MAJINI MAHABA HULETA UMASKINI KATIKA FAMILIA -2


MAJINI MAHABA HULETA UMASKINI KATIKA FAMILIA -2
Mpendwa msomaji katika sehemu hii ya pili nitakuletea ujumbe kuhusu mapepo haya kwa kiingereza yanaitwa( Mormon) ama (pepo la mali au chuma ulete) yanavyoweza kumletea mtu umasikini kwa kuunganisha mirija yao ya fedha na ya  kwako benki zao na za kwako biashara zao na za kwako kwa watu wasiomcha Mungu;
     bibilia inasema. Kaati na nungu watamiliki,bundi na kunguru watakaa huko nae atanyoosha kamba ya ukiwa na timazi ya utupu…….. Wakuu wao watawaitia ufalme lakini watakuwa si kitu,miiba itamea majumbani mwake upupu na mbigili ndani ya maboma yake nayo litakuwa kao la mbweha na ua la mbuni.

Isaya 34:11-13 na
Je bwana wangu amenituma kwa bwana wako na kwako wewe niseme maneno haya;hakunituma kwa watu hawa walio ukutani wale mavi yao wenyewe na kunywa mkojo wao wenyewe pamoja nanyi?
    Isaya 36:12
Hakuna mtu anayeweza kufanya hivi kama hamna nguvu isiyo ya kawaida nyuma ya jambo hili ikiwa kuona kwa ucahafu huu ni shida utadhubutuje kula hii ndiyo nguvu ya giza ni mpaka pale nuru itakapoingia ndani ya huyu mtu ili giza ling'olewe nayo ni Yesu.
 
Rafiki yangu wale wasiomtumikia Mungu na wale wanaomtumikia kwa kufuata mambo yao binafsi pamoja na wanaojiita wataalamu huwa wanajiunga na majini ambayo yanawasababishia ugumba wa mali; utajuaje unafuatiliwa ama unao majini wa ugumba wa mali ama roho za umaskini tufuatane pamoja ili ujue dalili zake na jinsi ya kujitoa katika gereza hili zito;
 
1. Kulala mfululizo;
Huu ni ulalaji kama waswahili wanavyosema usingizi wa pono mtu analala zaidi ya masaa 12 bila kujigeuza ama kushtuka;Biblia takatifu inasomeka hivi
Mithali 6:9-11. Ewe mvivu utalala hata lini utaondoka lini katika usingizi wako?bado kulala kidogo kusinzia kidogo. Bado kukunja mikono upate usingizi .hivyo umaskini wako huja kama mnyan'anyi na uhitaji wako kama mtu mwenye silaha. Umeona ndugu yangu hii dalili za kunyemelewa na umaskini
2: Kiburi na hasira au maskini jeuri
Hili ni pepo na linawasumbuwa sana maskini wengi utakuta mtu anashida lakini hataki kujishusha ili asaidiwe;Kuna watu ambao huwa wanajidanganya hawahitaji msaada wa mtu yoyote. Wala ushauri na wala hawaoni kuwa wana shida.Ukiona hivi ni roho ya umaskini; wengine wanaenda mbali sana unakuta ana hasira kitu kidogo tu kakosana na wafanyakazi ama bosi wake anakimbilia kuacha kazi ama akigombana na mke wake au mume  anachoma nguo, kuvunja vyombo ,tv,cm na uharibifu mwingi.
Mithali 9:12 nayo inasomeka hivi kama una hekima una hekima kwa nafsi yako na kama una dharau utaichukua peke yako.
 
3: Njaa isiyozuilika:
Hii nayo ni dalili ya kuwa na mapepo ya umasikini kwani unakuta mtu anakula kila saa na kila kitu anachokiona akimuona mtu anakula chochote ataomba ama atanunua na yeye hata kama hana njaa
 
4: Manunuzi;
Kuna watu anbao wanapenda kununua kitu hata hana kazi nacho
Mfano mtu anaishi uswahilini hana hata neti ya mbu ananunu slashi zile za kunasia mbu ama inzi ambazo wanatembeza wamachinga fikiri pamoja na mimi hii ataitumia saa ngapi; wakati zile ni kwa matumizi ya kwenye bustani za mapumziko nyumbani ama hotelini.
 
