.JIFUNZE NAMNA YA KUJISAIDIA MWENYEWE
Jitambue
Ya Chris Mauki.....JIFUNZE NAMNA YA KUJISAIDIA MWENYEWE (Self Help Skills)
Utafiti
uliofanywa katika maeneo mengi katika nchi zilizo endelea na zinazoendelea
unaonyesha kuwa watu wengi bado wanahitaji kiwango kikubwa cha uwezo wa
kujisaidia wenyewe. Hata katika nchi kama marekani ambayo teknolojia ni
kubwa lakini watu pia wanakiu kubwa ya jinsi ya kujua kujisaidia wenyewe
katika baadhi ya mambo yanayowasibu kimwili, kihisia na maisha kwa ujumla
Wachunguzi
wakubwa wa maswala ya kisaikolijia Richard na Tony Robbins wanaafiki kwamba
yawezekana kabisa tukarekebisha na kuweka sawa vile visivyokaa sawa katika
miili yetu au akili zetu pasipo kutegemea msaada wa daktari au mshauri.
Watu wengi
ulimwenguni wanapata msada wa ujuzi huu kupitia kuenea kwa mtandao wa intanet
na vitabu vya ujuzi huu vilivyo vingi sana (self help books).
Takwimu
zinaonyesha wamarekani walitumia zaidi ya dola 563 milioni kwa manunuzi ya
vitabu vya ujuzi wa kujisaidia mwenyewe, na pia zaidi ya tovuti 12000 za
masuala ya afya ya akili “mental health” hutumika nchini marekani. Yote
hii ni watu kutafuta uwezo wa kujisaidia zaidi ya kutegemea kusaidiwa
hasa katika mambo ya afya ya akili, hisia ,nk. Zaidi ya 40% ya tovuti za
masuala ya afya kutumiwa na watu hasa katika kutafuta kufahamu juu ya tatizo
la kupoaaza moyo na upweke (depression).
Huu ni
wakati wa kila mmoja kujua jinsi ya kurekebisha maumivu yake na kuponya
majeraha yake mwenyewe. Hii inawezekana.
Habari au
taarifa nyingi za namna ya kujisaidia binafsi zimekuwa zikikosewa na
kutafsiriwa tofauti mara nyingi. Hii ndio maana wengi wamekuwa
hawatilii maanani na pia wengi kutopata matokeo halisi yanayotarajiwa.
Safu ya gazeti hili leo inakwenda kukufungua na kukusaidia.
Yafuatayo
ni baadhi ya maeneo katika maisha yetu ya kila siku ambayo huleta matatizo
kwa kushindwa kuwa na ujuzi wa kujisaidia wenyewe.
1.Unapokuwa
Katika Hasira Kali.
Kama vile
yalivyomatundu katika kuta kubwa kwa ajili ya kupumulia hewa na kupunguza
presha katika ukuta huo ili usije pata nyufa (ventilations)
ndivyo hivyo mtu mwenyehasira kali hutakiwa kujua jinsi ya kuyaruhusu
mazingira aliyopo yaweze kumsaidia kuipumulia nje ile hasira pasipo kuleta
madhara kwake yeye na wale wanaomzunguka ( venting anger )
Tumeona
sana katika filamu au vitabu vya asili ya nchi za magharibi wengi
wakiwa katika hali hii hukumbatia au kung’ata au kupiga ngumi mito ya kulalia
(pillow) au wengine hutupa ngumi katika mfuko wa mazoezi ya kupigana (punching
bag) katika hali hii hasira kali hupata pakupenyezea na kupoa. Watalaam
wameshauri kutumia nguvu zote kutupa ngumi au kupiga mito hii au puching bag
na kama ni mtu amekuudhi basi fikiria kuwa unauona uso wake katika mto huo na
uiachie hasira yako kimwili (kwa kupiga) na kimaneno kwa kuongea yale
yote yaliyo moyoni mwako. Watafiti wanasema aina hii yaweza pia kuwa msaada
kwa kupunguza msongo wa mawazao mbali na hasira.
Tafiti za
hivi karibuni zimeonyesha mtazamo wa tofauti kidogo katika hili. Dr
Brad Bushman mwanasaikolojia wa Iowa state university anasema
watu wengi hufikiri kwa kufanya hivi wanafanikiwa kupona hasira ila wale
wachache ambao inashindikana wanakuwa na hasira kali maradufu na
kuchanganyikiwa.
Baadhi ya
tafiti zimeonyesha kuwa kukosewa kwa namna ya kuipunguza au kuitoa hasira
kumewasababishia wengi matatizo ya misuli ya kichwani na hivyo kuhatarisha
akili zao.
