuponya huyu kijana. Tunajua hilo silo jambo maana wakati alipo kuja, Alisema, “Mleteni hapa Kwangu.” (Mathayo 17:17) Baada ya mazungumzo machache na babaye, Yesu akamponya kijana huyu. Tendo hili la Yesu lina thibitisha ilikuwa ni mapenzi ya Mungu kuponya huyu kijana.
Baadaye, wanafunzi walishangashwa na yale waliyo ya ona na kwa nini hawangeweza kuponya kijana. Yesu ana eleza, “Akawajibu, ‘‘Kwa sababu ya imani yenu ndogo. Ninawaambia kweli, mkiwa na imani kama punje ndogo ya haradali, mtauambia mlima huu, ‘Ondoka hapa uende pale’ nao utaondoka. Wala hakutakuwa na jambo lisilowezekana kwenu.’’ ‘‘Lakini hali kama hii haitoki ila kwa kuomba na kufunga.’’ (Mathayo 17:20)

Kama Lori au Kiasi cha Kijiko cha Chai

Je una ona utafauti kati ya kuamini kwa akili na imani ing’oayo milima? Wanafunzi wali weka katika matendo imani ya akili. Hakuna swali! Wali amini kwa uponyaji au hawange jaribu kuponya yule kijana. Yesu ana onyesha iwapo wangekuwa na imani ya kweli badili ya imani ya akili, wangehitaji tu imani kama punje ya haradali na muijiza ungetukia.
Mabilioni ya dola zinazo stahili katika kuamini kwa akili na hakuna kitu kina tendeka, ila tu peni la imani - ile imani ya Mungu - na hakuna kisicho wazekana.
Tunacho ita “imani” ni tu kuamini katika akili au “nia juu ya wazo.” Watu wanaweza kusikika wakirudia kusema, “Mimi nimeponywa. Nimeponywa,” au “ Mimi nimepata, nimepata, nimepata,” Ni yangu, ni yangu, ni yangu.” Inakuwa ni kama tukirudia kitu zaidi,tutaweza shawishi nia yetu sisi wenyewe kwamba tuna amini hatimaye tuta kipata.
Imani ambayo Yesu anatupa, imani ya aina ya Mungu, ni ile iko hai, yenye nguvu na uweza. Tusi jaribu kufanya imani idunishwe katika “hatua tano, fungo kumi, siri saba, au siri kumi.” Imani haiwezi kufanyizwa katika kanuni au “hatua”. Ni zaidi ya kuthibitisha funzo faluni, ni nguvu za Yesu Mwenyewe ziki pita ndani mwako; ni neema ya uungu.
Lori iliyo jawa na imani ya akili ambazo zime zalishwa na nguvu na kung’ang’ana kwa mwanadamu, hasiwezi kufanya kitu,ila kijiko cha chai kilicho jawa na imani ya Yesu ita weza kuong’oa milima kila wakati. Habari njema ni kwamba Yesu anafanya hii imani kuwa ya kufikiwa.Unahitaji tu kumjia Yeye, uliitiye jina Lake, na umkaribiye Yeye. “ Bali wote waliompokea, Yeye kwao Yeye aliwapa uwezo wa kufanyika watoto wa Mungu, ndio wale waliaminio Jina Lake. (Yohana 1:12)Yote imaefungamanishwa katika “Yeye,” “Yeye na “Yake” Yeye hufanya kazi na sisi tuna pata faida.

Jinsi nilivyo

Siwezi kijisifia hata kitu chochote mzuri kuhusu mimi, pamoja na kujisifia imani yangu. Ila kwa wepesi nakuja ni kiomba rehema za Mungu.
Katika kila mkutano wa hadhara wa Billy Graham, wakati mwaliko wa kuja kwa Kristo unapo fanywa kwaya inaimba, “Jinsi nilivyo bila ombi, ila damu yako ilimwagika kwangu,” Nina penda maneno hayo, “bila ombi.” Hii inamaanisha sina lolote la kujiombea mimi mwenyewe. Siwezi nika jisifia chochote kizuri mimi, hata kujisifu kwa imani yangu.Badili yake, nina kuja niki omba rehema za Mungu.
Kumbuka mkutano wa maombi katika hekalu uko Yerusalemu, na yule mtoza ushuru nyuma akilia rehema, na yule Mfarisayo wa haki ya kibinafsi akiwa mbele ya hekalu akishukuru Mungu kwamba hakuwa kama “watenda dhambi wengine”. Je kiatu cha nane unaweza kuvaa: cha ya mtoza ushuru au yule mwenye haki ya kibinafsi - Mfarisayo? Hakukuwa na baraka kuja kwa Mungu na kujiletea mambo yetu wenyewe, ila rehema na neema itiririkao kwake yule aliye kuja “bila ombi lake tu.” Majaribio yetu yote ya akili dhidi ya imani ni kazi bure. Tunapo kuja kwa Yesu bila chochote chetu, malongo yaliyo furika na rehema Yake na Upendo inafunguka wazi kwetu.