5:Kununua vitu vilivyo kuzidi ama kupungua
Hii nayo ni aina ya kujua uko kwenye kona ya umasikini utakuta mtu ananunua labda shati ama suruali kubwa kuliko saizi yake anapovaa utafikiri kaazima ama aliletewa wakati kanunua kwa pesa yake na kwa mkono yake; akijifariji kuwa atakuwa nalo ama atakaa nalo mda mrefu au kiatu kidogo ambacho kinambana na hajui kwa nini alikinunua mwisho kinamtoa vidonda hii ni ishara ya kuwa na majini ya umasikini ama kununua vitu vingi ambavyo huwezi kuvitumia hatimae kuharibika. Wakati mwingine unanunua kitu alafu unapofika nyumbani ukivaa kinakuwa hakikutoshi ama haupendezi ama unaachana nacho kabisa ama unagawa.
 
6:Kununua ama kupenda nguo ya rangi iliyokolea sana
Hii nayo dalili ambayo imewakamata watu wengi sana ngoja nikupe mfano kabla hatujaenda mbali kuna mwaka fulani hapa nchini kwetu Tanzania tulikuwa tuna hali ngumu kiuchumi na tulikuwa tunapata nguo kutoka Uganda zilikuwa zinaitwa jinja na zinatoka jinja yalikuwa ni mashati ya blue iliyokolea sana sana, hii ilikuwa ni dalili ya umasikini hapa kwetu kuna kaniki na utakuta mtu kanunua kaniki ili ikichafuka isijulikane aweze kuivaa mara nyingi huu ni umaskini nakupa ushauri nenda fanya utafiti kwa watu wanaopenda kuvaa nguo nyekundu sana, kijani sana,nyeusi sana pinki,nguo za kumeremeta lakini kaivaa mchana kaangalie maisha yao yana mashaka hizi ni dalili za majini ya umaskini.
 
7: Kuota una hesabu pesa
Unapoota unahesabu pesa ina maana hizo pesa si za kwako maana wewe haufanyi kazi usiku na unapohesabu ina maana unakabidhi pesa kwa chuma ulete kwani ndiyo wanaofanya kazi usiku;Lakini kwa mtu aliyeokoka ni tofauti nikiota nahesabu pesa huwa nafurahi maana najua maombi ya kubatilisha iwe kinyume chake na inakuwa halisi.
8: Kufanya biashara kwenye ndoto
9: Kupokea pesa nyingi sana kwenye ndoto
10: Kuota unachambia pesa
11: Kuota umelalia mapesa yakawa kama godoro
 
Madhara yake ni kwamba mtu anakuwa haoni mpenyo kabisa kwenye maisha yake na ankuwa kama amewekewa mpaka katika maisha yake yaani asivuke kiwango fulani cha maendeleo ama asishike kiasi zaidi ya kiwango fulani cha fedha.
Ni wengi tumewaombea na wamefunguliwa katika hili na walipofanya kazi zilezile kwa bidii na uvumilivu wakaona mpenyo katika kazi waliokuwa wanaifanya mwanzo kwa bidii ileile lakini wasione mafanikio baada ya maombezi na kufunguliwa wanasonga mbele.
Zipo dalili nyingi sana lakini kwa kifupi nimekuletea hizi kama una maswali ama maoni nitumie kwa anuani hii  iliyopo kushoto ama mwishoni
     
MAJINI MAHABA HULETA UMASKINI -3

Karibu sehemu ya tatu kuhusu majini haya yanavyosababisha madhara kwa elimu; yanajulikana kama KOKORO na AKALWA ambacho ndicho chanzo cha kuanguka kwa watoto kielimu na pia wanazimia  siku za mitihani;
 
