SOMO: MAHUSIANO YA VITI VYA ENZI NA MAFANIKIO YAKO MSEMAJI: MWL. C. MWAKASEGE Jangwani Dar es salaam 01-08 march 2015 SIKU YA TANO:

SOMO: MAHUSIANO YA VITI VYA ENZI NA MAFANIKIO YAKO

MSEMAJI: MWL. C. MWAKASEGE

Jangwani Dar es salaam
01-08 march 2015

SIKU YA TANO:

Ufunuo 13:2,7
Mathayo 23:1-3

Shetani anawapa watu wake nguvu, kiti cha enzi, na uweza mwingi.
Lengo ni kufanya vita na watakatifu na kuwashinda.

Shetani ameachilia viti vyake katika ngazi mbalimbali kama kanisani, kabila, ukoo, taifa, lugha, nk

Jana nilikuonesha ishara zinazoonesha kwamba vita uliyonayo unapambana na viti vya enzi. Leo tuendelee mbele zaidi:

7. Unapoona ofisi za viongozi wa dini na viongozi wa dola wanapoungana pamoja ili kupinga kile kizuri unachoifanyia jamii
 Matendo 3:
 Matendo 4:

Utaona hapa akina petro wanawekwa gerezani baada ya kumponya kiwete na kuhubiri injili watu kuamini.
Utaona viongozi wa dini na dola kwa pamoja wanawauliza akina petro ni nguvu gani na kwa jina gani mmetenda haya?
Hawana shida na mtu kupona, shida yao ni mamlaka ipi wametumia?

Ukiona hivyo ujue hiyo vita inatoka kwenye kiti cha cha enzi kilichowekwa na shetani.


8. Unapoona kiti kishindwacho katika vita ya viti vya enzi katika ulimwengu wa roho watu wake wanakuwa na hasira isiyo ya kibinadamu na haina maelezo kiutu.
 Ufunuo 16:10,11

Tunaona malaika anapeleka adhabu kwenye kiti, na ufalme wote unatiwa giza na watu waliotumika katika hicho kiti wanapata maumivu, na hasira.
 Pia wanatukana. Ukiona hivyo ujue hiyo vita ilikuwa ni ya viti.

Mfano: mkoa mmoja pepo mmoja lilikutana na nguvu za Mungu likaanza kuachilia matusi, tukajua kwamba kiti chao kimepigwa na kiti tulichokalia katika Yesu.

9. Kuoteshwa ndoto au kuoneshwa maono yanayozungumzia juu ya kiti cha enzi na mafanikio yako
 Daniel 4:1-15
 Daniel 5:17-21
 Nebukdreza aliota ndoto
Ayubu 29:7,19,25
Mara ingine utaona kiti au kisiki katika ndoto. Utajua kwamba hiyo vita uliyonayo inatoka katika viti vya enzi.
Soma hiyo mistari ya ayubu utaelewa vizuri

10. Kuwekewa vikwazo kikazi vinavyokulenga wewe bila kuonesha wazi kwamba vinakulenga wewe ili tu uache kazi
 Daniel 6:1-17
Hapa watakupambanishi na kiti kilichokupa kiti.
Haleluya! Unasema mwakasege unaongea kiti gani? Soma biblia yako.

11. Tazama mazingira ambayo Mungu amekupa uishi na utumie kupata kipato, kuna nini?

Penye utawala wa kiti huwa kuna alama ya kiti.
Waamuzi 6:25,26,28,30

Kulikuwa na madhabahu na ashera. Gideoni aliharibu madhabahu na kuikata ashera. Alipofanya hivyo watu wa mji walichukia kwa sababu ile viti ilikuwa ni ya viti.

Madhabahu peke yake bila kiti haina mamlaka ya kutawala kisheria

Madhabahu inatumia kiti kutawala

Kiti kinatumia nguvu za madhabahu kutawala

Madhabahu na kiti vinatakiwa kufanya kazi pamoja.
Unaweza kubaki na madhabahu na kiti umekabidhi kwa Mungu mwingine.

Mfano:
Nilienda nchi mmoja ulaya. Nilipata nafasi ya kutembelea kanisa fulani. Kwenye eneo la kanisa nikakuta mti umesimamishwa na juu umewekwa vitu kama masikio. Wenyeji waliniambia wao wanatoa msaada kwa wahindi wekundu, kwa hiyo hao wahindi wakawapa zawadi ya Mungu wao kama shukrani ya misaada wanayopokea.

Unaona wana madhabahu, lakini kiti wamekabidhi kwa Mungu mwingine. Angalia kiroho chao kilianza kuharibika.

Vita ya viti ni ngumu sana. Kuna mtu mmoja Ethiopia aliona watu wakiabudu kwenye mti siku nyingi, alivyoonakufariki hvyo alichukua shoka kwenda kukata. Mti ulivyoanguka naye akaanguka na  hapohapo.
Kwanini? Yeye alienda na shoka kumbe wao wameenda na  viti.

Ooh! Hii ni siri ya ajabu unahitaji kufahamu. Nilikwambia sikutaka kufundisha hili somo, lakini Mungu akanibana nifundishe.
Masomo kama saa ingine hatufundishi watu wote, unachukua wachache unasema nao. Maana ni mazito

Lakini ukiona Mungu ameachilia wazi namna hii ujue kuna mahali anatupeleka ni kuzuri sana.

Kesho nitakufundisha namna ya kuangalia kama umekaa kwenye kiti au hujakaa.

Itaendelea.

Comments

Popular Posts