KUTOA ZAKA KILA UPATAPO KIPATO.

KUTOA ZAKA kila mwezi au kila upatapo kipato.

sadaka+zaka

   mafundisho ya kutoa zaka kila upatapo kipato ni SAHIHI, sio mafundisho potofu hata kidogo. Naomba ninukuu maandiko ambayo tunayafahamu sote kisha nitayafafanua. “Yakobo akaweka nadhiri akisema, Mungu akiwa pamoja nami, akinilinda katika njia niiendeayo, na kunipa chakula nile, na nguo nivae; nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo Bwana atakuwa Mungu wangu. Na jiwe hili nililolisimamisha kama nguzo litakuwa nyumba ya Mungu; na katika kila utakalonipa hakika nitakutolea wewe sehemu ya kumi“. – Mwanzo 28:22. Hebu ongezea na andiko hili “Lakini, ole wenu, Mafarisayo, kwa kuwa mwatoa zaka za mnanaa na mchicha na kila mboga, na huku mwaacha mambo ya adili, na upendo wa Mungu; iliwapasa kuyafanya hayo ya kwanza, bila kuyaacha hayo ya pili”. – LUKA 11:42 (SUV msisitizo added).

Utoaji wa Zaka/Fungu la kumi/Sehemu ya kumi ni jambo lilikuwepo hata kabla na baada ya sheria. Yakobo anasemakatika kila utakalonipa hakika ………. Bwana Yesu anawaambia mafarisayo wasiache kutoa zaka za mnanaa na mchicha na kila mboga. Swali ni kwamba ni wakati gani mboga mboga hizi zinapatikana? Je si wakati wa kuzivuna? Lakini jambo la kuzingatia ni kuwa kila atoae zaka yampasa kuleta ZAKA KAMILI ( Malaki 3:10). Logical thinking rahisi ni zipi, kuleta zaka kamili kwa mtu wa kawaida ambaye uwekaji wa kumbu kumbu sio kivile? Hivi Mungu huagiza wanawe na kisha kuweka ugumu wa kuyatekeleza. ukikaa na zka muda mrefu hakuna uwezekano wa kusahau, na ukisahau itakuwa umetoa zaka kamili? Kwa nini mambo yasiwe rahisi kwa kutoa kila unapopata? Hebu chukulia mfanyakazi akae na zaka kisha baada ya mwaka ndipo atoe, Je, ataweza kutoa mapato ya 120% (yaani 10% mara miezi 12)?

Ninajua tunakubaliana kuwa kutoa Zaka ni wajibu wa kila mwamini. Sasa frequency (mara ngapi kwa kipindi gani) isiwe issue. Huenda mpendwa Milinga unatatizwa na andiko lifuatalo; nanukuu “Usiache kutoa zaka ya fungu la kumi katika maongeo yote ya mbegu zako, yatokayo shamba mwaka baada ya mwaka”.  - KUMB 14:22. Kama ndiyo andiko hili, basi naomba uangalie tafasiri zingine zinasema nini kuhusu maongeo. Hebu angalia ya KJV – neno maongeo limetafsiri ni “increase”, yaani ongezeko. Hawa ndugu zetu walikuwa na aina mbali mbali za Zaka katika kitu kimoja. Wote tunajua kuwa zaka zinatolewa nyumbani mwa Bwana lakini hebu ona hii “Kila mwaka wa tatu, mwisho wake, toa fungu la kumi lote la maongeo yako ya mwaka huo, uliweke ndani ya malango yako;”. – KUMB 14:28(SUV – msisitizo added). Agizo hapa ni kuiweka zaka ndani ya malango yako sio nyumbani mwa Bwana!!!

Pia kuhusu ile zaka ya kila mwaka inawezekana walikuwa wanavuna mara moja kwa mwaka. Ona tafasiri hii  “You shall tithe all the yield of your seed, which comes forth from the field year by year”. – Deut 14: 22 – RSV. Hivyo mavuno ya shamba ni tofauti na mambo ya msharaha au faida katika biashara ambayo mpendwa anapata mapato kila mwezi, wiki n.k. Nimalizie kwa kusema, Zaka ya kila mwaka iliyoonyeshwa hapo juu, ilikuwa inatolewa nyumbani mwa Bwana lakini inaliwa na mtoaji pamoja na mlawi. Swali ni hili Je, Zaka unazotoa huwa unakula mwenyewe? Zaka ya kila baada ya miaka mitatu ilikuwa inatolewa na kuwekwa malangoni ili mlawi, mjane, watima na mgeni wakiiona waweze kuchangamkia (Soma mwenyewe KUMB 14:22-29 uthibitishe).

Ninaona kuwa nimejibu hoja hii na kuthibitisha kuwa kutoa zaka kila unapopata mapato ni mafundisho sahihi na inawezekana pia nimekuongezea na aina nyingine ya Zaka.

Comments

Popular Posts