 Karibu mpenzi msomaji wa ujumbe huu  Neno la Mungu linalotuongoza ni 
Mathayo 12:43-45 unasema hivi pepo mchafu amtokapo mtu hupita mahali pasipo maji ,akitafuta mahali pa kupumzika,asipate.alafu husema nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka,hata akija aiona tupu imefagiwa na kupambwa,mara huenda na kuwaita pepo wengine saba waovu kuliko yeye na huingia na kukaa humo hali yake mtu yule ya mwisho huwa mbaya kuliko ya kwanza ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kibaya; anagalia hili neno kizazi kibaya kwa nini kiwe ni hiki kibaya kwa nini lisiseme kile kibaya ujumbe huu ni wa kizazi cha leo
         Hapa alikuwepo pepo mmoja tu ambaye aliingia muda usiyo julikana lakini baada ya muda mwingi anatafuta namna ya kumuharibu mwanafunzi huyu, juu ya masomo yake maana mwanzo alikuwa labda pepo la ukaidi kutokusikia wazazi anpoanza darasa la kwanza linaongeza tabia inayoendana na levo aliyoko,kwa mfano kuna magonjwa yanayowapata watoto wadogo na wengi tunajua ni kawaida lakini siyo ndani yake kuna pepo linalokazia hili kule uchagani kuna aina ya ugonjwa wa watoto ambao haupo popote ni kule tuu ni kwamba ni aina ya pepo linalowabababisha watu tu maana pale wanauita "KIRUNG'U" mimi watoto wangu hawakuumwa ingawa mama yangu aliniambia huyu mtoto anaumwa kirung'u unatakiwa umpelke kwa bibi akachanjwe chale wao wanaita "MAKEKU" nikauliza kwani unamuonaje akasema ninaona kama ni mweupe sana mimi namuona yuko sawa lakini pepo lililoko ndani yake anaona hivyo.
Sasa turudi kwa wanafunzi anapofika darasa la saba au form one pepo yule yule aweza kumletea tabia umalaya ambayo hakuona kwa mtu yoyote akiwalal au kulalwa na kila mwanamme ua mke hawezi kusema hapana anaanza kuwatamani majimama au mababa huyu ni pepo yuko nyuma ya yote na shida yake ni kumuharibia uzima au maisha yake,jinsi muda unavyoenda na levo ya mambo  sasa anaongeza na la kutoroka shule na la uvivu wa kusoma au kusinzia darasani na mwisho kushindwa kabisa mtihani huyu ni pepo yule yule sas kwenye akili za wazazi au walezi wanafikiria labda ni kwa sababu ya masomo yamekuwa magumu kulingana na levo ndiyo maana hafanyi vizuri siyo kweli kwa uzoefu niliyo nao jinsi unavyoongeza vidato ndivyo unavyozidi kufanya vizuri maana mengi ni muendelezo wa ulikotoka.
 
