Msalaba unakawanya lile ya "kale kutoka kwa jipya"
Wakristo wengi wanapotambua msalaba wa Yesu ni wa muhimu, wengi hawatambui ukuu wa umuhimu wake.
Msalaba unagawa mstari kati ya agano jipya na la kale. Wakati Yesu alipo lia “imekwisha” ya kale yalikuwa yamepita na mapya yame kuja!Mabadiliko kubwa kuliko kiasi
Mabadiliko yalikuwa kubwa kuliko kiasi mwanzoni kwamba hata wafauzi wa Yesu walipata ni ngumu kuacha ya kale nyuma. Simoni Petero alisahihishwa mara mingi, Mara mbili wazi na Yesu (Matendo 10 na 11) na pia Paulo (Wakalatia 2 ) maana alivutwa nyuma na agano la kale katika uso wa yale Yesu tayari alikuwa ametimiza kwa msalaba. Iwapo yule mtume aliye hubiri siku ya pentakote, na aliye ona miujiza kitika kivuli ikiangukia wagonjwa alihitaji kusahihishwa. Si ajabu kwamba wengi leo hii wamekosa kuielewa kazi ya Yesu kamilifi ya ukombozi. Badala ya kuyumbayumba mbele na nyuma kati ya agano la kale na agano jipya, lazima turuhusu dira yetu, Roho mtakatifu alenge mwelekeo wetu na kutukumbusha sisi yale yote Yesu ametundea na kwa ulimwengu wote.Mungu amesha Toa yote
Kabla msalaba watu walingia katika mambo ya rohoni ili kwamba wapate kitu toka kwa Mungu, kumbe baada ya msalaba tuna omba, tuna abudu na kuamini kwa sababu ya yale Mungu asha tufanyia. Sheria ya Musa likuwa dhairi ya kwamba watu walipaswa kutii na kutii amri “usiku na mchana” ili kwamba wapokea baraka za Mungu ( kwa uhakika hakuna aliye faulu ) Katika agano jipya tunapokea baraka kwa sababu ya yale Yesu amefanya. Utii na kujitolea kwake kumewekwa upande wetu. Yabesi aliomba ili Mungu ambariki. Haya yalikuwa maombi mzuri kwake Yabesi, maana aliishi chini ya agano la kale, lakini hayafai kwetu sisi. Tuna omba kwa sababu Mungu asha tubariki katika Kristo “Atukuzwe Mungu na Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo! Maana, katika kuungana na Kristo ametubariki kwa kutujalia zawadi zote za kiroho mbinguni. Waefesso 1:3 ) Tambua Mungu “ametubariki” sio jambo linilo husu “kuende kutubariki mbeleni.”Mungu amesha leta “mtembeo”
Maisha yetu mapya katika Kristo kikamilifu yana tegemea na kufungamanishwa katika kazi ya Yesu iliyo kamilika, Siyo “wewe kufanya mwondoko alafu Mungu ana leta mtembeo.” Jinsi nimesikia wahubiri wakisema mara nyingi. Ujumbe wetu ni kwamba Mungu amesha ridhishwa na toleo la Yesu. Mungu asha leta “mtembeo”. Yeye haidikii sisi kwa sababu ya nguvu zetu – Mungu asha idikia kwa kutulea yote ambayo tutahitaji katika Yesu Kristo.Kazi yetu ni rahisi, ni kuamini yale Yesu amesha fanya. Imani yetu haifanyi mwondoko wa Mungu. Ingefanya hivyo ina maanisha Mungu ako mahala pabaya. La, imani ni kutegemea yale Yesu amefanya. Imani haitizamii yale Mungu atatenda siku fulani ( hiyo itakuwa fikira za agano la kale ) Imani ya kweli inaangalia yale Yesu amefanya msalabani. Inatosha.Tumbua ulicho nacha tayari
Kabla ya msalaba tuna aina, ya vivuli na kanuni za dunia. Baada ya msalaba tuna ukweli waumini walitizimia kuona kazi ya Kristo: na sasa tuna angalia nyuma kwa yale amefanya. Hii ndiyo asili ya maisha ya Mkristo. Mara ya kwanza tunapo okoka hatujui yote Kristo ametutwalia sisi. Bado huu wakati wa “kuzaliwa upya” tunapokea kila kitu tutakacho hitaji. Hatuhitaji kutafuata “zaidi”ya Mungu, maana tayari tunacho. Badili yake kutafuta kwetu ni kutambua tulicho nacho. Jinsi Adam alipaswa kufungua macho yake na kutumbua yote Mungu alikuwa ameanda katika bustani la Edeni, kwa hivyo Roho mtakatifu anatufungua macho kutambua urithi wetu. Mtume Paulo hakutoa pendekezo ya kwamba walikosa chochote, lakini walihitaji kutambua walicho nacho. Katika maombi yake kwake Filomoni, ana andika : “Naomba ili imani hiyo unayoshiriki pamoja nasi ikuwezeshe kuwa na ujuzi mkamilifu zaidi wa baraka zote tunazopata katika kuungana kwetu na Kristo.” (Filomini 6)
Iwapo tungeli paswa kuuliza wakristo wafanya nakala mbili, moja inayo tambua shida, udhaifu, kushindwa na ingine inayo kubali waliyo nayo. Nina hofu nakala ya kwanza itakuwa mrefu mno. Imani yetu haitendi kazi kwa kadri ya yale hatuna, lakini kwa yale tuliyo nayo. Wakati Paulo alipo waeleza waumini wa kanisa la Waefeso; “ili Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo Baba mtukufu, awajalieni Roho wake atakayewapa hekima na kuwafunulieni Mungu, mpate kumjua. Namwomba Mungu aifunue mioyo yenu iweze kuuona mwanga wake, mpate kutambua lile tumaini alilowaitieni na utukufu mkuu wa zawadi alizowawekea watu wake, mpate kutambua jinsi uwezo wake ulivyo mkuu mno kwa ajili yetu sisi tunaoamini. Uwezo huo unaofanya kazi ndani yetu, ni sawa na nguvu ile kuu mno” (Waefesso 1:17-19 )
Tambua Paulo haombi kwamba Mungu atawapa Waefesso chochote- ana omba macho yao yatafunguliwa kuona walicho nacho.
