Kujifunza Neno la Mungu katika Mwanga wa Agano Jipya
Ni ya kuthibitisha ya kwamba tunajua baadhi ya sehemu fulani katika Neno la Mungu. Hi hakika itaweza kuongeza ufunuo wetu mpya na agano lilo bora
Tunapo soma Bibilia, ni ya kuthibitika ya kwamba tulitumie Neno la Mungu kwa usahihi, Kwanza yafaa tuone, makundi ya watu tafauti inazungumizia, la pili, yafaa tuelewe matukio faluni yaliyo fanya mtengo wakati huu. Ukweli ni kwamba wakati Yesu alipo kuwa akitembea duniani. Hangeweza kutupa ufunuo wote, licha Yake kuulenga ufunuo huo. Hii ni kwa sababu kazi Aliyo paswa kuifanya hakuwa ameikamilisha.Maandiko yanaeleza majira, kipindi cha ratiba ya Mungu, na maagano tofauti.Katikati mwake tuna pata msalaba wa Kristo. Kuna matungo ya mtengo wakati wa kifo, ufufuo, na kupaa kwa Yesu, na umwagikaji uliofuata wa Roho matakatifu wakati wa Pentakote. Yesu aliongea zaidi kipindi baada ya Pentakote. Alisema “Wakati huo mtajua kuwa Mimi niko ndani ya Baba na ninyi mkondani Yangu na Mimi niko ndani yenu. (Yohana14:20).
Kuna matungo ya mtengo wakati wa kifo, ufufuo, na kupaa kwa Yesu, na umwagikaji uliofuata wa Roho matakatifu wakati wa Pentakote.“Atakapokuja huyo Roho wa kweli atawaongoza awatie katika kweli yote.” (Yohana 16:13)
Paulo anaeleza mtengo huo katika kipindi chake na anazungumza kuhusu wakati “ kabla imani kuja” na “baadaya imani kuja” (Wagalatia 3:23-25).
Tuna tunuko kuu kuishi baada ya imani imefunuliwa, baada ya wazia kuwa katika utendaji(Waebra 9:16-17), na baada ya Roho kuja. Tuna ishi “katika siku hiyo” Yesu alizungumzia juu yake kwa bidii. Huu ni wakati anaweza kuongea wazi ketu sisi.
Makundi matatu
Msiwe kikwazo kwa mtu ye yote, kwa Wayahudi au kwa Wayunani, au kwa Kanisa la Mungu, (1 Wakor 10:32)Neno la Mungu lina gawa watu katika makundi matatu: Wayahudi, Wayuni, na kanisa la Mungu. Mimi nina shukurani kwa Rev Keneth Hagin, aliyefunguwa macho yangu kwa kanuni hii iliyo rahisi. Niliweza kushika hili soma kupitia mwelekeo wa Roho Mtakatifu. Usubuhi moja nilipo kuwa nikiombea hali fulani ambayo mimi kama mchungaji nilipaswa kusululisha, Roho Mtakatifu alininea mimi na akasema jawabu nililoskuwa nikitafuta lingepatikana katika baadhi ya mafundisho ya Kenneth Hagin, ambayo nilikuwa nayo kwenye kanda.Niliweza kupata jawabu nililo hitaji,walakini,pia niliweza kushika kitu ambacho kimikuwa cha msaada sana katika kujisomea Neno la Mungu. Ningili kiona wazi katika Bibilia. Unaweza kutaka kujisomea hii zaidi katika undani. Basi fungua 1 Wakori 10:32, 1 Wakori 9:19-23, Warumi 2:14-15, Matendo 15:19-21, Matendo12:25, na Wagalatia 2:7-8
Paulo hayupo chini ya Sheria, wala kukosa sheriaNi rahisi tu hivyo – makundi matatu ya watu na Mungu hufikia kila kundi katika njia tofauti. Ufunuo ambao Hagin alikuwa ana shiriki katika kanda hiyo, ilikuwa ni kwamba sheria tatu tofauti hutawala makundi tatu tafauti. Wayahudi wana Sheria ya Musa, Mataifa wana “ sheria ya dhamira,” na kanisa la Mungu lina “sheria ya Kristo” au “ sheria ya upendo.” Makundi haya yote yamo katika 1Wakori 9:20-21: Wayahudi wapo chini ya Sheria: Mataifa wapo chini ya Sheria. Paulo hayupo chini ya Sheria, wala bila sheria. Yeye yupo katika sheria ya Kristo. Hii ni wazi, na rahisi.
Mimi ni mwanafunzi asiye ponywa.Nina hitaji kuwa na zaidi ya Andiko moja katika kweli: ushahidi wa aina mbili au tatu ndiwo wa kiwango cha chini. Kweli yafaa iingiane na ukamilifu, na ni lazima isilete mashindano katika semi zingine zilizo wazi katika neno la Mungu. Wakati mwingine inaweza onekana kana kwamba Bibilia ina jipinga, lakini ni kwa sababu hatuonin muktadha
wote.Neno la Mungu kila wakati lina kubaliana lenyewe.
