USIANO WA VITI VYA ENZI NA MAFANIKIO YAKO MWL:C.Mwakasege Venue:Jangwan Siku ya SABA
UHUSIANO WA VITI VYA ENZI NA MAFANIKIO YAKO
Siku ya saba
* Ufunuo 13: 2 na 7: a yule mnyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na kinywa chake kama kinywa cha simba, yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi., ...Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa.
*
Namna ya kufanya unapokuta mafanikio yako yamekwamisha na viti vya enzi
1. Mambo ya kujikumbusha
1. Shetani anaweza kutumia kiti chake cha enzi kama silaha ya kupinga mafanikio yako ya kimungu na ya kawaida...Yule joka ambaye anawakilisha shetani/mpinga kristo anatafuta wa kumpa kiti, mamlaka na uweza kuwapiga vita watakatifu. Utakatifu ni kutengwa kwa ajili ya kusudi lake, iwe kitu au mtu.... Kumtumikia Mungu haina maana unasafari ya mbinguni bali ukimtumikia atahakikisha unaenda
2. Kiti cha enzi ni nafasi iliyoko ktk ulimwengu wa roho, nafasi yenye mamlaka juu ya maisha na mwelekeo wa maisha ya watu..Mwaka jana nilikumbusha mfano wa neno mwenyekiti linatumika bila kujua uzito wake ktk ulimwengu wa roho,...mnaweza kuwa watu kumi na kuambiwa mjichague mwenyekiti mnaweza wote kuketi laini bado manachagua mwenyekeiti na huyo anakuwa na mamlaka...mkimchagua akikubali anachukua nafasi na kuchukua mamlaka..mambo yakimzidia utasikia akisema kiti kimeongea akitumia ile mamlaka
3. Kila aliyeokoka anayo nafasi na uhalali wa kuketi na Yesu kwenye kiti chake cha enzi...Efeso 2: 6 akatuketisha ktk ulimwengu wa roho.....Efeso 1:21...ktk ulimwengu wa roho ni juu sana.....ufunuo 5:9-10 "Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuzifungua muhuri zake; kwa kuwa ulichinjwa, ukamnunulia Mungu kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,
10 ukawafanya kuwa ufalme na makuhani kwa Mungu wetu; nao wanamiliki juu ya nchi."..Nao wanamiliki juu ya nchi...Mungu anakuokoa ili ktk uzima wa milele ulionalo uwe mfalme na kuhani kkt kristo ili umiliki pamoja naye hapa duniani kama shetani nae atafutavyo watu wa kila lugha jamaa........Yesu anajua kwamba shetiani anatumia kiti na ndio sababu Yesu anataka utumie kiti chake cha enzi kupambana
4. Ili uwe na mamala ya kutumia nafasi uliyopewa ni lazima uketi.....Ufunuo 3:21...Yeye ashindaye nitamapa kuketi...Mfano: wewe ni mwanamke umeolewa, ni mfanyakazi, mfanyabiashara na ni mkristo kwahiyo una maeneo 4....nyumbani, kazini, kanisani, biasharani, ktk agano jipya tuna kiti cha enzi cha Yesu kinaweza na hiki kinaweza kuwa na majukumu tofauti tofauti kulingana na eneo..hiki kinakuruhusu eneo lolote unalotaka kuona mafanikio...kama unahitaji mafanikio ni lazima ujifunze kuketi na kristo ktk lile eneo unalotumika....Chukua/tumia nafasi yako.Mtu anaweza kuketi na kristo kanisani lakini mataani asiketi na kristo na hivyo analalamika kama wengine mtaani juu ya changamoto zilizopo...ukishaona hivyo ujue hujaketi....Ukiamua kuketi maeneo mengi unakuwa na vita nyingi zaidi...kibiblia unaweza pata nafasi ya kushikilia ofisi,kanisani na mtaani...maana kiti cha enzi kina nafasi kubwa....Kuna mamlaka ambayo wakristo wanajaribu kuyatumia wakati hawajaketi na hii inapelekea wao kushindwa....ukiwa meneja haina maana umeketi, kwenye ulimwengu wa roho, ukikubali na kusign haina maana umeketi ktk ulimwengu wa roho. ktk ulimwengu wa roho unahitaji kuketi ili kusimamia kusudi la Mungu. Ufalme wa Mungu ukisimama mahali ina maana haki, amani vitatawala.....Kama watu watakuwa wanaomba kwa miungu mingine na Wewe ukaomba kwa MUNGU wako, wenzako wanakuja na kiti wao watakushinda kwa sababu wao wanatumia kiti wewe hutumii kiti...
