Maswali ya Ndoa na majibu yake Kibibli



Maswali ya Ndoa na majibu yake Kibiblia

swali: “Je, tunapaswa kikamilifu kutafuta kwa mchumba, au kumsubiri Mungu kuleta mchumbae kwetu?”
Jibu: Jibu kwa maswali yote ni “naam.” Kuna uwiano muhimu kati ya hizo mbili. Hatupaswi kutafuta mchumba kana kwamba inategemea tu juhudi zetu wenyewe. Wala hatupaswi kuwa watazamaji tu, kufikiri kuwa Mungu siku moja atamfanya mke kufika katika mlango wetu. Kama Wakristo, katika wakati Fulani ikiwa tumeamua kwamba tunamtafuta mchumba, tunapaswa kuanza mchakato na maombi. tukijuwazilisha wenyewe kwa mapenzi ya Mungu katika maisha yetu ni hatua ya kwanza. “Nawe utajifurahisha kwa Bwana naye atakupa haja za moyo wako” (Zaburi 37:4). Kujifurahisha katika Bwana ina maana sisi kupata radhi katika kumjua Yeye na kuamini kwamba yeye pia atatufuraha. Yeye ataweka matamanio yake ndani ya mioyo yetu, na katika mazingira ya kutafuta mchumba, kumaanisha tunajitamani mchumba Yeye anatamani tupatemwenye anajua atatuletea furaha. Mithali 3:6 inatuambia, “Katika njia zako zote mkiri yeye, naye atayanyosha mapito yako.” Kumtambua Yeye katika kutafuta mchumba inamaanisha kujiwasilisha kwa mapenzi yake tawala na kumwambia kuwa chochote Yeye ataamua ni bora ndicho utataka.
Baada ya kujitoa sisi wenyewe kwa mapenzi ya Mungu, tunapaswa kuwa wazi juu ya tabia ya mume mcha Mungu au mke na tutafute mchumba ambaye amehitimu ngazi ya kiroho. Ni muhimu kuwa na uelewa wa wazi wa sifa hizi kwanza na kisha kutafuta mtu ambaye ako nazo. “Kuingia katika mapenzi” na mtu na kisha kugundua yeye hana sifa za kiroho kumwezesha kuwa mchumba wetu ni kukaribisha maumivu ya moyo na kujiweka katika nafasi ngumu sana.
Tunapoielewa Bibilia na kufahamu kile tunachotakiwa kukitafuta kulingana na maandiko, tutafahamu vyema cha kukitafuta kwa mchumba na kuelewa kwamba Mungu atamleta yeye katika maisha yetu kwa wakati wake mtimilifu na kulingana na mapenzi yake. Tunapoomba, Mungu atatuongoza kwa yule anayetufaa. Ikiwa tutasubiri wakati wake mtimilifu, tutampokea anayetufaa kwa mienendo, matamanio yetu na hata atakayetufaa kiasili. Tunafaa (methali 3:5), hata wakati majira yake si majira yetu. Wakati mwingine Mungu anawaita watu wasioe kwa vyovyote vile (1 Wakorintho 7), lakini katika hali hizo, yeye anaweka wazi kwa kuondoa hamu ya ndoa. Muda wa Mungu ndio kamili, na kwa imani na uvumilivu, sisi hupokea ahadi zake (Waebrania 6:12).
Maana ya Ndoa.
Je! Bibilia ya funza nini kuhusu ndoa?. Imeandikwa, Mathayo 19:5-6 “Asema kwasabu hiyo mtu atamwacha babaye na mamaye ataambatana na mkewe na hao wawili watakua mwili mmoja? hata wamekua si wawili tena bali mwili mmoja basi aliowaunganisha Mungu mwanadamu asiwatenganishe.”
Je! waume wawatendeaje wake zao?. Imeandikwa, Waefeso 5:25-28 “Enyi waume wapendeni wake zenu kama Kristo naye alivyolipenda kanisa, akajitoa kwa ajili yake ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno apate kujiletea kanisa tukufu, lisilo na ila wal kunyazi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa. Vivyo hivyo imewapasa waume na kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe mewenyewe.”
Waume wa waheshimu wake zao. Imeandikwa, 1Petro 3:7 “Kadhalika ninyi waume kaeni na wake zenu kwa akili na kupa mke heshima kama chombo kisicho na nguvu, na kama waridhi pamoja wa neema ya uzima kusudi kuomba kwenu kusizuiliwe.”