Kwa hivyo, Neno la Mungu hugawa watu katika makundi matatu, na sheria tofauti huongoza kila mojawapo ya haya makundi. Ukiweka haya niani mwako ni rahisi kuelewa ya kwamba tunaweza kubaliana na haya makundi matatu katika njia tofauti. Ni vema tujiulize wenyewe maswali faluni tunapo jisomea Bibilia, ili kwamba tukapate kuelewa muktadha.
Maswali ya kuuliza unapo soma Bibilia
Jambo lilo rahisi, na la msingi kwa kuelewa Maandiko ni kwa urahisi uliza:Ni nani anaongea?
Na kwa akina nani wanazungumzia?
Na wanazungumza juu ya nini?
Swali ya kwanza ni: “Ni nani anaongea?”
Mungu ameruhusu watu kunukuliwa katika Bibilia, pamoja na wajinga. Hata Shetani ananukuliwa mara nyingi. Katika kitabu cha Ayubu kuna sauti nyingi ambazo zimeruhuziwa. Na ni muhimu kuona ya kwamba Mungu ana zikemea katika sura ya 42, akisema,”…. Hamcha sema ya kweli kunihusu Mimi …..” Na Ayubu mwenyewe anasema nime wasikia, “Masikio yangu yalikuwa yamesikia habari zako,lakini sasa macho yangu yamekuona.Kwa hiyo najidharau mwenyewe na kutubu katika mavumbi na majivu.” (Ayubu 42:5-6) Hii ni habari iliyo muhimu sana. Yafaa usome sura za kwanza 41 za kitabu cha Ayubu katika mwanga wa haya hapo basi utakuwa una tumia kwa usahihi Neno la Kweli.
Mungu ameturuhusu kujiunga na utafiti ambako ukweli mwishowe una funuliwa. Na vita vingine vya mashairi vipo kama hizi- kwa mfano, kitabu cha Mhuburi. Ni muhimu kuelewa ya kwamba siye Mungu anaye tangaza, “ Yote ni ucbatili!”. Ni mhubiri katika kitabu hiki anaye sema haya katika kipindi fulani maishani ambako alikuwa amesumbukana, akitafuta ukweli. Mungu anaturuhusu kuhusika katika upitilizo huu, na watu wengi wanajitambua wenyewe.
Swali la pili ni:”Ni kwa akina nani inazungumziwa ?”
Timotheo anaambiwa anywe divai kidogo kwa ajili ya tumbo lake, hii si kama amri kwetu sisi wote kunywa divai. Upande mwingine, hapa mtume Paulo anatafsiri sheria ya upendo kuhusu hili jambo katika Warumi 14, na mwisho wake ni: tembea katika upendo!
Mengi ambayo Yesu alisema katika injili pia yafaa katika kujisomea katika mwanga wa nani aliye kuwa akimzungumzia. Mara nyingi alijibu mswali toka kwa Wafarisayo, na kwa kweli majibu yake yange husiana na Wayahudi chini ya Sheria na sio Mkristo aliye wa mataifa baada ya Pentakoste. Alisema waziwazi hivi, “ Sikutumwa ila kwa kondoo waliyo potea wa nyumba ya Israeli.”
Wakati mwingi Yesu alikuwa anazungumza kuhusu Sheria kwa wale watu waliyo chini ya Sheria, na katika hali ya kawaida katika utendeji wake kwa yule mtaifa aliye zaliwa- mara pili chini ya sheria ya Kristo sio sawa.
Hakika Mafundisho ya Yesu yana umuhimu kwetu sisi leo hii. Lakini yafaa tujifunze jinsi ya kutumia Neno la ukweli katika usahihi. Yafaa tulisome katika muktadha wake. Kwa mfano, wakati Yesu alipo sema na yule kijana tajiri kwamba ange okoka kwa kushika amri, alisema haya kwa sababu alikuwa akizungumza na Myahudi aliye chini ya Agano la Kale. Alijua, hakika, hakuna mtu anaye ishi kulingana sheria anaweza kujiokoa mwenyewe. Walakini katika tukio hili, alihusisha jawabu lake kwa ujumbe wa Mungu kwa Wayahudi. Leo hii jawabu lake kwa huyu kijana tajiri, lingekuwa tofauti kabisa. Sasa huu ujumbe ni “Kwa maana, “Kila mtu atakayeliitia Jina la Bwana, ataokoka.’’ (Warumi 10:13). “Mwamini Bwana Yesu Kristo,nawe utaokoka,…” (Matendo 16:31).
