KUFUNGULIWA KUTOKA NDOA NA MAPEPO AU JINI MAHABA.
“Nami nimeona lililo na uchungu kupita mauti yaani,Mwanamke ambaye moyo wake ni mtego na tanzi na mikono yake ni kama vifungo; Yeye ampendezaye mungu atamponyoka,bali mwenye dhambi atanaswa na yeye“(Mhubiri 7:26)
Mpendwa mapepo dume na mapepo jike yapo
na ni halisi.pepo mahaba dume kwa kiingereza linaitwa incubus. Pepo jike
linaitwa sacubus. pepo dume linauwezo wa kulala na mwanamke kadhalika
na pepo jike lina uwezo wa kulala na mwanaume katika ndoto. Mapepo
mahaba yanatoka baharini au kwenye mito au kwenye maziwa.(wote
niwatendakazi wa shetani asili yao kuzimu)kuna wanaume ambao wameoa
katika hali halisi na pia wameoa katika ulimwengu wa roho.hivyo
kunauwezekano wamtu kuwa na mwanamke katika halihalisi na kuwa na kuwa
mwanamke katika ulimwengu wa roho. Solomoni anasema “Nami nimeona lililo
na uchungu kupita mauti,yaani mwanamke ambaye moyo wake ni mtego na
tanzi,na mikono yake nikama vifungo; yeye ampendezaye mungu
atamponyoka,bali mwenye dhambi atanasw na yeye” (Mhubiri 7:26).
Andiko hili linatuonyesha picha ya
utendaji kazi wa mapepo mahaba.Na haya mapepo yapo katika jinsia
zote.kwahiyo ukipenda dhambi utanaswa na ukichagua kumpendeza mungu
utaponyoka.uamuzi ni wako kunaswa au kuponyoka (nimeshakupa maarifa).
Mungu akusaidie uponyoke ndiyo sababu nimeleta kwako samo hili iliujue
dalili za mapepo mahaba na ufunguliwe kutoka katika kifungo cha ndoa za
mapepo mahaba. Pepo mahaba ni pepo awezaye kumtawala mwanaume au
mwanamke katika ulimwengu wa roho, pepo huyu mchafu ana madhara mengi
sana mfano kuzuia kushika mimba au kuharibu mimba,au kuzuia kuoa au
kuolewa (kuvunjika uchumba/ndoa) pepo mahaba hujidhihirisha katika
ndoto,kwani mtu aliyenaswa na pepo mahaba huota ndoto akifanya ngono.
UTAJUAJE KAMA UNA VIFUNGO VYA KIPEPO MAHABA/JINI MAHABA?
Unaweza ukawa umeoa au hujaoa / umeolewa au hujaolewa katika hali halisi.
UNAJUAJE KWAMBA UNAHITAJI HUDUMA YA KUFUNGULIWA KUTOKA VIFUNGO VYA MAPEPO MAHABA?
Ilikujibu swali hili ngoja tuone dalili
za mapepo mahaba katika maisha ya watu mbalimbali.Kwa ufahamu huu utajua
kwamba unahitaji huduma ya kufunguliwa.
DALILI ZA MAPEPO MAHABA
1.Kuchoka katika ndoa – Kabla ya kuoa au
kuolewa kila mtu alikuwa na shauku ya kufurahia ndoa.lakini baada ya
muda mfupi wanandoa wamechokana na ndoa imekosa ladha.Wakati mwingine
mwnandoa mmoja anamchoka mwenzi wake.Kama ungepewa nafasi ya kuamua
kwaupya huenda usingekubali kuolewa na mwanaume huyo au kuoa mwanamke
huyo. Mpendwa msomaji kama unajisikia kuchoka ndoa hiyoni dalili ya
kuwepo kwa mapepo ya mahaba tafuta msaada wa huduma ya kufunguliwa
2.Kufanya tendo la ndoa au mapenzi kwenye ndoto na mtu unayemfahamu au usiyemfahamu.