Je wake nao wake na waume zao vipi?. Imeandikwa, Waefeso 5:22-24 “Enyi wake watiini waume zenu kama kutii Bwana wetu kwa maana mume ni kishwa cha mkewe kama Kristo naye nikichwa cha kanisa, naye nimwokozi wa mwili. Lakini kama vile kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.”
Je inamaanisha ya kuwa wake wafanye kila jambo? Asha!. Imeandikwa, Waefeso 5:21 “Hali mnanyenyekea katika kicho cha Kristo.”
Je tumeagizwa kutoa kupigana kwa mke na mme. Imeandikwa, Wakolosai 3:19 “Ninyi waume, wapendeni waume zenu, msiwe na uchungu nao.”
Kuwa na ndoa njema nivema kutatua mafaragano au kutoelewana mara moja. Imeandikwa, Waefeso 4:26 “Mwea na hasira ila msitende dhambi; jua lisichwe na uchungu wenu bado haujawatoka.”
Fanya ndao yako ikuwe kwa umoja na kuelewana. Imeandikwa, Waefeso 4:2-3 “Kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendo na kujitahidi kuuhifadhi umoja kwa Roho katika kifungo cha amani.”
Je! watu wapaswa kuiona vipi ndoa. Imeandikwa, Waebrania 13:4 “Ndoa na iheshimiwe na watu wote na malazi yawe safi kwa maana washerati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.”
Kwa amri gani Mungu ameilinda ndoa. Imeandikwa, Kutoka 20:14, 17 “Usizini”. Usitamani nyumba ya jirani yako usitamani nyumba ya jirani yako…”
Je Mungu ameamua kuvunja ndoa katika hali gani? Imeandikwa, Mathayo 5:32 “Lakini mimi nawaambia, kila mtu amwachaye mkewe isipokua kwa habari ya uasherati amefanya kuwa mzinzi, na mtu akimwoa yule aliyeachwa azini.”
Je ndoa ikae kwa mda gani. Imeandkwa, Warumi 7:2 “Kwa maana mwanamke aliye na mume amefungwa na sheria kwa yule mume wakati anapokua hai, bali akifa yule mume amefunguliwa ilesheria ya mume.”
Je tumeagizwa kumuoa nani? Imeandikwa 2Wakorintho 6:14 “Msifungwe nira pamoja na wasioamini kwa jinsi isivyo sawasawa kwa maana kuna urafiki gani kati ya haki na uasi? tena pana shirika gani kati ya nuru na giza?.”
Malazi yamebarikiwa na Mungu wakatika ndoa. Imeandikwa, Mithali 5:18-19 “Chemchemi yako ibarikiwe nawe umfurahiye mke waujana wako ni alaya apendaye na paa apendezaye.”
Kutokuoa
Kuolewa na kutoolewa ni baraka kutoka kwa Mungu. Imeandikwa, 1Wakorintho 7:6-7 “Lakini nasema hayo kwa kutoa idhini yangu si kwa amri ila nipendalo ni kwamba watu wote wawe kama mimi nilivyo walakini kila mtu ana karama yake itokayo kwa Mungu, huyu hivi, na huyu hivi.”
Wakati mwema wa kukaa bila kuoa ni kuweza kuwa na mda wa kumtumikia Mungu. Imeandikwa, 1Wakorintho 7:29-31 “Lakini ndungu nasema hivi muda ubakio si mwingi basi tokea sasa wale walio na wake na wawe kama hawana na wale waliao kama hawalii na wale wafurahio kama hawafurahi na wale wanunuao kama hawana kitu na wale wautumiao ulimwengu huu kama hawautumii sana kwa maana mambo ya ulimwengu huu yatapita.”
Kutongoza na kuonana kimwili
Yanayo tupasa kufanya wakati wa kutongozana. Imeandikwa, Warumi 13:13 “Kama ilivyohusika na mchana na tuenende kwa adabu si kwa ulafi na ulevi si kwa ufisadi na uasherati, si kwa ugomvi na wivu.”
Tunapo tongozana, tusije tuka onana kimwili. Imeandikwa, 1Wakorintho 6:13, 18, “Vyakula ni vya tumbo, na tumbo ni kwa vyakula lakini Mungu atavitowesha vyote viwili tumbo na vyakula lakini mwili si kwa zinaa…(18) bali kwa Bwana naye Bwana ni kwa mwili. Ikimbieni zinaa, kila dhambi aitendayo mwanadamu ni inje ya mwili wake ila yeye afanyaye zinaa hufanya juu ya mwili wake mwenyewe.”