Nina amini unaweza kuona umuhimu wa kujua majibu ya haya mswali, na pia kwa swali la tatu: “ Je wana uliza kuhusu nini?” Mara nyingi Yesu alikuwa akiongea juu ya Sheria kwa watu walio chini ya Sheria, kwa kawaida kuweka katika utendaji kwa yule mataifa aliye zaliwa- mara ya pili chini ya sheria ya Kristo sio sawa sawa vile.Yote haya yata tusaidia sisi kama wafanya kazi ambao wana tumia Neno la Kweli kwa usahihi. Lakini kunayo zaidi.
Maandiko
Bibilia imegawanywa katika Agano La Kale na Agano Jipya. Wakati Agano jipya linalenga Mandiko matakatifu, “ ina sema juu ya Agano la Kale.Hiyo ndiyo Bibilia waliyo kuwa nayo. Agano Jipya ilikuwa bado kuandikwa. Yesu mara nyingi alisema, “ imeandikwa” au Je hamcha isoma?”Katika Matendo ya Mitume tunaweza kusoma kuhusu watu wa Beroya, na jinsi wali “ walipokea Neno kwa hamu na wakawa wanachunguza Maandiko matakatifu kila siku kuona waliyo sema kama ni kweli” (Matendo 17:11).
Mtume Paulo alitumia Maandiko katika hudumu wake, “kwa maana kwa uwezo mkubwa aliwakanusha hadharani Wayahudi, waliokuwa wakipinga akionyesha kwa njia ya maandiko kwamba Yesu ndiye Kristo.” (Matendo 18:28).
Kwa hivyo ni dhahiri ya kwamba ni ya faida ya sasa kwa Mkristo kuchunguza Maandiko - Agano La Kale.Tuna penda Bibilia toka kifuniko hadi kifuniko.
Lakini sasa tunaweza kuisoma katika mwanga mpya. Sasa tuna Agano Jipya linatoa jawabu kwa yale Agano la Kale ilikuwa ikilenga. Bibilia ina eleza kwamba vitu vyote vilitendeka kwa watu katika Agano la Kale ili wawe mfano kwa sisi ambao tuna ishi sasa. (1 Wakori 10:11).
Katika Injili na Matendo ya Mitume
Sehemu ya kwanza ya Agano Jipya ni ufunuo wa maisha ya Yesu.Tuna weza kusoma kuhusu maisha Yake na mafundisho na kuona yale Alitutendea kwetu sisi. Ni ya ajabu kufuata kwa akaribu Mwana wa Mungu, na kujua ya kwamba alikuja kutuonyesha jinsi Mungu alivyo.Mitume waliandika haya chini kulingana na vile Roho Mtakatifu alitaka wao kuyaandika. Hudumu wao ilikuwa ni kunakili maisha na safari za Yesu.Matendo ya Mitume ndicho kitabu kinacho fuata.Ni historia ya Wakristo wa kwanza. Maneno na ahadi za Yesu zina wekwa katika utendeji wakati huu, na msingi wa kanisa la Agano Jipya unawekwa.Hili ni soma lenye nguvu!
Nyakati za vitabu za Injili, Agano Jipya lilikuwa bado kuingia katika utendajiHata hivyo, kuna mambo ya muhimu ambayo mtu yafaa ajue. Katika kipindi cha vitabu vya Injili, Agano Jipya lilikuwa bado kuingia katika utendaji. Hii ndiyo sababu Yesu hakika anasema alitumwa tu kwa Wayuhudi pekee yao. Hudumu wake wa duniani ulilenga wao peke yao, licha ya maisha yake, kifo chake na ufufuo wake ni kwa ajili yetu sisi sote, na mataifa hata walio mbali sana
(Mathayo 15:24, Mathayo 10:5-6) Ni ya muhimu kuelewa kwamba Yesu mara nyingi alizungumza juu ya Sheria kwa watu walio chini ya Sheria, na kwamba Aliyo yasema, hapo, hayaleti maana kwa sisi tunao ishi baada ya Kalvari.
Basi natakupa mfano mwingine ili kwa uwazi nika onyeshe wewe matukio yenye uweza wa Kalivari ilizalisha.
Alitu Samehe Sisi ili Tu Samehe Wengine
Kabla ya Kalivari, Yesu alipo wafundisha wanafunzi Wake jinsi ya kuomba” kabla ya Pentekote,” utatambua kupokea msamaha kwanza ulipaswa kutoa msamaha. Jugumu likuwa juu yako, na alikuwa ni mwanadamu aliye hitaji kusemehe na kupenda kwanza, alafu Mungu ange semehe. Soma Mathayo 6:12, 14-15.
Ujumbe ni wazi. Hautapokea msamaha mpaka kwanzausamehe. Hii imeleta usumbuvu mkuu miongoni mwa watu ambao wamekuwa na wakati mgumu kusamehe wazazi walio watumia vibaya wakiwa watoto, au wanandoa wasio waminifu walio wakosea wapenzi wao. Washauri wengi wame lazimisha msamaha wa moyo unao kubala ulio nusu kwa watu ili walio wakosea wasemeheane.