Amani Katika Dhoruba

Katika tukio lingine wakati Yesu na wanafunzi wake walipo kuwa katika merikebu, wimbi la dhoruba lilitisha kuwazamisha wao. Wanafunzi walikuwa pale wakilia Mungu, waki amru dhoruba litulie, ila hakuna kilicho tukia. Kwa kawaida waliamini Mungu angetuliza hiyo dhoruba, lakini ilikuwa ni imani iliyo toka katika nia zao. Yesu kwa urahisi aliongea maneno haya, “uwe kimya, tulia” na tukawa na utulivu mkubwa (Mariko 4:39). Hii ndiyo alama inayo tafautisha kuamni kwa akili na imani inayotokana na Yesu. Kuamini kwa akili ni nguvu zetu kuamini na kuona kitu kikitukia, Imani ya Yesu inakuja na amani kuu.

Amini na Nena

Mtu anaweza kuuliza, “Si ni muhimu kwamba tunene katika imani?” Ndiyo imani hunena na hukiri Neno la Mungu. Kukiri kuzuri kwa Neno la Mungu hutoka kwa imani, lakini imani haitoki katika kukiri maneno mazuri, ila imani hutoka kwa Yesu. Hiyo ndiyo sababu Andiko lasema, “Nina amani na kwa hivyo nina nena,” Na sio nalinena mpaka nilipo amini Unaweza kuuliza, “Je imani haina tendo?” Ndiyo, tendo hutoka kwa imani, na sio imani kutoka kwa tendo - kwa hivyo imani hutoka kwa Yesu.

Viatu vipya vya Vasco

Nilipo kuwa nina hubiri katikati mwa mji wa Plovdiv Bulgaria, mama mmoja alileta mwanawe wa amri wa maika tano, Vasco, ambaye alikuwa ame pooza.Yule mama alikuwa amesikia maajabu ya Yesu yaliyokuwa yametendeka katika mikutano ya juzi kule Sofia, mji mkuu wa Bulgaria. Alikuwa amfurahihia zaidi na yale aliyo ya sikia, akitarajia mwanawe atatembea alimnunulia suriri ndefu ya jeans, na jaketi na viatu mpya. Huyu kijana hakuwahi kuwa na vyatu vyovyote, hakuzihitaji maana hangeweza kusimama wale kutembea. Walakini, mamake Vasco alikuwa na uhakika kwamba atahitaji vyatu maana Yesu atamponya huyu mwana. Nilivyo hubiri Yesu usiku huo yule mwana wa miaka tano na mamaye wakaja madhabuhuni. Na yule Vasco akakimbia mbele na nyuma akionyesha watu yaliyo kuwa yametendeka. Watu walikuwa pale walikuwa na furaha. Hiyo ndiyo imani ya Yesu. Alimpa mamaye Vasco imani ing’oayo mlima.
Imani sio njia- imani ni mtu
Na sasa ninaweza kusema hiyo hadithi na yule mtu aliye kiwete anaweza kununua vyatu na aje katika mkutano na hakuna kitu kitatendeka. Kwa mtu moja hii ilikuwa ukweli ulio hai; kwa mtu mwingine inaweza kuwa mbinu fulani ya imani. Imani sio njia - imani ni mtu.