Jeweke safi. Imeandikwa, 1Yohana 3:3 “Na kila mwenye matumaini haya, katika yeye hujitakasa kaa yeye alivyo mtakatifu.”
Tusije tukaumia sharti weka tamaa ya zinaa mbele za Bwana. Imeandikwa, 1 Wathesalonike 4:3-5 “Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu kutakaswa kwenu muepukane na uasherati kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima. Sikatika hali ya tama mbaya kama mataifa wasio mjua Mungu.”
Je kama umekwisha zini ufanye je? Kwanaza kubali kuwa umefanya dhambi. Imeandikwa, Zaburi 51:2-4 “Unioshe kabisa na uovu wangu unitakase dhambi zangu maana niejua mimi makosa yangu na dhambi yangu imbele zangu daima. Nime kutenda dhambi wewe peke yako na kufanya maovu mbele za macho yako wewe ujulikane kuwa una haki unenapo. na kuwa safi utoapo hukumu.”
Pili omba msamaha wa dhambi zako. Imeandikwa, Zaburi 51:7-12 “Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi unioshe nami nitakuwa mweupe kuliko theluji unifanye kusikia furaha na shangwe mifupa ulioiponda ifurahi usitiri uso wako uzitazame dhambi zangu uzifute hatia zangu zote Ee Mungu uniumbie moyo safi uifanye upia roho iliyotulia ndani yangu, usinitenge na uso wako wala roho yako mtakatifu usiniondolee unirudishie furaha ya wokovu wako unitegemeze kwa roho ya wepesi.”
Latatu, Amini kuwa Mungu amekusamehe dhambi zako. Imeandikwa, Zaburi 32:1-6 “Heri aliye samehewa dhambi na kusitiri makosa yake, Heri Bwana asiyemhesabia upotovu. Ambaye mwoyoni mwake hamna hila niliponyamaza mifupa yangu ilichakaa kwa kuugua kwangu mchana kutwa kwa maana mchana na usiku mkono wako ulinilemea jasho langu likakauka hata nikawakama nchi kavu wakati wa kaskazi Nalikujulisha dhambi zangu wala sikukufisha upotovu wangu nalisema nitayari maasi yangu kwa Bwana nawe ukanisamehe upotovu wa dhambi yangu kwa hiyo kila mtu mtauwa akuombe wakati unapopatikana hakika maji makuu ya furikapo hayata mfikie yeye.”
Ngono
Hali ya kuonana kimwili ni zawadi kutoka kwa Mungu inapofanywa katika ndoa kwa raha zao. Imeandikwa, Mithali 5:18-19 “Chemchemi yako ibarikiwe nawe umfurahiye mke wa ujana wako ni ayala apendaye na paa apendezaye maziwa yake yakutoshe sikuzote na kwa upendo wake ushangilie daima.”
Kufuraiana na kuonana kimwili ni jambo la kutiliwa maanani katika ndoa. Imeandikwa, Waebrania 13:4 “Ndoa na iheshimiwe na watu wote na malazi yawe safi kwamaana washerati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu.” 1Wakorintho 7:3, 4 Yasema “Mume ape mke wake haki yake na vivyo hivyo mke na ampe mumewe haki yake mke hana amri juu ya mwili wake bali mumewe vivyo hivyo mume hana amri juu ya mwili wake bali mkewe.”
Mungu aliumba hali ya kuonana kimwili kuwa uhusiano katika ya mke na mume katika ndoa. Imeandikwa, 1Wakorintho 7:5 “Msinyimane isipokuwa mmepatana kwa muda ili mpate faragha kwa kusali mkajiane tena shetani asije akawajaribu kwa kutokuwa na kiasi kwenu.”
Tusije tukajikwaa nivema tuweke mahitaji ya. zinaa katika uwezo wa Mungu. Imeandikwa, 1Wathesalonike 4:3-5 “Maana haya ndiyo mapezi ya Mungu kutakazwa kwenu muepukane na uasherati kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima si katika hyali ya tamaa mabaya kama mataifa wasiomjua Mungu.”
Amri ya saba ya onnya kuzini. Imeandikwa, Kutoka 20:14 “Usizini”.
