UHUSIANO WA VITI VYA ENZI NA MAFANIKIO YAKO Mahali; Jangwani Mnenaji;Mwl C.Mwakasege Day:1 Date:1/3/2015

UHUSIANO WA VITI VYA ENZI NA MAFANIKIO YAKO

Mahali; Jangwani
Mnenaji;Mwl C.Mwakasege
Day:1
Date:1/3/2015

Nini Maana ya Kiti cha Enzi

Ni nafasi ya utawala ambayo iko katika ulimwengu wa Kiroho yenye mamlaka juu ya mwelekeo wa maisha ya watu

Nafasi hii utikuta katka ngazi tofauti
1.Siasa
2.Familia
3.Huduma
4.Taifa
5.kabila
6.Kanisa
7.Ofisini
8. Biashara
9. Jamii n.k

Kimuonekano kunaweza kikawa ni kiti cha kawaida mf:kanisani au maaskofu anapokua hayupo huwa kiti chake kinafunikwa au hakiruhusiwi mtu kukalia kwa ishara ya kwamba amepewa heshima na watu wanaomzumguka na anaongea kwa kiti sio kama yeye.

Mat 23:1,2
Kutok 3:9,10
Kutk 4:12-16

Musa alipokufa kiti chake kiliendelea kubaki na Mungu alimpa Nafasi ili aheshimike Kiroho na kiutawala

Mungu akikupa kiti anaheshimu sana na kusikia maneno yanayotoka kwa Yule aliyeko au aliyekalia hicho kiti.

Mat 22:14
Shetani hana shida na na waitwao ana shida na Mteule au wateule
Mf:katika uchaguzi wa nafasi au kiti cha Urais waliopeleka kugombea nafasi hizo kutoka katka vyama vyao wao ni wateule katika chama chao ila katka tume ya uchaguzi ni waitwao na atakayepita katka mchakato na kuwa Rais yeye ndiye Mteule.
Rais akisimikwa ndio anakuwa mwenyekiti maana hawezi kuwa mwenyekiti wakati yuko Rais mwengine ambaye bado hajaachia kiti.

Ufunuo 3:21
Efeso 2:6
Efeso 1:20

Katikati ya kuchaguliwa na kuketi kuna mapambano makalo kwa hiyo huwezi kuketi bila kushindana au kupambana.

Ufun 13:1,2,7,9

Shetani akikuvuruga katka kusikia kwako ina maana kavuruga imani yako.

Ni hatari sana kwa kanisa kutegemea upako kuliko kukaa katka kiti

Ufunuo 2:12-17
Matendo 1:8

Antipas alikua na uwezo wa kuhubiri lakini alikuwa hana mamlaka ya kulinda kazi ya Mungu na usalama katka kile anachohubiri na aliyekaa ktka kiti cha peligamo ni mchungaj wake ambae alikaa katka kiti cha enzi cha shetani

Sifa ya kanisa la peligamo ni walikuwa na kiburi cha uzima na walikuwa vuguvugu.

Ufunu 22
Mungu aliweka Kiti katika Hema alilotengenezewa na wana wa Israel.

Kazi ya kiti ni kutengeneza mazingira ya kiroho na kupitisha mambo na kulinda mambo yaliyopitishwa kiroho.

Mf: Wamama walioolewa katka makanisa ambayo mume wao amekaa katka kiti cha enzi cha shetani cheki viroho vyao!

Cheki nchi ambayo wamesema itaongozwa kwa minajili ya kiislam cheki wakristo walioko unakuta hawana uhuru na usalama wa viroho vyao

Yerem 1:10

Ukiwa na mamlaka ya kiti au ukikaa katka kiti umepewa mamlaka ya kuvunja, kung'oa, kubomoa na kuharibu vitu vya shetani then upande na ujenge vitu vya Mungu.

Kama kila anayekataa kiti eidha cha uongozi je nani atakayebomoa?na huwezi bomoa,kuvunja kama hujakaa katka kiti maana unakuwa huna mamlaka.

Isaya 6:1

Watu wengi wanafikiria kwamba Shetani kawapiga bao ktk huduma yao katka utumishi wao, katika kazi zao, ofisi zao etc na hakuna faida wala manufaa kumbe laa,kuna mtu kakaaa katka hicho kiti cha enzi ambacho kinamfanya awe kipofu na haoni kitu cha Mungu kwa sababu hayupo katka kiti. Na huwezi kukaa katka kiti kama hujapigana au kupambana.

Unataka kuona mafanikio katka familia au ofisi au kanisani cheki kile kiti cha hapo mahali na mpe Mungu nafasi.

Asomea na afahamu.

Itaendelea day 2....

Comments

Popular Posts