Chujia Agano la kale kupitia msalaba wa Yesu
Msalaba hubadilisha mtizamo wetu wa maandiko ya Agano la kale, maana sasa tunaelewa Musa, Zaburi na Manabii ni ushuhuda wa Yesu. Luka 24:27, 44-45 ) Bila hili “ Kristo” ufunuo wa Agano la kale ni katibu kilicho tiawa “pazia” utasoma bila kuelewa. “Lakini akili zao zilipumbazwa. Mpaka leo hii lisomwapo Agano la Kale, kifuniko hicho bado kipo. Kifuniko hicho kitaondolewa tu na mtu anapoungana na Kristo.” 2 Wakorintho 3:14) Japokuwa Paulo ana wazungumzia Wayahudi waandishi, hii kweli leo hii. Wengi husoma Agano la kale bila ufunuo wa kazi ya Kristo iliyo kamilika msalabani, wakati njia iliyo bora ya kuelewa maandiko haya ni kuchujia Agano la kale kupitia msalaba wa Yesu. Tunapo mwona Yesu, tuna tambua Yeye ni Sehemu maradufu, ni upako, mwombezi wetu, imani yetu, yote katika yote.Hatutembei katika wayo za Eliya au manabii wengine :tuna mfuata Yesu Kristo.Hizi sio “siku za Eliya” au siku siku za Ezakieli ila ni siku za Yesu Kristo na waumini wake. Musa na Eliya, wanawakilisha Sheria na Manabii, waliwesha kutoweka huko Mlima wa Mageuzi, na akabaki tu Yesu. Hii ni picha ya aina gani mzuri jinsi Agano la Kale na mpangilio wake wa Sheria na Manabii imepita, na kubadilishwa na Yesu Kristo, ambako ndani kuna ukamilifu wa Mungu.Sheria imetimilika
Wale wanao shindani, hakika wana shida kubwa. Kulinganna na Yesu sisi tuna wajibika kwa “nukta au sehemu ndogo ya sheria” mpaka “yote yatimie” Mungu asifiwe kwa maana yote yametimia! Bila hiyo tungewajibika kwa kila sheria ya Musa. Badili yake tupo katika agano jipya, maana “ Kristo ndiyo mwisho wa Sheria ya haki,” (Warumi 10:4 )
Kabla ya msalaba utii wetu ulikuwa wazi; sasa ni utii wa Kristo. Alafu ikiwa kuonekani kwa inje kwa taratibu za dini: na sasa ni mabadiliko ya moyo kwa uwezo wa msalaba.
Hakuna nakala inayo weza kuanza kuonyeza kilindi kilicho kimilika cha msalaba wa Yesu. Mara moja tuna weza kuona ufunuo wa umuhimu wake, tuna tambua ya kwamba kwa milele inatenganisha kutoka Sheria, Msalaba ndiyo mahala pa malipo ya dhambi za dunia. Sasa tunamfikia Mungu kwa sababu ya yale Yesu amefanya. Hapo sasa Agano Jipya sasa yaleta umaana. Mandiko ya Mtume Paulo yanakuwa hai. Hatujioni tena sisi wenyewe kama “wasio navyo,” ila tuna kila kitu ndani ya Kristo.
Safari Ya Utambuzi
Nina kuimiza uende katika safari ya utambuzi.Jisomea Agano Jipya kana kwamba unasoma mara kwanza na amini ya kwamba “mambo yote” katika maeneo yote ya maisha ni yetu kupitia ufahamu wa yale Yesu alifanya. (2 Petero 1:1-4)
Comments
Post a Comment