Lakini Injili huleta habari njema, Inaleta msamaha kwa nafsi iliyo pakawa, na kuachilia msamaha wa kweli kuelekea wao wanao hitaji. Hapa kuna ujumbe:
“Iweni wafadhili na wenye kuhurumiana ninyi ninyi, mkisameheana, kama vile naye Mungu katika Kristo alivyowasamehe ninyi.” (Waefe 4:32).
Baada ya Kalivari mpangilio umebadilika! Na sasa hatuhitaji kusemehe ili tupokea msamaha, lakini tunahitaji kusemehe kama tunda tayari tumesha samehewa.
Kazi yake iliyo kamilika inatangaza kwa Kwa kujitoa Kwake, tayari Amesha fanya upatanisho kwa ajili ya dhambi za dunia, na sasa tume samehewa pale msalabani.
“kwa sababu Yeye kwanza alitupenda, tuna mpenda Yeye”. (1Yohana 4:19) Haitangulii na sisi- ina anza na Yeye. Kuelewa hii tofauti ni kuelewa Injili yenyewe.
Baada ya Kalivari mpangilio umebadilika!“Huu ndio upendo, sikwamba tulimpenda Mungu, bali Yeye alitupenda, akamtuma Mwanawe, ili Yeye awe dhabihu ya kipatanisho kwa ajili ya dhambi zetu (1 Yohana 4:10).
“Lakini Mungu anaudhihirisha upendo Wake kwetu kwamba: Tulipokuwa tungali wenye dhambi, Kristo alikufa kwa ajili yetu” (Warumi 5:8).
Lilianza na Mungu, na sio sisi. Yeye alitupenda kwanza, alitusemehe kwanza, na Alitufilia tulipokuwa tungali wenye dhambi.
Wakol 3:13 inathibitisha Waefeso 4:32 vema sana. “Vumilianeni na kusameheana. Mtu akiwa na lalamiko lo lote dhidi ya mwenzake, sameheaneni kama vile Bwana alivyowasamehe ninyi. Kwa hivyo nanyi lazima mfanye” (Wako 3:13)
Tena ni wazi ua kwamba nani aliye mtu wa kwanza kusamehe. Ni Kristo ambaye tayari asha samehe sisi.Hii ndiyo sababu lazima tusemehe.Ukombozi ulete huo utofauti : sasa tunaweza kujenga kwa yale tayari Asha fanya. Na upendo wake usha miminwa moyoni mwetu unaotuwezesha kusemehe wengine (Waru 5:5).
Je una ona tofauti kubwa iliyo kuja baada ya Kalivari? Masalaba umeacha alama za milele kwa historia, na agano mpya lilo bora lime kuja na msingi mpya na ulio bora.
Ufunuo ulikuwa bado kupeanwa
Ufunuo ambao Paulo alipokea kuhusu kanisa, na kuhusu injili kwa mataifa, ulikuwa bado kufunuliwa wakati Yesu alikuwa akitembea duniani. Kwa hivyo ni, haikuandikwa katika injili vitabu nne za Injili. Yesu anatuonyesha ufunuo wa haya, lakini bado ilikuwa haicha funuliwa. Anatoa “ishara” fulani ya unabii kuhusu haya, haswa katika Injili ya Yohana, lakini anasema, “Ningali nina mambo mengi ya kusema kwenye, lakini hamwezi kuyastahamili sasa”.
Yesu anaonyesha mgawanyiko ambao ulipaswa kuja baada ya kifo chake, na anasema, ““Nimewaambia mambo haya kwa mafumbo. Saa yaja ambapo sitazungumza nanyi tena kwa mafumbo bali nitawaeleza waziwazi kuhusu Baba. Siku hiyo mtaomba kwa Jina Langu….” (Yohana 16:25-26).
Tena alisema, “Bado ninayo mambo mengi ya Kuwaambia, lakini hamwezi kuyastahimili sasa.Atakapokuja huyo Roho wa kweli atawaongoza awatie katika kweli yote (Yohana 16:12-13).
Roho alikuwa amekuja kabla ya kuongozwa katika kweli yote.Hii ndiyo sababu Bibilia haingetimilizwa hapo awali baadaye Roho alikuwa asha kuja, na mtume Paulo apewa wito wa “kutimiliza Neno la Mungu.” Yesu alikuwa na mambo mengi ya kusema, ambako hakupata nafasi ya kushirika alipokuwa hapa, lakini sasa ameshiriki haya kwa kujifunua Yeye mwenyewe kwake Paulo.Katika wakati huu Ameeleza waziwazi na kwa uwazi kuhusu maana maisha Yake na Yeye kama dhabihu, na sio katika lugha ya mafumbo (Yohana 16:25).
Yesu alikuwa na mambo mengi ya kusema kwamba Hakupata nafasi ya kushirika alipo kuwa hapa, lakini sasa Ameshiriki kwa kujifunua Yeye mwenyewe kwake Paulo.