Zinaa ni kubaya ikifanywa nje ya ndoa, ijapokuwa hatuwezi kuona matokeo yake hapo kwa hapo. Ieandikwa, 1wakorintho 6:18 “Ikimbie zinaa kila dhambi aitendayo mwanadamu ni aya nje ya mwili wake ila afanyaye zinaa hutenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe.”
Dhambi ya zinaa ya anzaa vipi?. Imeandikwa, Mathayo 5:28 “Lakini mimi nawaambia kila mtu atazamaye mwanake kwa kutamani amekwisha kuzini naye moyoni mwake.”
Bibilia ya onya zinaa kati ya mwanamume na mwanamume au mwanamke na mwanmke. Imeandikwa, Warumi 1:26-27 “Hivyo Mungu aliwaasha wafuate tama zao zaa aibu hataa wanawake wakabadili matumizi yasiyo ya asili wanaume nao vivyo hivyo waliasha matumizi ya mke ya asili wakawakiana tamaa wanaue wakiyatenda yasiyo wapasa wakapata nafsini mwao malipo ya upotevu wao yaliyo haki yao.”
Bibilia yaonya zinaa kati ya ndugu na dada. Imeandikwa, Mambo ya walawi 18:6 “Mtu ye yote aliye wakwenu asimkaribie mweziwe aliye wa jamaa yake ya karibu ili kumfunua atupu mimi ndimi Bwana.”
Bibilia yaonya zinaa na wanyama. Imeandikwa, Mambo ya walawi 18:23 “Wala usilale na mnyama ye yote ili kujitia unajisi kwake wala mwanamke asisimame mbele ya mnyama ili kulala naye ni uchafuko.”
Bibilia ya onya kufanya mapenzi na kahaba. Imeandikwa, 1Wakorintho 6:15-17 “Je hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? na kuvifanya viungo vya kahaba? hasha au hamjui yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili moja naye lakini yeye aliye ungwa na Bwana ni roho moja naye.”

Swali: “Bibilia inasema nini kuhusu uchumba?”
Jibu: Ingawa neno “uchumba” halipatikani katika Bibilia, tumepewa kanuni kwamba Wakristo wanastahili kupitia kabla ya ndoa. Kanuni ya kwanza ni kwamba ni lazima tutafautishe mtazamo wa dunia kuhusu uchumba kwa sababu mtazamo wa Mungu wahitilafiana na ule wa dunia (2 Petero 2:20). Huku ikiwa mtazamo wa dunia juu ya uchumba huenda usiwe na jinsi tunavyo taka, cha muimu ni kutambua tabia ya mtu kabla tufanye ahadi naye. Lazima tujue ikiwa huyu mtu ameokoka katika roho wa kristo (Yohana 3:3-8) na kama huyo mtu ako na nia ile kama ya kristo (Wafilipi 2:5). Lengo kuu la uchumba ni kumtafuta mpenzi wa maisha. Bibilia inatuambia kwamba, kama Wakristo tusioe wasio Wakristo (2 Wakorintho 6:14-15) kwa sababu hii itafanya uhusiano wetu na Kristo na tuaibishe tabia zetu na kanuni zetu ziwe hafifu.
Wakati mtu amejitoa kw uhusiano, hata kama ni wa uchumba, ni muimu kukumbuka kumpenda Mungu kuliko vitu vyote (Mathayo 10:37). Kusema au kuamini kuwa mtu mwingine ni “vitu vyote” au kitu cha maana katika maisha ni kuabudu sanamu, ambayo ni dhambi (Wagalatia 5:20; Wakolosai 3:5). Pia hatustahili kuichafua miili yetu kwa kufanya usherati (1 Wakorontho 6:9, 13; 2 Timotheo 2:22). Dhambi ya usherati sio dhambi kwa mwili pekee bali ni kinyume na Mungu (1 Wakorintho 6:18). Ni muimu kuwaeshimu na kuwachukulia kuwa watu wa heshima vile tunavyojipenda wenyewe (Warumi 12:9-10). Na hii ni kweli kwa uhusiano wa uchumba. Hata kama mnachumbiana, kuifuata kanuni hii ndio njia nzuri kuwa na msingi salama wa ndoa. Mojawapo ya maamuzi tutakayofanya, kwa sababu wakati watu wawili wanaoana, hushikana na kuwa mwili mmoja kwa uhusiano ambao Mungu anaunuia uwe wa kudumu na usiovunjika (Mwanzo 2:24; Mathayo 19:5).