Nini
Kifanyike Basi
i)
Jaribu kufanya chochote kile ambacho chaweza kikachukua nafasi ya hasira
moyoni, kila mtu anakitu anachokipenda, kifanye hicho sasa, kwa mfano;
kuangalia filamu, picha, kusoma au kusikiliza hadithi au kusikiliza nyimbo
unazozipenda, jihadhari kukaa karibu na yule aliyekukwaza mpaka mmesuluhisha
yaliyowasibu.
ii)
Pata muda wa kucheka na marafiki wengine, kama ni baba pata muda wakutoka
na watoto wako, hawa wananafasi kubwa ya kukuingia moyoni kwa haraka na
kusafisha hasira uliyonayo.
iii)
Usikimbilie sana kwenye mazoezi ya viuongo kwasababu utafiti wa Dr. Bushman
unaonyesha kuwa mazoezi ya viungo yananafasi kubwa ya kuiamsha hasira, wengi
waliotafitiwa walienda kupigana mara tu baada ya kumaliza mazoezi ya viungo.
iv)
Michezo ya kijadi kama vile tai, chi, na yoga yaweza kuwa msaada wa
kurekebisha hisia na hali ya akili, ni vema ukafanya michezo hii kama
unaujuzi nayo na kama inaruhusiwa na imani yako, kwa sababu mingi iko zaidi
katika imani za dini za nchi za bara Asia.
v)
Muendelezo wa kufanya kazi au shughuli itakayochukua muda mrefu wa
kufikiri na kuifanya bize akili yako inaweza kupooza hasira pia.
2.
Unapokuwa Umefadhaika, Umepooza, Unahuzuni na Kuvunjika
Moyo
Tafuta
sana kufikiria yale yaliyo mema na ya kukutia moyo. Peleka moyo wako
katika yale yanayokupa furaha zaidi kuliko katika yale yanayovunja furaha
yako. Funga milango yako ya akili, usiruhusu chochote kisicho cha furaha
kuingia ndani. Tumia ubongo wako kufikiri kuwa yote yanawezekana
(optimistic
thinking).
Teka uwezo
wa akili na fikra zako na uzielekeze kule tu unakopenda wewe,
usiruhusu
kamwe watu au mazingira yakuletee picha inayokuumiza moyo
Tafiti
zinaonyesha kuwa mara nyingi tunapokuwa katika huzuni na kuvunjika moyo kila
kitu huonekana kinyume nasi. Nguvu ya ubongo nayo inashindwa
kuyadidimiza yale yaliyo mabaya ili tusiyawaze. Na kila tunapojaribu
kujitahidi wenyewe kuikataa hali hii mawazo na mitazamo ya kufeli na
kushindwa hujaza fikra zetu. Mara unapojaribu kufikiri yale mema moto
huwa mkali zaidi na kuona kuwa wewe ni wakushindwa zaidi.
Ufanye
nini Basi?
i)
Pata muda zungumza na marafiki, watu wa dini (wachungaji, mapadri,
shekhe, washauri au yeyote anayeweza kukupa mitazamo ya tofauti na
kukuwezesha kuwaza mambo mengine.
ii)
Nenda katika maeneo ambayo watu wanafurahi, kama vile sherehe, ufukweni,
hotelini, super market au katika maduka makubwa, taratibu utaona roho
na nafsi yako vinanyanyuka upya.
iii)
Na kama unajua kuwa kunakitu kitakuudhi na kuharibu furaha yako panga
vitu vingi vilivyo vyema na vyakukujenga utumie muda kuviwaza hivyo.
3.
Unapojihisi Kupoteza Mwelekeo wa Maisha
Kumbuka na
uyafikirie tena na tena malengo yako, hii itakuwezesha kuyafanya yawe kweli.
Pata mawazo na picha ya wewe ukifanikiwa na sio ukishindwa, iache picha hiyo
ikae katika akili yako, itakusaidia kuyafanya matendo yako yapiganie uhalisi
wa kile kilichopo akilini mwako.
Kuwaza tu
kuwa unafanikiwa hakutoshi, hapa ninazungumza pia na wale wenye imani zao
kali za dini ambao hukesha wakiamini wanafanikiwa na wamekwisha fanikiwa na
wakati hakuna wanachokifanya, lazima ufanye mabadiliko yakimtazamo lasivyo
kifo kitakukuta hapo hapo ukiwaza unafanikiwa wakati watu wanakuona wewe kama
mfano mzuri wa walioshindwa maisha. Lazima picha ulionayo ya kufanikiwa
itiwenguvu na matendo(actions) ya kila siku katika kuifanya ndoto yako kuwa
halisi “to make your dream come true”
Shelley
Taylor, Daktari wa saikolojia wa chuo kikuu cha UCLA Marekani ameonyesha kuwa
katika kufikiria tu kuwa unafanikiwa na kuliwekea picha lengo lako
katika akili bila matendo ina athari mbili; Kwanza inalitenganisha lile lengo
mbali na kile kinachohitajika kufanywa ili lengo lifikiwe, na pili inakufanya
ufurahie utamu wa kuwa mtu aliyefanikiwa wakati bado kabisa hujafika
popote, hali hizi zinafifisha nguvu ya lengo lako (power of the goal)
na kukufanya kushindwa kujitahidi kufanya kazi na kukubali kupoteza (to take
risks) katika kukipata kile ambacho kiko katika ndoto zako za kila siku.