Agano Jipya katika Utendaji Baada ya Kifo
Katika ukweli ni ufunuo unasababisha vipande kuingia mala pake. Ufunuo ni kuelewa umuhimu wa msalaba wa Bwana Yesu Kristo!Hii ndiyo sababu mtume Paulo ana sema “ Yesu Kristo alithirishwa waziwazi miongoni mwenu kama aliye sulubishwa, na jinsi gani “msijue chochote miongoni mwenu ila Yesu Kristo na Yeye aliyesulubishwa.” Na hata jivunia lolote “ ila katika msalaba wa Bwana Yesu Kristo”.
Angalia yale Bibilia inasema: “Kwa habari ya wosia, ni muhimu kuthibitisha kifo cha yule aliyeufanya, kwa sababu wosia huwa na nguvu tu wakati mtu akishakufa, kamwe hauwezi kutumika wakati yule aliyeuandika akiwa bado yuko hai.” (Waeb 9:16-17)
Kwa hivyo Agano Jipya linaanza utendaji mwisho wa vitabu vya Injili. Tuna pata ufunua kidogo katika kitabu cha Injili ya Yohana, haswa katika sura za mwisho.Hapo Yesu anatoa unabii jinsi itakavyo kuwa baada ya Roho kuja.
Maagano ya Mungu ni “ maagano ya damu,” kwa hivyo Agano Jipya halingeweza kuanza kabla Yesu hachafa na kutoa damu yake.
Bibilia inahitaji kusomwa katika mwanga wa jambo hili lilo kiini:yaani msalaba wa Bwana yetu Yesu Kristo. Inahitajika kusomwa katika mwanga wa jambo hili ya kwamba Yesu alingia Patakatifu pa watakatifu, mpaka Mbinguni kwenyewe, kwa damu Yake, na ameketi chini kama Kuhani Mkuu kwa ajili kila baraka zote za wokovu ambazo sasa tuna ishi ndani.Alipo keti mbinguni,Roho alimiminwa kwetu. Hapo ndipo wakati “agano la Roho lenge anza.”
Utukufu Baada ya Msalaba wa Yesu
Mtume Petero anafundisha lile jambo kama mtume Paulo, tukitaja kuhusu msalaba kama gawanyo la wakati.Ana andika. “Kwa habari ya wokovu huu, wale manabii walosema kuhusu neema ambayo ingewajia ninyi, walitafuta kwa bidii na kwa uangalifu mkubwa, wakijaribu kujua ni wakati upi na katika mazingira gani ambayo ndani yao Roho wa Kristo aliyokuwa akionyesha alipotabiri kuhusu mateso ya Kristo na utukufu ule ambao ungefuata”.Katika maneno mengine, walipo yaona ilikuwa ni mateso ya Kristo (msalaba) na na utukufu ungelifuta. Walitabiri kuhusu kipindi cha majira fulani, wakatafuta ni nini, au ni wakati gani, walikuwa wakitabiria juu yake.Waliona hapo mwanzoni utukufu ambao sasa tuna ishi ndani - sisi tunao ishi baadaya ya Pentakoste, wakati wa Agano Jipya.
Walione mapema utukufu ambao tunaishi ndani- sisi tunao ishi baada ya Pentakote, wakati wa Agano Jipya.
Tokea wakati wa Yohana mbatizaji mpaka Pentakote
Tukisoma sana kwa uangalifu, tuta kuja kuona tokea wakati wa Yohana Mbatizaji mpaka Pentakote ni mgawo mwingine wa majira. Wakati huu Injili ya ufalume wa Mungu ilihubiriwa na iliwezekana, kujiingiza ndani yake” au “kuteka kwa nguvu”.‘‘Torati na manabii vilitumiwa mpaka kuja kwa Yohana Mbatizaji. Tangu wakati huo habari njema za Ufalme wa Mungu zinahubiriwa na kila mmoja hujiingiza kwa nguvu.” (Yohana 16:16)
“Amin, nawaambia, miongoni mwa watu waliozaliwa na wanawake, hajatokea mtu aliye mkuu zaidi ya Yohana Mbatizaji, lakini aliye mdogo kabisa katika Ufalme wa Mbinguni, ni mkuu kuliko Yohana. Tangu siku za Yohana Mbatizaji hadi sasa, Ufalme wa Mungu hupatikana kwa nguvu, nao wenye nguvu wauteka. (Mathayo 11:11-12)
Watu wengine husoma haya na kuamini ya kwamba Agano Jipya lilianza na Yohana Mbatizaji, lakini sasa hapo “ hautumie neno la ukweli kwa ushahihi.” Kwanza, Mathayo 11:11 inaonyesha ya kwamba Yohana Mbatizaji hakuwa amezaliwa mara ya pili na kwa sababu hii alikuwa mdogo kamwe katika ufalme.Unahitaji kuzaliwa mara ya pili ili uingie katika ufalme wa mbinnguni (Yohana 3:3-5 ), na ilikuwa ngumu kuzaliwa mara ya pili kabla ya ufufuo wa Yesu.Yesu alipaswa kufufuka toka wafu, “ ili awe mzaliwa wa kwanza katika wengi” (Warumi 8:29 na Wako 1:18).