Hatua nne za kufanya baada ya kugundua vita kuna vita inayozuia mafanikio yako kutoka kwenye kiti
1. Hakikisha umeketi pamoja na Kristo..umekuabli kutumika kwa ajili ya ufalme wa mbinguni mahali ulipo..Hakuna haja ya kukubali nafsi na usionekane ofisini...ufunuo 3:21 "Yeye ashindaye...nitampa kuket"...Kwa nini shetani anakupiga vita usichukue hiyo nafasi? kitu gani anacho ogopa wakristo wakiketi kitatokea?
Tuangalie kidogo kiti cha enzi
* Ufunuo 4:1 -11
* Una uamuzi wa kuketi au kutoketi pamoja na Yesu, ukiona tunasoma habari za kiti cha enzi kile unachokiona kimeandkiwa ujue kinakuhusu na wewe kama umeketi kwenye kiti
* Kiti kilikuwa na upinde wa mvua..hii inaonyesha mungu ndiye ashikaye maagano na ukiketi hakuna atakeyweza kukubandua hapo
* Ishara ya Upinde wa mvua ni agano
* Fikiri umeketi pamoja na Kristo na ule umeme na ngurumo zinapotoka na wewe uko hapo, zile Roho saba za Mungu zipo hapo
* Ufunuo 5:11: Nikaona nikasikia sauti ya malaika wengi pande zote za kile kiti cha enzi, na za wale wenye uhai, na za wale wazee, na hesabu yao ilikuwa elfu kumi mara elfu kumi na elfu mara elfu,
* Ezekiel 10:1 "1 Ndipo nikaangalia, na tazama, katika anga lililokuwa juu ya vichwa vya makerubi, kulionekana juu yao kana kwamba ni yakuti samawi, kuonekana kama mfano wa kiti cha enzi.
* Isaya 6: ""1 Katika mwaka ule aliokufa mfalme Uzia nalimwona Bwana ameketi katika kiti cha enzi, kilicho juu sana na kuinuliwa sana, na pindo za vazi lake zikalijaza hekalu.
2 Juu yake walisimama maserafi; kila mmoja alikuwa na mabawa sita; kwa mawili alifunika uso wake, na kwa mawili alifunika miguu yake, na kwa mawili aliruka.
3 Wakaitana, kila mmoja na mwenzake, wakisema, Mtakatifu, Mtakatifu, Mtakatifu, ni Bwana wa majeshi; dunia yote imejaa utukufu wake. "
* Yeye ashindaye nitampa kuketi na maandiko pia yanasema yeye alivyo ndio tulivyo
* Cheki vitu vilivyo kizunguka kiti cha enzi na ukisha kaa pale shetani anagogopa maana mamlaka uliyo nayo hawezi kupambana nayo.....ijapokuwa hata acha kujaribu kupambana
* Yeye aliye na siko na sikie., .imani huja kwa kusikia... vita ya kwanza atakayo ileta shetani ni juu ya imani....atacheza na wewe kwa kutokujua ya kwamba hiyo nafasi ina mamalaka
2. Jifunike kwa damu ya Yseu ikulinde
* Usianze kupambana na kiti bila kujifunika na damu ya yesu, wewe pamoja na eneo unalo pambana
* Math 23:1 -2..Musa alikuwa na kiti,
* Kutoka 11:4-5...Mungu hakumruhusu musa kwenda bila ya kuketi. alipokataa musa ilibidi haruni apewe kiti ili kiti kiende vitani kwa farao
* Ebrania 11: alichinja sadaka ya kondoo ili damu iweze kuwalinda kwa kupakwa kwenye miimo ya mlango
* Pigo lisiwapete na shetani atakapo amka na hasira asiwapate
* kama kiti kimeshikilia wazaliwa wa kwanza, au unaenda kuombea wazaliwa wa kwanza..uwe na uhakika shetani atalenga wazaliwa wako wa kwanza
* Kama Mungu amekupa kiti ofisini na unaanza kupamba na kiti kilicho kabla basi linda sana ofisi usije kufukuzwa kazi..unahitaji ulinzi.. usipigane ofisini bila ulinzi utafukuzwa
* Kama unaomba juu ya familia basi weka ulinzi juu ya ndoa yako , maana unaenda kupigana na kiti ambacho kinaweza sema hii ndoa haipo
* Kama uko kwenye biashara, linda kwanza biashara usije kosa wateja, filisikia au kupoteaza tu hamu ya kuendelea kufanya biashara
* Lind haya maeneoe kwa damu ya Yesu
* Unapoombea mtaa wako linda nyumba yako maana utapata mapambano tu
* Unapoenda kupamabana viti vya miungu linda imani yako....