Nini
kifanyike?
i)
Pamoja na kuwaza kila siku na kuwa na ndoto za mafanikio, pata wakati
jiulize ninini unaweza kufanya ili kufikia mafanikio hayo, na ukipata njia au
mbinu hizi anzia kuzifanyia mazoezi akilini kabla ya kuziweka katika
uhalisia.
ii)
Kwa malengo ya muda mfupi waweza kupitia hatua zote ulizo zipanga ndani
ya siku moja kabla ya kuanza kuzitendea kazi. Lakini kwa malengo
makubwa na yamuda mrefu unaweza kupitia mipango yako tena na tena kadri
unavyozidi kuendelea na mchakato mzima na uone kama kunahitajika
marekebisho.
4.
Unapokuwa na hali ya Kutojithamini na Kutojipenda (Low Self Esteem)
Jitambue
ya kuwa wewe ni wathamani na ni mtubora zaidi. Hii itakuwezesha
kujithamini na kujipenda. Jifunze kuandika maneno ya ushindi yanayoonyesha
ujasiri na ukakamavu (affirmation) kwa mfano viko vikaratasi vidogo vya
kunatisha (stickers) katika kuta au katika magari vinamaneno “every thing is
possible” vikimaanisha kila kitu kinawezekana. Nyingine zimeandikwa “I
can do it’ (ninaweza), nakumbuka nimeona katika gari la rafiki yangu
kikaratasi cheye maneno ya dini “nayaweza yote katika yeye anitiaye
nguvu” maneno haya na mengine mengi yawe ya dini au yakutungwa au waweza
kuandika mwenyewe na kubandika katika ukuta wako, kioo cha kujitazama, katika
mlango wa friji yako, ndani ya gari lako, pembeni ya kitanda au bafuni.
Kwa teknolojia ya sasa unaweza kuyarekodi maneno haya na yakasema katika
redioyako mara kwa mara au kuyaandika katika compyuta yako yakawekwa
kama “screen saver” ili mradi tu kila unapogeuka unayaona yanasema na
wewe. Maneno haya yana nguvu ya kupenyeza ujumbe ndani ya fikra na moyo
wako na kuruhusu mwili wako kudaka na kuyatendea kazi.
William
Swann, daktari wa chuoo kikuu cha Texas anasema mtazamo huu unaweza kuwa
mgumu kidogo na sio wote wanaweza kufanikiwa katika hili kwasababu kubadili
jinsi tunavyojihisi wenyewe ni kazi ngumu sana.
Hali ya
kujithamini na kujipenda inategemea mambo mawili; Kwanza hisia zetu za jinsi
gani tunavyojipenda, na pili hisia zetu za uwezo gani tulionao katika kazi
zetu na shuhuli nyingine zinazohitaji ujuzi na vipawa vyetu. Katika hili
matumizi ya maandishi yanayoonyesha ushindi na kuweza (affirmations)
yaweza kufanikiwa kwa baadhi ya watu lakini pale yanaposhidwa kufanya kazi
huweza kumuacha mtu akiwa ameumia moyo zaidi.
Mara
nyingi wale wenyemitazamo mibovu kuhusu wao wenyewe hawajiamini na hawaamini
kama waweza kusema au kufanya kitu bora hata siku moja kwa jinsi hii
hata kama wakiandika vimaneno vingi vilivyo vya kutia moyo bado hawatakuwa na
imani maana wanachokijua wao ni kwamba kamwe hakuna chema kitakachoweza
kutoka kwao. “Nothing good shall ever come from them”
Nini
kifanyike basi?