Walakini, majira na kipindi tokea Yohana Mbatizaji kufikia Pentekote, mmoja ange chukuwa baraka za ufalme kwa nguvu.Hii ndiyo sababu wakati huo walipata kuona msamaha wa dhambi na uponyaji kuliko wakati mwingine wowote. Hata Mataifa, ambao hawakuwa kati yao “wale watoto” ambao mkate ulikuwa ni wao, ambao ni Wayahudi, walichukuwa ufalme kwa nguvu—, licha ya Mataifa kuitwa “mbwa” (angalia. Matt 15:22-28 ).
Majira ya kipindi tokea Yohana Mbatizaji hadi Pentekote ilikuwa kipindi muhimu cha untangulizi.Yesu alikuwa anatembea duniani na ufalme wa Mungu alikuwa umekaribia.
Walakini,wakati mpya mkamilifu ulianza baada ya Kalivari. Sasa uadui ukakomeshwa, Mataifa wana husika, na sasa ametuleta katika ufalme wa Mungu.
Yesu alitabiri Zaidi Kuhusu Nyakati Tunazo Ishi Sasa
Wakati Yesu alikuwa karibu kuondoka aliongea kuhusu Agano Jipya na nyakati baada ya Pentekote.Alisema, “ Nami kama Baba Yangu alivyonipa ufalme, kadhalika mimi nami ninawapa ninyi.” (Luka 22:29)‘‘Msiogope enyi kundi dogo, kwa maana Baba yenu ameona vema kuwapa ninyi Ufalme.” (Luka 12:32)
Ufalme we Mungu ulikuwa uje kwa nguvu, na sasa hakuna ambaye ange “ uteka kwa nguvu” au “kuingia ndani yake.”“Yesu akaendelea kuwaambia, ‘‘Amin, amin nawaambia, kuna watu waliosimama hapa ambao hawataonja mauti kabla ya kuuona Ufalme wa Mungu ukija katika nguvu.’’ (Mariko 9:1)
Katika maneno mengine : Ufalme wa Mungu ulikuwa uje katika nguvu, na sasa hakuna ambaye ange “ teka kwa nguvu” au “kuingia ndani yake.” Kwa uhakika mmoja haitaji kufanya hivyo wakati “ ufalme umeletwa kwetu” na ilikuwa ni furaha ya Baba ilio njema kutupa sisi ufalme “kuingia kwa nguvu ndani yake” imekwisha.
Tumeingizwa Katika Ufalme wa Mungu
Angalia ni vipi hii ni tofauti baadaKalvari: “Kwa maana alituokoa kutoka katika ufalme wa giza na kutuingiza katika ufalme wa Mwana Wake mpendwa.” (Wakolos 1:13)Tupo ndani, na sio inje! Hatuchukuwi kwa nguvu - tunaishi ndani yake.Hii ilitendeka bila nguvu zozote upande wetu; tuli kuwatulipelekwa katika ufalme wake. Ilikuwa Yeye aliyetenda haya—na sio sisi. Hatukuhitajika kuteka kwa nguvu – Alituweka ndani yake. Na sasa tumewekwa katika ufalme wa Mwana wa pendo Lake, kwa hivyo hatusimami inje yake tukijaribu kujisukuma ndani au kuteka kwa nguvu. Sisi tusha pelekwa ndani ya ufalme.Tupo ndani, na sio inje! Hatuchukuwi kwa nguvu- tuna ishi ndani.Tunapo hubiri ya kwamba Wakristo yafaa wajingize kwa nguvu ( Luka 16:16 na Mathayo 11:12), tunapuuza ile kazi kamili ya Kristo, jinsi inavyoletwa katika Wakolosai 1:13.
Injili kulingana na Paulo –katika tafsili ya maandiko nyekundu
Miaka michache zilizo pita kanisa letu lilipata tunuku la kuwa na mkutano ulikuwa na mwinjilisti anaye julikana kwa jina Dk. T.L Osborn. Katika mazungumzo yetu, alisema kitu kilicho toa ushahidi kwa moyo wangu. Alisema anatumai mtu ange toa chapa ya tafsili ua maandiko nyekundi ya barua za mtume Paulo, ambako kila kitu ambacho Paulo anasema kuhusu ukombozi, na kazi ya msalaba ingetolewa chapa nyekundi, na yaliyo baki yatolewe chapa katika rangi nyeusi. Alisema kwamba tuna injili kulingani na Mathayo, Mariko, Luka na Yohana, lakini injili ya Mataifa- ambayo ni sisi- ni injili kulingana na Paulo, na kwamba, hii yafaa itolewe chapa katika maandiko ya rangi nyekundi.Unaona, Mathayo, Mark, Luka na Yohana wana tuambia zaidi ya yale yaliyotendeka, “ yaonekanayo” ikilinganishwa na mauti na ufufuo wa Yesu. Tuna soma kuhusu kusulubisha, lile kaburi, ufufuo, malaika, na kuhusu Yesu aliyefufuka anaye jifunuwa Yeye mwenyewe.
