KUOTA NDOTO ZA KUFA KILA SIKU
KUOTA NDOTO ZA KUFA KILA SIKU
Mtu wa MUNGU, BWANA YESU asifiwe. Mimi ni mzima ila
tatizo kuu na kubwa maishani mwangu ni kuota ndoto za kufa kufa kila siku na
kama ikititokea sijaota nakufa au nimekufa au niko kwenye jeneza ni mara chache
sana ila kila mara naota nakufa au nimekufa au niko kwenye jeneza. Je jambo
hili ni nini? Naomba msaada wako au kwa sababu wewe unafahamiana na watumishi
wengi basi omba majibu ili kunisaidia maana jambo hili huniletea woga sana na
kuna siku hadi nilijiandaa kwa kutubu ili hata nikifa niende mbinguni. Nimeokoka
tangu 2010 na jambo hili nimemwambia rafiki yangu wa kike akaniambia
niombe tu kwa MUNGU ili kuvunja mpango wa shetani maishani mwangu, nimeomba
lakini hupungua tu kidogo yaani naweza nikapitisha siku 4 au 5 lakini jambo
hilo hurudi tena na mambo ya kupungua kwa tatizo langu hili yameanza siku za
karibuni tu ila mwanzo haikua hivyo. Jambo kubwa nataka nijue ‘’KUOTA NDOTO ZA
KUFA INAMAANA GANI?’’. Pia naomba msaada wako kama unafahamu maana kuna rafiki
yangu yeye ameota anakimbizwa na nyoka na pia kuna dada yangu yeye kuna
siku aliota nakimbizwa na mbwa na hatimaye yule mbwa akamng’ata mguuni. MUNGU
akubariki sana na naomba majibu sahihi maana mimi naamini kabisa ndoto ni
ujumbe haijalishi ni ujumbe mzuri au mbaya, ni hayo tu. Ni mimi Lucy Khamis niko
manyoni singida.
MAJIBU KUTOKA MAISHA YA USHINDI BLOG.
Lucy ubarikiwe kweli kweli na umeuliza mambo ambayo hakika yanagusa wengi sana na ni wengi sana wametokewa na mambo hayo. Na majibu haya naomba yamsaidie kila mmoja atakayesoma haya. Ni kweli kabisa ndoto ni ujumbe na ndoto ni tukio la ulimwengu wa roho na ulimwengu wa roho unaweza kuwa ni ulimwengu wa roho wa nuru chni ya ROHO MTAKATIFU au ulimwengu wa roho wa giza ambao shetani na malaika zake ndio wahusika.
Kuna aina 3 za ndoto anazoota mwanadamu.
1: Ndoto au ujumbe kutoka kwa MUNGU
2:Ndoto za shetani
3:Ndoto ambazo zinatokana na mtu mwenyewe. yaani yawezekana kwa kuliwazia sana jambo fulani inapelekea unaota jambo hilo, au mfano unafiwa na mtu muhimu sana kwako inapelekea kumfikiri mtu huyo kila muda nayo inaweza kupelekea kumwona kwenye ndoto.