i)
Njia pekee ya kubadilisha matunda ya vile tunavyojihisi au tunavyojithamini
ni kubadili vile vinavyotuingia na kutengeneza ile hali ya jinsi
tunavyojiona. Kwamfano; kama unajikuta unashindwa kujithamini au kujipenda
sababu ya wale unaohusiana nao au unaokuwa nao zaidi, basi
badilisha,chagua watu wengine wakuhusiana nao, labda hao watasema yaliyobora
kuhusu wewe na kukutia moyo zaidi. Kama uko katika ajira ambayo kila
mtu anakuona wewe hujui na wewe niwakushindwa tu, amua kuwataka wabadili
mtazamo wao kwako au ikibidi ondoka pata kazi sehemu ambayo watu
wanamtazamo mzuri kwako. Jaribu kufanya kazi yako vema zaidi ya
ulivyoifanya kule kwa awali.
ii)
Simama ujitetee mwenyewe usingoje
kutetewa “stand for yourself”
hakikisha
unazungukwa na watu wanaokuona kuwa wewe ni wathamani, unayeweza, na ni mtu
mwema. Hakikisha wanalikiri hilo kwa vinywa vyao.Uwe mvumilivu na wakati wote
jitahidi kutimiza majukumu yako ili usiwavunje moyo wale wanokuona wewe kuwa
mtu mwema na wanayekuamini. Fahamu kuwa jinsi tunavyojiona sisi wenyewe, na
mtazamo tulionao kuhusu sisi wenyewe (self esteem) ni mjumuisho wa jinsi
tunavyohusiana na watu wanaotuzunguka kwa muda tuishio hapa duniani na
kwamwe hauwezi kubadilika kwa usiku mmoja.
5.
Unatatizo la Mawasiliano Katika Mahusiano Uliyonayo:
Usikivu
makini (active listening) unaweza kukusaidia kuwasiliana vema na rafiki yako
au mpenzi wako. Katika usikivu makini tunamaanisha sio tu kusikia, bali
kuelewa kwa uhakika kile mwenzako anachojaribu kukisema. Hapa ndipo
tofauti kati ya neno “hearing” na neno “listening” inapojidhihirisha na hata
maneno kusikia na kusikiliza yanapoonyesha tofauti. Katika mahusiano
baina ya watu, marafiki, wapenzi, ni lazima kuwepo na kusikilizana “listening”
na sio “kusikiana”
Mahusiano mengi na hata ndoa nyingi zimekuwa na migogoro na hata
mivunjiko maana kumekuwa na kusikiana zaidi ya kusikilizana kamwe msisahau
kuwa tunayasikia magari, tunasikia ndege wa angani na ndege za abiria,
tunasikia upepo na miti na makelele mengine lakini tunawa sikiliza watu
na yale wanayoyasema.
Tunasikiliza
kile tunachoelezwa kwa kukitathmini kama vile kilivyosemwa na tunakirudia kwa
maneno yetu wenyewe tukijaribu kifikiri kile mwenzetu anachojaribu kutuambia.
Katika hili tunatambua yakwamba kusikiliza ni mchakato (process) wakati sio
hivyo katika kusikia. Baadhi ya wachunguzi wamegundua kwamba usikivu makini
au masikilizano, yanawasaidia zaidi wale walioko katika mahusiano mazuri,
lakini maranyingi mchakato mzima wa kusikilizana hukwama hasa pale wapenzi
wanapokuwa katika ugomvi au mahojiano makali, hapa kusikilizana huwa ni
ndoto.
Zingatia
haya!
Walioko
katika mahusiano (wanandoa) wajaribu kupeleka jitihada zao zote katika
mambo matatu muhimu
i)
wanawake wajitahidi kuwasilisha hoja na madai yao katika hali ya upole na
upendo. Tafiti zinaonyesha kuwa wanaume wengi wamekuwa tayari kusikiliza toka
kwa wanawake pale ambapo
wanaongeleshwa kwa utulivu na unyenyekevu.
ii)
Wanaume wanahitaji kuwasikiliza wenza wao kiufasaha na kuzingatia juu ya
hisia na mawazo yao.
iii)
Pande zote mbili yaani wanaume na wanawake jitahidini kwa kila hali
kuutuliza utu wa kiume na kuutiisha. Kiasili wanaume wanatabia ya kuhemka
nakuwaka hisia zao za hasira haraka hasa wanapogadhibishwa, na kwa hali hii
hujitahidi kujitoa kwenye tatizo haraka ili waziponye nafsi zao hatakama
ufumbuzi wa tatizo haujapatikana na hii hufanya matatizo mengi katika
mahusiano kuachwa bila suluhisho “unsolved Conflicts” na hali hii pia
huwaacha wanawake katika hasira na maumivu makali.
Jitahidini
kuhakikisha hamfikii katika hali hii kwa kurushiana utani kidogo au mwanamke
kumkumbatia mwanaume angalau kupunguza gadhabu yake na mara mtajikuta
mnaishia pazuri.
|
|
ujumbe huu umeandikwa na kaka Chris Mauki. |
Comments
Post a Comment