Lakini ni mtume Paulo anaye tuonyesha matokeo ya rohoni kwa yale yaliyotendeka! Anaeleza ya kwamba tulikufa na Kristo,tukafufuka na Yeye, na tumeketi na Yeye Mbinguni.
Yeye anatuonyesha vilindi vya ukombozi, na anaeleza ya kwamba Yesu alifanyika dhambi kwa ajili yetu ili tuwe haki ya Mungu katika Yeye. Barua zake zinafunua sisi ni akina nani katika Kristo na yale Kristo aliye ndani yetu.
Siri ya Kanisa imefunuliwa, na vipande vyote vimewekwa pamoja, ili tuweze kuona picha yote katika hali ilipokuwa imefichwa hapo awali. Hii inahusisha nyakati za Injili na nyakati Yesu alipo tembea hapa duniani.
Hii ndio sababu barua za Paulo lazima ziwe na mahala malumu katika maishani mwetu sisi tulipokuwa Mataifa lakini sasa tupo sehemu ya Kanisa. Sisi tumepindukizwa katika msabibu, na Paulo, aliye “Mtume kwa Mataifa,” yeye amepewa jugumu la kufunuwa injili kwa “wasiotairiwa”.
Hii sio kupunguza umuhimu wa Agano Jipya au injili, ila ni kutuhimiza sisi kusoma Bibilia katika mwanga wa Injili! Iwapo tutakosea kupata ufunuo katika Bibilia na katika mpango wa Mungu, tumesoma Bibilia kupitia miwani yaliyo na giza ambayo yanapufusha mtizamo. Kuna miwani nyingi yenye giza ambayo mila na dini zimetupatia.
Unaweza kushanga, kwa nini nina sema barua za Paulo zitolewe chapa katika maandiko nyekundu, ile rangi ambayo maneno ya Yesu katika injili yalitolewa chapa nayo. Labda unafikiri hii ina tia chumvi umuhimu wa Paulo. Na unaweza kushanga kwa nini nina sema tu sehemu fulani ya barua zake yafaa zitolewe chapa nyekundu- sio maandiko yake yote. Na tuangalie haya.
Kwanza, Paulo ana andiko kueleza ufunuo wake wa injili. Hakupokea haya kutoka kwa mwanadamu, ila ni kutoka kwa Yesu Kristo Yeye mwenyewe ( Wagalatia1:11-12).
La pili, ana andika baada ya Mshauri amekuja. Na sasa Yesu anaweza kushirika pamoja nasi kila kitu Alitaka kutuambia sisi, lakini hangeweza, kwa huo wakati Alikuwa hapa. “ Ile Siku” Yesu alitazamia na kulenga imekuja (Yohana 16:25).
Siye Paulo aliye mtu wa muhimu, lakini ufunuo Yesu alimpa. Siye karani ndiye aliye mkuu, lakini yule anaye amrishwa kitabu.Kwa hivyo, jambo ni, Paulo ni karani tu. Yeye ana andika ule ufunuo alio upata toka kwake Yesu aliyefufuka. Yafaa tuelewe ufunuo wa Paulo. Siye Paulo ndiye aliye wa muhimu, lakini ufunuo ambao Yesu alimpa yeye. Siye karani aliye mkuu, ila ni yule anaye amrishwa kitabu. Hii ndiyo sababu haya maneno pia yanawaeza chapishwa katika rangi nyekundu. Sisi hatumsifu Paulo. Kinyume chake, tuna msifu Yesu, aliye mwiita na kumpaka mafuta mtume Paulo na kumpa huduma wa kutimiliza Neno la Mungu, jinsi nilivyo sema hapo awali.
Tatu, Paulo anaitwa mtume kwa Matiafa, na ni yeye Mungu alimwita na njia ya kipekee kuhubiria Mataifa, wasiotairiwa, kama vile Petero aliitwa kufikia walio tairiwa. Jambo hili kwamba Mataifa walipaswa kuhusishwa ilikuwa baadhi ya hiyo siri ilifunuliwa kwake Paulo.Tuta angalia hayo baadaye, lakini lengo langu hapo ni Paulo alikuwa anapanda makanisa, na Babilia inasema alikuwa “na wajibu mkuu kwa makanisa”
(2 Wakor 11:28) Kama baba wa makanisa aliandika barua kusaidia wao na mambo fulani iliyo husu maisha ya kila siku katika makanisa. Alihitaji kuzungumzia mambo fulani kwa lile kanisa la Wakorintho, na mambo mengine kwa makanisa mengine. Katika barua kwake Timotheo, ana mhimiza na kumwelekeza Timotheo jinsi ya kuwa kiongozi katika kanisa. Haya mambo kwa uhakika ni muhimu kwetu sisi, na tuna jifunza mengi toka kwayo, ila haya si sehemu ya ile siri iliyo kuwa imefichwa toka vizazi na karne. Kwa hivyo kurusa kama hizo haziwezi kuchapishwa katika nyekundu.