3.Kuchukia kuoa au kuolewa (unajuta kama usingeolewa au usinge oa)
4.Kufanya maamuzi yasiyo sahihi wakati wa kuoa au kuolewa. Kuolewa au kuoa mtu asiye sahihi.
5.Kuachwa na mume au mke.Kila mwanamume
akikuoa baada ya muda mfupi anakuacha.Ujue unamapepo mahaba yanayofukuza
wanaume katika maisha yako.Unakuta mwanamke mzuri amesoma na ana
(uwezo) kazinzuri lakini anaachwa na wanaume au anatelekezwa na wachumba
hapo unahitaji huduma ya fufunguliwa.
6.Kuchukia mahusiano ya kindoa na mumeo au mkeo.Wakati usiku unatembelewa na mapepomahaba.
7.Kunyonyesha watoto kwenye ndoto wakati
huna mume wala mchumba /au umeolewa na huna mtoto kabisa! Ni dalili ya
kifungo cha pepo mahaba.
8.Kuogesha watoto kwenye ndoto wakati hujaolewa ni dalili mapepo mahaba.
9.Kuota una familia kwenye ndoto wakati hujaolewa / au kuoa na wala huna mchumba.
10.Kuota unafanya shopping na mwanaume au mwanamke wakati hunahata mchumba.
11.Kumchukia mwenzi wako kiasi cha kutamani afe ili uoe au uolewe na mtu mwingine.
12.Kuota wanawake au wanaume wako uchi,au wewe mwenyewe kujiota ukouchi.
13.Wanandoa kuota mwanaume au mwanamke yuko katikati yenu au pembenimwa kitanda chenu wakati mmelala.
14.Mwanaume kukosa nguvu na kushindwa katika tendo la ndoa.
15.Mwanamke kupata maumivu makali sana wakati wa hedhi (maumivu makali ya tumbo)
16.Matatizo ya mfululizo ya magojwa ya kike mfano ya tumbo la uzazi,kuziba mirija ya uzazi.
17Kuotaunabakwa ndotoni.Kuharibu mimba baada ya kuota unafanya tendo la ndoa.
18.Kujutia kuoa / kuolewa bila sababu ya msingi
19.Kukosa hamu / moyo wa kuambatana na
mwezi wako.Hujisikii tena kuongea na mwenzi wako wa ndoa unapenda
kucheka na wanawake / wanaume wengine kuliko mwenzi wako hizi nidalili
za kifungo cha pepo mahaba tafuta msaada wa kufunguliwa haraka upone!.
20.KIla wakati kuwaza kwamba ndoa
itavunjika unapotazama miaka miaka mitano ,kumi huoni kudumu kwa ndoa
yako hata hapo ulipo unaonakama muujiza.
21.Kukosa utoshelevu w moyo kat ika ndoa uliyonayo.
22.kama ni msichana huoni kijana yeyote
aliye wahi kukusemesha kwamba atakuoa ujue maranyingine hata wachawi
wanaweza wakawa wamekufunga.
24.Kupewa ahadi za kuolewa bila kutimiwza / kama hakuna anayemaanisha unahitaji huduma ya kufunguliwa.
25.Kuachwa baada ya wanaume kuujua mwili wako au kuchukiwa baada ya mwanaume kulala na wewe.
26.Kucheza na nyoka ndotoni wala hung’ati hili sijambojema ni hatari.
27.kubakwa mara kwa mara katika halihalisi.
28Kumpamimba msichana mwingine halafu unaoa mwanamke mwingine.
29.Mchumba kufariki kabla ya ndoa (kufaghafla mipango ya harusi imeandaliwa)
30.Kuachiswa kazi au biashara kufa mara baada ya kuoa au kuolewa.
31.Kupata ajalimba ya baada tu ya kuoa au kuolewa.