Ndiyo maana Yesu alisema kizazi hiki ni kibaya wazazi wamepatwa na mapepo haya una kuta tunawapenda sana watoto wetu na kuwapa vitu vizuri tena vya anasa alafu tunajidanganya tunaenda na wakati ni kwamba pepo aliyekuwa anakuendesha kabla ya kupata pesa alikuwa hana uwezo wa kukuendesha leo kwa sababu  hiyo pesa iliyoongezeka akakuletea pepo wa jinsi ya kutumia pesa kwa anasa; uliwahi kuwaza kabla mtu hajapata pesa watoto wanapanda daladala na wanafanya vizuri tu na yeye ndoa yake ina amani baada ya kupata pesa watoto wanageuka kuwa machangudoa,kujirusha kwa sana, kufeli darasani uwezo wa elimu unashuka, kiburi, makundi, mbona havikuwepo kabla ni pepo hili limeenda kuwaita wengine saba na hali ya huyu kijana itakuwa mbaya sana; Wakati mwingine tunawachagulia watoto masomo ya kusoma kwa sababu inalipa haraka mambo si hivyo tuangalie kile mtoto anapenda saa ingine akili zetu zimetumiwa na huyu pepo bila ya sisi kujua maana ya kujifunza ni kupata matokeo ya kitu kilichoko ndani ya utashi mwanadamu aliyopewa na Mungu na siyo matokeo ya kile tulichokijua kwanza kama ndivyo hamna haja ya kusoma maana tunajua, wengi hatujajua elimu ni mpango halisi wa Mungu na usipomtegemea Mungu kwa hili haitakusaidia wengi wana maPHD lakini wamefeli maisha yanawatatiza kama wengine wanaumwa lakini waliomtegmea Mungu wako na amani hata kama hana elimu. Sikuambii kusoma sana ni vibaya la hasha somea unachotaka, unachokipenda usijaribu kuwa mtu mwingine utakuwa kopi;
Biblia inasema katika
 Mithali 4:13 Mkamate sana elimu usimwache aende zake ;Mshike maana yeye ni uzima wako; Watoto washike sana elimu siyo simu za mkononi siyo kazi ipi ya kusomea upate utajiri wa haraka elimu ni uzima wa mtoto na pepo anapoharibu elimu ya mtu ina maana amemuharibia maisha maana ya uzima ni maisha yako yaliyo na pumzi ya uhai kwa hiyo jambo hili si la mtu mmoja ni la jamii; Kama unakumbuka hamna na wala huwezi mara kwa mara kusikia wanafunzi wanaanguka shuleni kipindi cha kawaida ila ni hadi wakati wa mitihani;
 Utasikia shule fulani wameanguka watoto kadhaa hii ni mbinu ya adui shetani na hata kama watafanya mitihani na wakafaulu chunguza elimu hii au ufahulu huu kwa walioanguka mapepo tatizo hatufuatilii baada ya pale mwisho wao nini kinatokea tunadhani alianguka tu na mambo yamerudi kuwa sawa haya ni mambo ya kiimani yanahitaji kumalizwa kiimani ufaulu wao au mwisho wao kuna kuwa bandia watoto hao watapata A darasani lakini  F maishani huu  ni ufunuo
Kwa kawaida hamna aina nyingi za mapepo kama wengi tunvyofikiri bali kuna kazi za mapepo kwa udhihirisho wake zilizo nyingi na watendaji wa hayo ni mapepo hayo hayo ya aina moja,Tumshukuru Mungu kuna Malaika wengi kuliko mapepo mara mamilioni;
 Kwa mfano kama mtu ana jini mahaba hili ndilo linatenda kazi ndani ya mtu huyo kwa vipindi na mazingira tofauti; labda tuseme mtu anaumwa kiuno unapofuatilia kwa kutibu kiuno waweza kujikuta unapona kiuno alafu linaanza tumbo, sasa utapata uhakika tumbo hili linatokana na dawa ninazokunywa za kiuno; kumbe pepo yule yule amegeuka kuwa aina ya pepo mahoka ambao hushambulia tumbo sana,Unapoanza kutibu tumbo aweza kukuletea kutapika ukafikiri ni kwa sababu ya dawa lakini yote hayo ni matatizo yanayoletwa na huyu pepo mmoja.
 Sasa basi baada ya kuishi mda wa kutosha huanza kuzaa ama kuwaalika wengine na hao wanaokuja huwa na uovu tofauti ambao humpeleka mtu mpaka eneo tunaloita kiroho ukanda wa maya hapo ndipo mtu anapoanza kutafuta waganga,wasoma nyota ama hospitali maalumu ama washauri mtu huyu kama hajahamua bado kutafuta watu wa Mungu wafanye naye maombi hujikuta anakuwa na mzigo wa shida lundo kama vile dunia imemgeukia kwa mabaya kama kuna watu mtaani wanaotuhumiwa kuloga wewe uu mmoja wao; kama wapo watoto wezi wa kwako ni mmojwao kama wako mabinti malaya wa kwako ni mmojawao kama kuna mwanamme aliyefumaniwa au mwanamke wa kwako yumo kama ni waliofeli darasa la saba au form four wa kwako yupo kila kitu kiovu duniani wewe hukosekani; Hata kama kuna bomobomo inapita mtaani itaikumba nyumba yako hata kama iko kwenye kona na kama mnalipwa malipo yako labda yachelewe ama yawe na matatizo ama ulipwe sicho na katika watu kumi wewe ndiye utakaye lalamika na kila mtu atakushangaa mbona sisi tumelipwa sawa wewe tu ndiye mwenye matatizo;
 Sasa hapa kama ni ugonjwa ambao ulikuwa unakutafuna na watu wengine hawauni unaanza sasa kunaonekana kama vile kansa,uwete, ulemavu na umaskini wa kupindukia na mwisho huwakamata familia nzima.
Utakuta familiya nyingine hawavuki umri fulani wanakufaga au hawolewi na wakiolewa hawakai kwa waume zao na wakikaa ni kwa mitala yaani hamna ndoa ni mwanamke tu anajilazimisha kwa sababu afanyeje hata mme akimfukuza hatoki,hata amletee mke mwingine kitandani haondoki kwa sababu anajua kwao hawakai kwa waume anajitahidi kuficha ndugu yangu njoo kwa Yesu tukuombee uwe huru
Wengine hawaoi na wakioa hawawezi kuishi bila kuwa na watoto nje unakuta katika familiya yao kuzaa nje ni kitu cha kawida mambo hayako sawa ni pepo wengine hawakai na wake kila anayemuoa anakuta shida ni ileile;
Mke uliyemuoa au mume aliyekuoa kama ana pepo fulani labda la kupiga au umalaya ujuwe hata kama utaachana na huyo mwenza wako ujuwe kama uko katika ukanda wa maya pepo hilo hilo lililokuwa linamtawala mke au mume uliyeachana naye ndiye atakayekukutanisha na mwingine ambaye ni mmoja wao maana wanajuana  katika ulimwengu wa kiroho na utakayekuja kukaa naye atakuwa kama yule wa kwanza tena hata kuzidi .
 