KUOTA NDOTO ZA KUFA :
ni ishara ya kufa kiroho kwa mtu aliyekua amesimama katika imani ya KRISTO pia wakati mwingine yawezekana kuna vitu vya shetani vimekufunga ambavyo umewahi kuingia navyo maagano mfano matambiko au kwenda kwa waganga wa kienyeji au hata kurogwa hivyo unapoota uko kwenye jeneza inamaana uko kwenye kifungo fulani ambavyo kinasababisha kushindwa kutimiza lengo la MUNGU kwako hivyo unapewa taarifa ili kwa njia ya maombi wewe mwenyewe au kwa kutumia watumishi wa MUNGU waaminifu ufunguliwe kutoka kwenye maagano hayo ya shetani. Pia ishara ya kufa ni kuonyesha huwezi kufanikiwa maana shetani amekufunga hivyo hadi utoke kifungoni au kwenye hilo jeneza. Wapo watu wengi wanashindwa wako kwenye majeneza ya shetani ya magojwa , wengine wako kwenye majeneza ya mikosi, wengine wako kwenye majeneza ya kukataliwa na wachumba yaani kila akipata mchumba wakitaka tu kufunga ndoa anamkataa , wengine wapo kwenye majeneza ya kuonekana wabaya mbele za watu kwa sababu jini shamsu anakua amevaa sura ile ndio maana mke wake au mme wake anampenda kwa muda tu na baada ya muda ni vita, wengine wako kwenye majeneza ya hasira, uongo n.k. na hii chanzo chake ni shetani ambaye katika Yohana 10:10 huwa anakukuja kwa watu ili kuvunja, kuharibu na kuua na kwa kusudi hilo ndio maana Mwana wa MUNGU, YESU KRISTO alidhihirishwa ili azivunje kazi zote za shetani (1 Yohana 3:8b). Ndugu nenda kwenye maombezi na utakuwa huru mbali na kuonewa na shetani na kwa wewe uliyeokoka ukiona yanakutokea hayo basi tambua kuwa kuna mlango umeufungulia ndio maana unaonewa maana pia kumbuka kuwa MUNGU ni mtakatifu.

KUOTA UNAKIMBIZWA NA MBWA:
Ni ujumbe kwako kwamba roho ya uasherati au uzinzi inakunyemelea , hii ni hatari sana na kuna rafiki yangu kazini aliwahi kuota anakimbizwa na mbwa na baadae mbwa huyo akamng’ata na nilimwambia afunge na kuomba avunje roho hiyo lakini kwa bahati mbaya hakufanya hivyo na hakika miezi 2 baadae alijikuta ameanza uasherati na dada mmoja na ikawa na ngumu sana kuacha na ikafika kipindi akitaka kuachana na dada yule yule dada anamwambia akimwacha atajiua hadi siku za karibuni tu ndio ameacha tabia hiyo kwa maombi mengi sana ya watumishi . hivyo usipuuzie unapoota unakimbizwa na mbwa tambua kuwa dhambi ya uzinzi inakunyemelea na kumbuka kuwa ndoto ni jambo la ulimwengu wa roho hakuna jambo hata moja linalotima katika ulimwengu wa roho hata kama unaona ajali zinatokea hilo ni mpango wa shetani ulioandaliwa katika ulimwengu wa roho ndio baadae unakuja kutimia katika ulimwengu wa mwili. Hivyo mbwa katika ulimwengu wa roho ni roho ya ukahaba au roho ya yezebeli.
KUOTA UNAKIMBIZWA NA NYOKA :
ni ujumbe kwako kwamba roho ya uongo inakunyemelea
maana nyoka katika ulimwengu wa roho ni roho ya uongo na kumbuka shetani alivaa
umbo la nyoka na kuwadanganya hata akina Adamu na Hawa katika bustani ya
edeni wakatenda dhambi (Mwanzo 3:4) na katika Ufunuo 20:2 shetani anaitwa
nyoka wa zamani yaani aliyewadanganya akina Adamu na Hawa. Hivyo ni kuwa makini
sana na kuvunja roho hiyo kwa jina la YESU KRISTO na mpango huo wa kuzimu
hautafanikiwa. Na mfano mzuri ni mimi siku moja nikiwa kanisani tunaomba
nilimwona nyoka anazunguka na kwa sababu nilikua sijajua kwamba hiyo ni roho ya
uongo unanyemelea watu wa MUNGU hakika kesho yake ulizuka uongo mkubwa na
kusababisha hadi baadhi ya viongozi wa kanisa kukosana na ndio ikawa
mwanzo wa mimi kujua kwamba nyoka anamaanisha nini katika ulimwengu wa roho.
MUNGU akubariki sana ndugu na kumbuka kuwa suluhisho pekee la yote haya na yote yanayowasumbua wanadamu ni YESU KRISTO na yeye mwenyewe katika Mathayo 11:28 anasema
MUNGU akubariki sana ndugu na kumbuka kuwa suluhisho pekee la yote haya na yote yanayowasumbua wanadamu ni YESU KRISTO na yeye mwenyewe katika Mathayo 11:28 anasema
Comments
Post a Comment