VIZUIZI VYA NGUVU ITOKANAYO NA KUFUNGA
Somo letu
la leo, ni somo la mwisho katika mfululizo wa masomo yahusuyo kufunga.
Ingawa kichwa cha somo letu ni “VIZUIZI VYA NGUVU ITOKANAYO NA KUFUNGA“,
hiki kitakuwa ni kimoja kati ya vipengele vitatu tutakavyojifunza katika somo
letu la leo:-
(1) AINA
MBILI ZA KUFUNGA;
(2)
KIPINDI CHA KUFUNGA;
(3)
VIZUIZI VYA NGUVU ITOKANAYO NA KUFUNGA.
(1)
AINA MBILI ZA KUFUNGA
Ziko aina
mbili za kufunga ambazo kila mtu aliyeokoka anapaswa kuzishiriki:-
- KUFUNGA KUTOKANA NA MBIU YA KUFUNGA – (2 NYAKATI 20:3-4; YONA 3:7-8; EZRA 8:21).
Huku ni
kufunga kunakotokana na mbiu ya kufunga inayoletwa kwetu tufunge kwa siku kadha
kwa ajili ya jambo fulani na kisha kukutana mahali fulani kwa ajili ya kilele
cha maombi, hiyo ni mbiu ya kufunga. Mbiu ya kufunga inaweza kutangazwa
na Kiongozi wa Zoni, Kiongozi wa Kanisa la Nyumbani, Kiongozi wa Kikosi Maalum
cha Maombi (Powerhouse), Kiongozi wa Kwaya n.k; na kiongozi huyo ataeleza
makusudi ya kufunga huko. Mbiu ya kufunga, huleta baraka kubwa kwa jinsi
inavyojumuisha watu wengi kwa pamoja, wanaopatana kwa nia moja, katika kipindi
kimoja, kuombea mambo fulani maalum.
- 2. KUFUNGA KWA UAMUZI WA BINAFSI (NEHEMIA 1:4)
Katika
maisha ya mtu aliyeokoka, mtu hujipangia binafsi vipindi vya kufunga na kuomba
ili achote baraka zitokanazo na kufunga. Kama kila mmoja anavyopasa
kujipangia binafsi muda wake wa maombi bila kungojea maombi ya pamoja tu
kanisani, vivyo hivyo, inampasa kila mmoja wetu kujipangia binafsi vipindi vya
kufunga na kuomba, tukiomba kwa ajili ya wenye dhambi wamjue Mungu, kudhihirika
kwa miujiza Siku ya Matendo ya Ajabu, tukiomba kwa ajili ya Mchungaji na
viongozi wa Kanisa na kazi ya Mungu kwa ujumla katika Kanisa, n.k.
(2)
KIPINDI CHA KUFUNGA
Je
tufunge kwa muda gani? Biblia haiweki sheria juu ya siku ngapi za
kufunga. Hata hivyo, tukiangalia vipindi vilivyotajwa vya mfungo katika
Biblia, tutaweza kujifunza mambo kadha. Mifungo mingi katika Biblia,
haitaji siku zilizotumika katika kufunga, lakini hapa tutaangalia ile
iliyotajwa siku za mfungo na sababu za kufunga.
NA.
|
ANAYEHUSIKA
KUFUNGA
|
KIPINDI
CHA MFUNGO
|
SABABU
ZA KUFUNGA
|
ANDIKO
|
1
|
DAUDI
|
Asubuhi
hadi Jioni.
|
Kumuombolezea
aliyekufa.
|
2
SAMWELI 3:35
|
2
|
ISRAELI
|
Asubuhi
hadi Jioni.
|
Wakati wa
Vita inaendelea kumwuliza Bwana juu ya kushindwa kwao.
|
WAAMUZI 20:24-27
|
3
|
DAUDI
|
Asubuhi
hadi Jioni.
|
Kumlilia
aliyekufa
|
2
SAMWELI 1:12
|
4
|
YUDA
|
Siku
moja nzima mchana na Usiku.
|
Kuutafuta
uso wa Mungu.
|
NEHEMIA
9:1-4
|
5
|
YUDA
|
Siku
nzima.
|
Kuutafuta
uso wa Mungu.
|
YEREMIA
36:6
|
6
|
FARISAYO
|
Siku
nzima mara mbili kwa juma kila wakati.
|
|
LUKA
18:9-12
|
7
|
ISRAELI
|
Siku
nzima.
|
Kumlilia
Bwana waokolewe na mkono wa Wafilisti.
|
1
SAMWELI 7:6-14
|
8
|
ESTA/MORDEKAI
|
Siku
tatu nzima.
|
Kuutafuta
uso wa Mungu ili kutoka katika matatizo.
|
ESTA
4:13-16
|
9
|
WATU
WENGI
|
Siku
tatu (3).
|
Kumsikiliza
Yesu akiwafundisha.
|
MATHAYO
15:32
|
10
|
PAULO
|
Siku
tatu nzima (3).
|
Wakovu
na wito wa Paulo.
|
MATENDO
9:9
|
11
|
DAUDI
|
Siku
saba (7).
|
Kumwomba
Mungu kwa ajili ya mtoto.