Swali: “Ni udogo gani ni umri mdogo sana kuwa katika uhusiano wa kimapenzi?”
Jibu: Ni udogo gani ni ” umri mdogo sana” kuanza uhusiano wanategemea ngazi za ukomavu wa mtu binafsi, malengo, na imani. Mara nyingi, wachanga tulivyo, tumepungukiwa ukomavu kutokana na ukosefu wa uzoefu wa maisha. Wakati tunaanza tu kufikiri sisi ni nani, huenda tusiweze kuwa na msingi madhubuti wa kutosha kiroho kuwa na hisia imara kimapenzi na inaweza pelekea kufanya maamuzi yasiyo ya hekima ambayo yanaweza kutuacha uharibifu wa hisia, kimwili, kisaikolojia na kiroho.
Kuwa katika uhusiano unamweka moja katika majaribu ya mara kwa mara, hasa kama hisia zinapoanza kujijenga na uvutio kwa mtu mwingine unapozidi kuongezeka. Vijana- wadogo na hata wakubwa wanahimiswa na homoni na shinikizo la kijamii ambayo wakati mwingine inaonekana kuwa ngumu. Kila siku huleta hisia mpya -mashaka, hofu, na kuchanganyikiwa pamoja na furaha na bashasha-ambayo inaweza kuwa na utata sana. Vijana hutumia muda wao mwingi kufikiria wao ni nani na jinsi wanaweza kuhusiana na dunia na watu wa karibu nao. Kuongeza shinikizo la uhusiano katika umri huu yanaonekana kuulizwa sana, hasa wakati mtu mwingine anakabiliwa na mageuzi hayo. Mahusiano hayo ya mapema huifanya vigumu zaidi kuepuka uharibifu wa picha ya kibinafsi inayojijenga, sembuse tatizo la kupinga majaribu. Kama wazo la ndoa lenyewea bado liko mbali, pengine ni mapema mno kuanza uchumba. La salama sana kwa wote wanaohusika ni shughuli za vikundi ambapo vijana wanaweza kukuza mbinu za kijamii na urafiki bila shinikizo na matatizo ya asili ya mihemko ya kimapenzi.
Haijalishi ni wakati mtu anaamua kuanza uhusiano wa kimapenzi, huu inapaswa kuwa wakati wa kujenga msingi wa imani ambao yeye au wao wamekuwa wakifundishwa, wa kukua na kuwaza ni nini Mungu anawahitaji kufanya. Sisi ni kamwe sio wadogo sana kwa kuanza mchakato huu wa kusisimua. “Mtu awaye yoe asiudharau ujan wako, bali uwe kielelezo kwao waaminio, katika usemi na mwenendo na katika upendo na imani na usafi” (1 Timotheo 4:12).

Swali: “Ni wakati ni wakati gani muafaka wa kuoa?”
Jibu: Wakati muafaka kwa ajili ndoa ni tofauti kwa kila mtu na wa kipekee kwa kila hali. Ngazi za ukomavu na uzoefu wa maisha ni kigezo tofauti; watu wengine huwa tayari kwa ndoa kuanza miaka 18, na baadhi kamwe hawako tayari kwa ajili yake. Kiwango cha talaka Marekani kinapozidi asilimia 50, ni dhahiri kwamba sehemu kubwa ya jamii yetu haioni kuona ndoa kama ahadi ya milele. Hata hivyo, huu ni mtazamo wa dunia, ambao kwa kawaida huitilafiana na wa Mungu (1 Wakorintho 3:18).