* Kama uko kwa ajili ya kumuombea mtu/mchungaji basi linda imani yako, linda mwili wako maana utasikia kuchoka na kwa jinsi ya kawaida hutaweza kuomba
* Tafuta watu wote wanoombea watumishi uone kama wana stamina ya kuomba kwa muda mrefu..sheati atatafuta kila nija ya kuwapinga ..wataletewa habari mambaya juu ya yule mtumishi ili kukata tamaa
* Kama mch wako amekaa kwenye kiti na wewe unamuombea basi utapigwa vita juu ya imani yako
* Linda imani yako, huwa na waombea wale ambao wanatuombea ili wasije wakapigwa na imani yao ilindwe
* Kama unaombea kiti na uko kwenye kanisa mablo lina kiti chaezni kama pergamo chunga uhai na imani na mafundisho upatayo
* Kama unaombe kiti ktk familia cheki maisha yako, gidioni alifanya hivyo likamletea matatizo...likatoka tangazo tumuue...unaweza futwa kwenye ukoo huko kwenye nguvu za giza na baada ya muda unaweza kufa kiajabu kwa sabau yakutojua sheria ya vita
3. Omba toba kwa ajili ya kile kilicho sababisha kiti cha enzi cha shetani kikapata nafasi na kutumika kuwamisha mafaniko yako
* Ufunuo 2: " Basi tubu; na usipotubu, naja kwako upesi, nami nitafanya vita juu yao kwa huo upanga wa kinywa changu."...
* kwa nini Yesu hakupambana na kiti cha shetani kanisani..bali akamwambia tubu na ha kuzungumza na shetani aliyeweka kiti kanisani?....kwa nini atubu?.... kwa sabau kuna kiti cha shetani kimepata nafasi kanisani
* Zaburi 89:3 -4 : " Nimefanya agano na mteule wangu, Nimemuapia Daudi, mtumishi wangu. 4 Wazao wako nitawafanya imara milele, Nitakijenga kiti chako cha enzi hata milele.
* "Kiti cha enzi hakiji hewani", kinetengenezwa na Mungu au shetani
* Kiti lazima kije na agano
* kama ni wewe au si wewe umehusika kwenye agano,au kuna kama kuna mtu kaingia agano, agano litabaki pale pale hata kama mtu aliyeingia kaondoka kwenye ile nafasi
* Toba inaondoa uhalali wa shetani kuendelea kukalia kiti
* Jifunze kuweka damu ya Yesu kwene agano
* Watu wengi wanapookoka wanafundishwa kuukulia wakovu bila kujua agano
* Agano linatoa nafasi ya kiti
4. Omba Mungu ahukumu juu ya miungu inayotumia kiti hicho kulicho kwamisha mafanikio yako
* Kutoka 12:12 "Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami nitawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wa mwanadamu na wa mnyama; nami nitafanya hukumu juu ya miungu yote ya Misri; Mimi ndimi Bwana."+ Hesabu 33: 4: "hapo Wamisri walipokuwa wanazika wazaliwa wa kwanza wao wote, Bwana aliokuwa amewapiga kati yao; Bwana akafanya hukumu juu ya miungu yao nayo"
* Kwa kuwapiga wazaliwa wa kwanza alikuwa anahukumu miungu
* Zaburi 89:14 "Haki na hukumu ndio msingi wa kiti chako, Fadhili na kweli zahudhuria mbele za uso wako."
* Kazi ya msingi ni kushilkilia kilicha juu
* kiti kina msingi na si agano tu
* kiti cha daudi kina kilikuwa na msingi wa haki na hukumu
* Nguvu za shetani zinatoka kwenye mazabahu za miungu na kiti chake ni kwa ajili ya kutengeneza mfumo
* Kiti bila madhabau hakina nguvu
* madhabahu bila kiti ni nguvu bila sheria
* ufunuo 13: 2 " Na yule mnyama niliyemwona alikuwa mfano wa chui, na miguu yake ilikuwa kama miguu ya dubu, na kinywa chake kama kinywa cha simba, yule joka akampa nguvu zake na kiti chake cha enzi na uwezo mwingi"
* Aliyepewa zile nguvu ni mnyama
* Mtu yeye anayetaka kiti cha shetani anachukua kwa mnyama
* mwanadamu lazima amtafua mnyama
* unaweza kuta mtu au kijiji kuna mnyama na hawamuui
* Huyo manyma saa nyingine ndie anayetaka kutolewa sadaka ili kulipa nguvu agano
* Mungu alipiga wazaliwa wa kwanza wa Farao kwasababu nguvu za ufalme wa farao zilikuwa juu ya kiti cha mzaliwa wa kwanza
* Kuhukumu maana yake ni kutenga kwa ajili ya adhabu
* takasa ni kutenganisha kwa matumizi
* Ukiomba hukumu kwa ajilia ya miungu maana yake ni watenganishwe na nguvu iliyo ktk miungu na adhabu ije juu yao
* Lazima ujue ukiketi na kuamua kuomba na kupambana nao lazima watakuja kukufuatilia hakikisha umeketi ili wakija wakute umzungunkwa na malaika na makerubi na nguvu za Mungu
Comments
Post a Comment