Katika Waefeso1 na 2, tuna weza pata tafsili iliyo tilia mkaso ya ujumbe Paulo alipewa.Katika Waefeso 1 na 2, tuna weza pata tafsili iliyo tiliwa mkaso wa ujumbe Paulo alipewa (jinsi Paulo anaeleza katika Waef 3:1-6 ) Katika Waef 1 na 2, kuna tu salamu fupi, na sasa anaenda “akilenga kusudi lake,” ili kusema. Hapana kutachwa kwa mambo yanayo husu mwandamu au kama hiyo. Paulo anasema, “unapo soma, utaweza kuelewa maarifa yangu katika siri ya ajabu ya Kristo.” Hizi sura mbili ndizo za tabia halisi ya siri iliyo funuliwa kwake Paulo.
Nina taka kila wakati nikalenge macho yangu kwa injili ya neema, na kwa hivyo, juma haliwezi kupita bila mimi kusoma hizi sura mbili. Paulo anaeleza zaidi juu ya ujumbe huu katika barua zake zote. Maandika nyekundi yanaweza kupatika mahala pengine pengi, lakini Waefeso 1 na 2 inaweza chapishwa katika nyekundi.
Barua za Petero na Yakobo
Siye Paulo pekee yake aliandika Agano jipya. Iwapo tutachukuwa ya kwamba Paulo ndiye mwandishi wa kitabu cha Waebrania, tungali tuna barua za Petero, Yakobo na Yohana. Hizi pia zimepeanwa na Mungu, na zinafaa katika kujenga, kuhimiza na kufariji.Lakini katika Wagalatia 2:7-8 Tuna soma kuhusu mgawo wa kazi, Petero aliitwa kufikia waliotairi, na Yakobo alikuwa mchungaji wa kanisa katika Yerusalem- kanisa lilo jawa na Wayahudi wa aina ya kimasihi. Kulingana na Matendo ya Mitume 21:20 wengi wao walikuwa” shauku ya sheria”.
Kwa asili, zile barua za Petero na Yakobo yalikuwa maandiko kwa makundi ya hawa watu. Utangulizi wa hizi barua hakika unaonyesha hizi zilikuwa za Wayahudi walio okoka. Hii pia ndiyo inahusu barua ya Waebrania.
Hizi barua pia ni Neno la Mungu. Na zina ujumbe kwa Mataifa, too. Yafaa tukumbuke zime andikwa kwa “ wailiotairiwa,” Na wakati Paulo haswa aliwandikia “wasiotairi”. Hapo tutakumbuka kusoma Bibilia katika mwanga wa maneno ya Bibilia, na hapo tuta tumia Neno la Ukweli kwa usahihi.
Soma Bibilia katika mwanga wa maneno wa Bibilia
Zile Barua za Yohana na ufunuo wa Yohana
Hakika barua za Yohana zipo katika mapatano yake. Yeye pia, alikuwa na wito kwa walio tairiwa.Lakini kulingani na Hitoria ya Kanisa, Yohana aliwendea Waefeso katika siku zake za mwisho. Kwa hivyo katika kitabu cha ufunuo tunaweza kuona alikuwa na mawasiliano na makanisa yaliyokuwa kule Asia. Haya ni makanisa ambayo Paulo ambayo na wafanya kazi wenzake walianzisha na waliyaendeleza. Wana historia wengine wanasema Timotheo alianza kufanya kazi kwa ukaribu na Yohana, baada ya kifo cha Paulo katika mwaka wa 67 AD. Timotheo alikuwa na shukurani kwa mafundisho ya Yohana ambayo yalikuwa dawa ya kuaribu sumu ya Wapinga Kristo.Hili funzo lina ng’aa kupitia barua za Yohana.Tunaweza kuona ya kwamba Yohana anakubaliana na mafundisho ya Paulo kuhusu uumbaji mpya na amri mpya.Tamatisho
Bibila yote ni neno la Mungu na linafaa kwa mafundisho, kuonya, kusahihisha na kuelekeza katika haki, lakini kwa jumla yanayo husu Agano Jipya yote ni yale yalifunuliwa kupitia Paulo.“Kila andiko, lililovuviwa na Mungu” (2 Timotheo 3: 16 ). Lakini inafaa tusome Bibilia katika mwanga wa yale ina sema yenyewe.
Comments
Post a Comment