Msingi imara ni muhimu kwa ajili ya mafanikio ya ndoa na lazima uanzishwe kabla ya mmoja kuanza kuchumbia mpenzi. Mwenendo wetu wa kikristo lazima uuzishwe na mengi zaidi mbali na kuhudhuria kanisa tu siku ya Jumapili na kuhusika katika kujifunza Biblia. Ni lazima tuwe na uhusiano binafsi na Mungu ambao unakuja tu kupitia kwa kuamini katika na kumtii Yesu Kristo. Ni lazima tujielimishe wenyewe kuhusu ndoa, kutafuta mtazamo wa Mungu juu yake, kabla ya kujiingiza ndani. Mtu lazima ajue ni nini Biblia inasema kuhusu upendo, ahadi, mahusiano ya kingono, jukumu la mume na mke, na matarajio yake kabla tujiingize katika ndoa . Kuwa na angalau maharusi Wakristo kama mfano wa kuigwa ni muhimu pia. Wanandoa wakomavu wanaweza kujibu maswali kuhusu yale yanayoendelea ndani ya ndoa na mafanikio, jinsi ya kujenga urafiki (zaidi wa kimwili), jinsi imani ni mchango mkubwa sana, nk
Wanaotazamiwa kuwa wanandoa pia wanahitaji kuhakikisha kwamba wao wanajuana vizuri sana. Wanapaswa kujua maoni ya kila mmoja kuhusu ndoa, fedha, mashemeji, ulezi wa watoto, nidhamu, majukumu ya mume na mke, kama ni mmoja tu au ni wote wawili watafanya kazi nje ya boma, na kiwango cha ukomavu kiroho cha mwingine. Watu wengi huolewa kwa kuchukua maneno ya mpenzi wao kuwa yeye ni Mkristo, na kugundua baadaye kwamba ilikuwa tu huduma ya mdomo. Kila wachumba wanauia ndoa wanatakiwa kwendea ushauri kwa mshauri nasaha Mkristo wa ndoa au mchungaji. Kwa kweli, wachungaji wengi hawawezi funganisha harusi isipokuwa wamekutana mara kadhaa na wachumba katika mazingira ya ushauri nasaha.
Ndoa ni si kujitoa tu pekee, bali ni agano na Mungu. Ni ahadi ya kubaki na huyo mtu mwingine maisha yako yote yanayosalia, haijalishi kama mpenzi wako ni tajiri, masikini, wa afya, mgonjwa, mnono, mkonde, au wa kuchosha. Ndoa ya kikristo inafaa kuvumilia kila hali, ikiwa ni pamoja na mapigano, hasira, uharibifu, maafa, huzuni, uchungu, madawa ya kulevya, na upweke. Ndoa kamwe haipaswi kuingiwa na wazo kwamba talaka ni chaguo- sio eti ni jambo la mwisho. Biblia inatuambia kwamba kwa njia ya Mungu mambo yote yanawezekana (Luka 18:27), na bila ya shaka ni pamoja na ndoa. Kama wanandoa hufanya uamuzi mwanzoni kukaa na kujitolea na kumweka Mungu kwanza, talaka sio suluhisho ili kuepukika hali mbayai.
Ni muhimu kukumbuka kwamba Mungu anataka kutupatia tamaa za moyo wetu, lakini hiyo in inawezekana tu kama tamaa zetu zinaingiana na zake. Mara nyingi watu huolewa kwa sababu “inahisika vizuri.” Katika hatua za mwanzo wa uchumba, na hata wa ndoa, unaweza kuona mtu mwingine anakuja, na unapta tumbo joto. Mapenzi ni kilele chake, na unajua hisia ya kuwa “katika upendo.” Wengi wanatarajia kuwa hisia hii itabaki milele. Ukweli ni kwamba haibaki. Matokeo yanaweza kukatisha tamaa na hata talaka hisia hizo zinapoisha, lakini wale walio katika ndoa na mafanikio hujua kwamba msisimko wa kuwa na mtu mwingine hauna mwisho. Badala yake, vitumbo joto hutoa njia ya upendo zaidi, ahadi nguvu, msingi imara zaidi, na usalama madhubuti.
Biblia ii wazi kwamba upendo hautegemei hisia. Hii ni dhahiri wakati tunaambiwa kuwapenda maadui zetu (Luka 6:35). Upendo wa kweli unawezekana tu wakati tunaruhusu Roho Mtakatifu kufanya kazi ndani yetu, kuzalisha matunda ya wokovu wetu (Wagalatia 5:22-23). Ni uamuzi sisi hufanya kila siku wa kujifia na ubinafsi wetu, na kumruhusu Mungu uangaze ndani yetu. Paulo anatuambia jinsi ya kuwampenda wengine katika 1 Wakorintho 13:4-7: “Upendo huvumilia, hufadhili; upendo hauhusudu; ;upendo hautakabari; haujivuni; haukosi kuwa na adabu; hautafuti mambo yake; hauoni uchungu; hauehesabu mabaya; haufarahii udhalimu bali hufurahi pamoja na kweli ni; huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahiimili yote.” Wakati sisi tu tayari kumpenda mtu mwingine kama 1 Wakorintho 13:4-7 inaeleza huo ndio wakati muafaka wa kuoa.




Comments

Post a Comment

Popular Posts