|
2 SAM.
12:16-18
|
12
|
ISRAELI
|
Siku
saba (7).
|
Kuomboleza
kifo cha Sauli na wanawe.
|
1 SAM.
31:13
|
13
|
PAULO
NA WATU 276
|
Siku 14
nzima.
|
Safari
iliyojaa misukosuko.
|
MATENDO
27:33,37
|
14
|
DANIELI
|
Siku 21
nzima.
|
Kumwomba
Mungu baada ya kufunuliwa Neno.
|
DANIELI
10:1-3
|
15
|
MUSA
|
Siku 40
nzima.
|
Kuketi
mbele za Bwana mlimani na pia kuwaombea Waisraeli.
|
KUMBUKUMBU
LA TORATI 9:9, 18, 25-29; 10:10
|
16
|
YOSHUA
|
Siku 40
nzima.
|
Mlimani
mbele ya Mungu.
|
KUTOKA
24:12-15
|
17
|
ELIYA
|
Siku 40
nzima.
|
Safari
ndefu baada ya chakula maalum.
|
1
WAFALME 19:5-8
|
18
|
YESU
|
Siku 40
nzima.
|
Kujaribiwa
nykani kutokana na kuongozwa na Roho.
|
MATHAYO
4:1-2
|
Kutokana
na jedwali hili tunajifunza yafuatayo:-
1.
Kipindi cha kufunga katika kumtafuta Bwana kwa maombi, kinabidi kiwe siyo
chini ya siku moja (saa 24). Kipindi kifupi chini ya hapo hutumika wakati
wa vita inayoendelea ili kuhifadhi nguvu za vita kwa mfano kufunga wakati wa
kulihubiri Neno la Mungu au kuhudumu.
2.
Kipindi cha kawaida cha mfungo hufikia siku tatu nzima. Ni katika uzito
usio wa kawaida tunazidisha hapo kwa maongozi ya Roho hata hivyo siku hazizidi
saba.
3.
Kufunga zaidi ya siku saba lazima kuambatane na kufunuliwa neno. Mtu
hawezi kufunga siku 40 bila kula na kunywa mpaka kuwe na maongozi DHAHIRI ya
Mungu kwake na uwepo wa Mungu na msaada wake maalum (1 WAFALME 19:8).
Mtendakazi
mzuri wa Kristo atajipangia ratiba yake na kuwa na moja ya kumi ya siku za
mwezi katika kufunga (siku tatu). Inaweza ikawa siku moja katika wiki
mara tatu na siyo mfululizo.
(3)
VIZUIZI VYA NGUVU ITOKANAYO NA KUFUNGA
1. NIA YA KUFUNGA
(WARUMI 12:2)
Nia ya
kufunga ikiwa siyo sawa na neno la Mungu, huzuia kupatikana kwa nguvu itokanayo
na kufunga.
2.
KUFUNGA KATIKA DHAMBI (YEREMIA 14:10-12; ISAYA 58:3-5).
3.
KUFUNGA BILA KUOMBA – Kufunga lazima kuambatane na kumtafuta BWANA kwa maombi (2 NYAKATI
20:3-4; EZRA 8:21).
4.
KUFUNGA HAKUPASWI KUCHUKUA NAFASI YA IMANI – Hatupaswi kuwaza KILA jambo
haliwezekani mpaka tufunge kwanza. Pasipo imani ni bure (WAEBRANIA 11:6).
Kufunga kunachochea tu Imani.
Ni sifa
ipi ya kutuwezesha kuingia mbinguni? Ni utakatifu (WAEBRANIA 12:14).
Ndani yake hakitaingia kamwe chochote kilicho kinyonge (UFUNUO WA
YOHANA 21:27). Kinyonge ni kipi? Ni yule anayetenda dhambi.
Huyu ni mtu asiyefaa, ni mnyonge! Je, wewe ni mtakatifu? Jibu
ni la! Maisha yako yamejaa dhambi, pamoja na kusema una dini; hivyo wewe
pia ni mnyonge, hufai kuingia mbinguni. Ukitubu leo dhambi zako zote kwa
kumaanisha kuziacha, na kuifuata njia ya Yesu Kristo, ndipo utakapopata rehema
ya kuingia mbinguni (MITHALI 28:13; YOHANA 14:6). Je, uko
tayari kutubu sasa ili upate rehema hii? Najua uko tayari. Basi
fuatisha sala hii ya toba kwa dhati kutoka moyoni; “Mungu Baba
asante kwa ujumbe huu. Hakika mimi ni mnyonge, mwenye dhambi.
Sistahili kuingia mbinguni. Natubu dhambi zangu zote kwa kumaanisha
kuziacha. Kuanzia leo nataka niifuate njia ya Yesu Kristo. Bwana
Yesu niwezeshe. Asante kwa kunisikia katika Jina la Yesu. Amen”.
Mpendwa msomaji umekubaliwa kuingia mbinguni. Ili uzidi kudumu
katika utakatifu mpaka siku ya kuiaga dunia hii, hakikisha unahudhuria
mafundisho katika Kanisa linalohubiri wokovu. MUNGU AKUBARIKI !!!
Comments
Post a Comment