Yule Mtu Aliye Tambaa

Katika mojawapo wa Sherehe za mikutano za Injili kule India, mwanaume aliye kuwa amepooza kiunoni mwake alikuwa amelala pale chini nilipo zungumza kuhusu Yesu Kristo. Yeye alijizongomeza chini pale kwa mikono yake akitambaa na kutafuta njia katika umati kupata njia ya kufika jikuani. Niliposema katika jina la Yesu, na viwete wamke na watembee, alijaribu kusimama lakini akaanguka chini. Akajaribu tena hata na yale matokea mabaya. Nisengelijua haya pasipo Mchungaji Fredrick Mwassa kutoka mshariki mwa pwani mwa Kenya alikuwepo. Alikuwa amesimama akiangalia huyu bwana mwenye huruma akijaribu kumka na kutembea. Alini ambia baada ya mkutano, “Peter, nili mfikia yule bwana kiwete nikisema, “ Nikusaidie?” Yule akasema, “La, nina amini neno la Yesu ambalo nisikia likihubiriwa. Nina liamini zaidi kuliko vile nina amini katika hali ya kupooza kwangu. Nita tembea mwenyewe”. Tena akajaribu na wakati huu, aliegemea kwa mikono zake. Aka sima kwa mikuu yake na akaja akikimbea kwa jikwa, hapo na watu wote waliye mwona waka anza kulia na walikuwa pale wenyewe kwa yale walikuwa wameshuhudia. Roho alikuwa akifunulia huyu mtu Yesu.Yesu alikuwa amempa yeye imani, na hakuna ambaye ange zungumza kumhusu yeye kutoka kwa ndani yake.
Nina weza kuhusisha hii hadithi na mtu mwingine katika hali kama hii ange sema na atende katika hali hii moja, na hakuna linalo weza tendeka.Ni ukweli imani huitikia kwa kutenda, kwamba imani bila matendo imekufa. Lakini imani haitokana na kuiga matendo ya mtu mwingine – imani hutoka kwa Yesu. Usijaribu kuiga au kunuku yale mtu mwingine amefanya, bali wewe mkaribie tu Yesu. Uliza Roho Mtakatifu kufunua Yesu kwako zaidi kila siku. Imani ya Yesu, hakikisho na amani vita kuja moyoni mwako. Hii ndiyo sababu kila ushuhuda wa muijiza ni wa ajabu, iwe ni ushuhuda toka kwa Bibilia au wa sasa. Kama vile kila mtu kibinafsi anajiunga na Yesu, yule mtu atatenda katika imani ndani Mwake.
Kwa wingi tunapo angalia nguvu zetu ndipo kwa ubaya mno inavyo kuwa, ili hali tunapo mwangalia Yesu kwa urahisi inakuwa.
Yesu ni ufunguo kwa kila kitu. Muijiza wetu upo ndani Yake. Kwa wingi tunpo angalia nguvu zetu ndipo kwa ubaya mno; inavyo kuwa, ili hali kwa wingi tunapo angalia Yesu kwa urahisi inakuwa. Kwa kuongezeka nime fanya mtizamo wangu wote kumwinua Yesu. Mtume Paulo ana andika “Ninyi Wagalatia wajinga! Ni nani
aliyewaloga? Yesu Kristo aliwekwa wazi mbele yenu kwamba amesulibiwa?” (Wagalatia 3:1) Imani, miujiza, uponyaji na maajabu hayatendeki kwa kwa binu za ujuzi wa imani. Hizi baraka huja wakati watu wanaona Yesu kikamilifu amedhirishwa. Hii ndiyo ilikuwa mtindo wa mahubiri ya Paulo: iliyo onyesha picha ya ukuu wa Yesu.

Ni Karama

Kuamini kwa akili hutoka ndani yetu. Tunajaribu kufikia hatua ya nafsi kuonekana mahali ambako tunafikiri tuna amini kitu. Hii ni kinyume kamili kuhusu imani ya Mungu.Angalia tena hili andiko: “Wake ndani ya Kristo Yesu. Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani, wala hii si kwa matendo yenu mema. Hii ni zawadi kutoka kwa Mungu, si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.” (Waefeso 2:8-9)
Hii inamaanisha:
1.  Imani sio “yetu sisi”
2.  Imani ni “karama ya Mungu.”
3.  Imani sio “ya matendo;”
4.  Iwapo imani ingetokana na matendo yetu wenyewe tunge jisifu, na kwa sababu hatokani nayo, majivuno yetu yote humwendea Yesu.
Tuna itunza na kufanya imani hii iliyo tolewa na Mungu kukua kwa kuendelea tukiangalia Yesu.
Mstari unafuata una angazia jinsi vile imani huja. “Kwa maana sisi ni kazi ya mikono ya Mungu, tulioumbwa katika Kristo Yesu, ili tupate kutenda matendo mema, ambayo Mungu alitangulia kuyaandaa tupate kuishi katika hayo.” (Waefeso 2:10) Kila kitu tuliyo nacho ni kwa sababu sisi ni viumbe katika Kristo Yesu. Sisi ni waumini kwa sababu Yesu Kristo, aliye mwanzilishi na mkamilishaji wa imani ndani mwetu. Tuna tunza na kukua katika imani iliyo tolewa na Mungu tukiendelea kuangalia Yesu.
Je wewe unatendea kazi “karama?” Kwa ukweli sio! Kipawa lazima kiwe uhuru au hakitakuwa kipawa. Imani ni kipawa cha Mungu.
Wakati mwingine husikia watu wakisema, “Nimejisomea bibilia kwa bidii na kuomba na imani yangu inakuwa.Nina amini nina weza kufanyia Mungu vitu vikuu sasa.” Aina hii ya maongoezi ina onyesha ya kwamba imani haifanyi kazi, maana hatuwezi fanyia kazi imani na mwishowe hatuwezi kujisifu ndani yake.
Na sasa usi kose kuni elewa mimi. Mimi hujisomea Bibilia, huomba, na nina nidhamu ya rohoni kwa moyo wangu wote. Tunaweza kusoma na kuomba kwa bidii na bado tukose imani inayo ng’oa milima. Ni Yesu tu anayeweza kutoa hii imani. Wakati wepo wake wa amani unapo kugusa, ulimwengu mwingine utafunguliwa kwako. Haiwi wewe kujaribu kwa imani, badili yake, ni imani Yake, imani ya Yesu, inatiririka kupitia wewe. Yeye ni CHANZO CHA MUJIZA KIKAMILIFU.

Comments

Popular Posts