Hali kadhalika mtoto ambaye anasoma shule fulani alafu akawa hafanyi vizuri ukahamua kumhamisha nakuambia utamhamishia shule nyingi kadri uwezavyo lakini ujue tatizo siyo shule maana waliopo pale wanaendelea vizuri tatizo ni pepo aliyeko ndani yake hata kama umemuhamisha kwa sababu shule hiyo ammekuwa na makundi ya wavulana wahuni na mabinti malaya, ukampeleka shule ya mabinti tu au wavulana tu ujuwe kama bado yuko ukanda wa maya kule atakutana na wavulana ambao ni wabaya zaidi ambao watajiusiha na ulawiti ambapo badala ya kumsaidia asitembee na mabinti kwenye shule uliyo muhamisha ataenda kuanza ushoga analawitiwa yeye kama ni mtoto wa kike ataanza kujifunza kusagana  nakuambia ni shida juu ya shida ni mpaka pale atakapopata maombi maalumu kwa ajili ya maisha yake,maana mtandao wa shetani ni mkubwa.
 
Hakuna tatizo kuhusu kuombewa nenda mahali walipo watumishi wa Mungu wakuombee tafuta kanisa la  karibu na unapoishi tafuta maombi mambo haya yanaanza kama vile;
 
KUOTA UNASUKWA,UNANYOLEWA AMA UMEVAA KOFIA
KUOTA KUPIGWA RISASI YA KICHWANI
 
Ujuwe ndoto ni halisi kuliko uhalisi wenyewe kwa hiyo unapoota usipuzie;
Sema maombi haya wewe unayetaka kumpa Yesu maisha ili akutetee kwa haya kumbuka sijakuambia ubadili dini ila umwamini Yesu kuwa anaweza
 
BABA MUNGU ASANTE KWA MOYO WA IMANI NAMI NIMEKUBALI KUKUAMINI KWA KUPITIA MWANAO YESU KRISTO NIKIMPOKEA KUWA BWANA NA MWAKOZI WA MAISHA YANGU NIPE USHINDI WA KUSHINDA YA DUNIA KWA ROHO WAKO MTAKATIFU NIKUFUATE WEWE ASANTE KWA MSALABA ULIONIKOMBOA AMENI

Comments

Popular Posts