32.Mwenzi wako hakubaliani nawewe katika jambololote mnalopanga (anakuwa mpinzani tu!)
33.Kila mwenzi anaye kuoa au unaye muoa anakufa
34.Kuwa na uamuzi wa kutoolewa au kuoa kwa kuogopa matatizo ya ndoa (hofu ya ndoa).
35.Mwenzi kutokukujali wakatiunaumwa
unajihudumia mwenyewe hadi unapona nayeye yupo hata ulalamike maumivu
anaendelea na shughulizake bila kujali.
36.kupigwa mara kwa mara bila huruma na mume wako.
37.kutishiwa kufukuzwa mara kwa mara na mumewako.
38.Kupotelewa na pete ya ndoa au cheti cha ndoa ktk mazingira ya kutatanisha.
39.Kupewa pete za mapenzi na waganga wa
kienyeji au wanajimu.Vua hiyo pete katika jina la yesu ni antena / agano
la kuvutia mapepo katika maisha yako.
40Kujuta kuolewa au kuoa mwenzi huyo.
41.Kupanga kwamba niki rudi nyumbani tu
nitapokeana na mwenzi wangu kwa furaha ghafla unawasili unaingiwa na
chuki moyoni juu yake.
42.Kuchelewa kurudi nyumbani bila sababu ya msingi (Baada ya ndoa mwenzi wako anabadili tabia ghafla).
Sura yako kuonekana mzee kuliko umri wako.
43.Kutokwa damu sana au kwa muda mrefu
wakati wa hedhi kukiambatana na maumivu makali (maranyingine siku
zinzkuwa za mvurugiko mvurugiko).
44.Unakuwa na roho ya liwalo na liwe hujali ndoa yako hata ukishauriwa hushauriki.
45.Kutokupata mimba katika ndoa yako hata vipimo vya kidaktari vikionyesha huna tatizo au kuharibika mimba mara kwa mara.
46.kutengana kwa wana ndoa hata ingawa mnakaa nyumba mmoja (mzungu wa nne) kila mtu ana chumba chake.
47.Tumbo lako kuonekana unamimba hata watu wana kuona hivyo wakati hauna.
48.Matiti kutoa maziwa wakati huna mimba wala mtoto.
49.Kujisikia mjeuri,hasira,ukaidi kutokuelewana ktk ndoa.
50.Kuonywa na mtu ktk ndoto kwamba hutaolewa.
51.udhihirisho wa wazi wa mapepo mahaba wakati wa usiku.
52.kukumbuka mahusiano ya mapenzi na rafiki zako wa zamani wakati una mkeo / mumeo kitandani.
53.Kujichua au kujiridhisha mwenyewe bila mwenzi usiku au bafuni.
Mpendwa msomaji hizi ni dalili kadhaa ktk
nyingi kama unaona hapo ikosehemu inakugusa tafuta mahala penye huduma
ya kufunguliwa upone, haya mapepo machafu yana leta hata kukufanya uwe
unaishiwa kila mara hata ungekuwa na pesa ya kutosha wewe mda mchache
huna kitu, amani katika ndoa ni ndogo sana ni hekaheka tu!na kama kuoa
au kuolewa kuna zuiwa na haya niliyo kupa mbinu jinasue ktk jina la Yesu
!
Njia kubwa ni umpe Yesu maisha yako. Na
usiogope hata wewe ambaye ulisha mpa Yesu maisha yako kama una dalili
hizi nenda kafunguliwe sio dhambi kufunguliwa uweze kuoa / kuolewa. Na
uliyeko katika ndoa ikiwa na mambo ya jinsi hii hauko salama hata kidogo
kafunguliwe uweze kufurahia ndoa yako katika Jina la Yesu.
HII NIMECOPY KUTOKA KWA KAKA PETER WAWEZA PIA KUTEMBELEA BLOG YAKE KUJIFUNZA ZAIDI http://www.maishaushindi.blogspot.com/.
Comments
Post a Comment